Samaki mkunje angali mbichi

Head Gelo

Head Gelo

Member
Joined
Oct 7, 2018
Messages
80
Likes
139
Points
40
Head Gelo

Head Gelo

Member
Joined Oct 7, 2018
80 139 40
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?? Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

#WazAzi fundisheni watoto nidhamu si inglishi
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
13,306
Likes
20,908
Points
280
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
13,306 20,908 280
Hahahahaa nimecheka japo ndio wazazi wengi wa sasa hulea watoto wao hivo, na watoto wenyewe wakishaona wageni au watu sifa hua mara mbili
 
beevenom

beevenom

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Messages
218
Likes
247
Points
60
beevenom

beevenom

JF-Expert Member
Joined May 1, 2017
218 247 60
Uncle umenivunja mbavu bure yaan
 
madindigwa

madindigwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2017
Messages
539
Likes
441
Points
80
madindigwa

madindigwa

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2017
539 441 80
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.
Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.
Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?? Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.
Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".
Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".
Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.
Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!
#WazAzi fundisheni watoto nidhamu si inglishi
Safi sanaa nimecheka peke yangu huu uzungu bwana
 
R

Rotomoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Messages
483
Likes
553
Points
180
R

Rotomoto

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2017
483 553 180
Nimecheka kama mwehu yaani hawa junia hawatakiwi kufanyiwa mambo ya kwenye luninga
 
G

Grahnman

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Messages
1,642
Likes
1,889
Points
280
G

Grahnman

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2017
1,642 1,889 280
Huu uzi ulishawahi kuletwa humu ila saizi hapo mwanzo umekuwa edited kidogo
 
S

silent lion

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
577
Likes
142
Points
60
S

silent lion

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
577 142 60
The problem with kids this days, they dont stay kids very long
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
5,037
Likes
4,619
Points
280
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
5,037 4,619 280
aisee mkuu saafii sana
 
Old story

Old story

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Messages
791
Likes
654
Points
180
Old story

Old story

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2018
791 654 180
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?? Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

#WazAzi fundisheni watoto nidhamu si inglishi
Umenikumbusha ile baba anajamba mtoto analipa na mtoto anajamba baba analipa
Siku mtto kajamba mbele ya babu zake anililia baba alipe ohoooo hapo ndo utaju nani atamfunga paka kengele
 
N

ngakotecture

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2014
Messages
1,011
Likes
592
Points
280
N

ngakotecture

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2014
1,011 592 280
Hahhahahhah kidude kijunia long live jf
 
General Galadudu

General Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2015
Messages
1,457
Likes
1,062
Points
280
General Galadudu

General Galadudu

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2015
1,457 1,062 280
Hiyo ilinifurahisha sana nilipoisoma kwa mara ya kwanza kwenye blog ya cheka na kitime......lakini pia nimefurahi kuiona tena hapa
 
Forum statistics

Threads 1,237,552
Members 475,552
Posts 29,293,044