samaki Aina ya GOGO

Gogo yupoje huyo.
Hawa samaki ziwa victoria nadhani walishapotea mara ya mwisho niliwaona miaka ya 80, GOGO, NINGU, SOGA, Wengine niwataje kwa majina ya kilugha kama NEMBE, NGELE hizo jamii zote kwa maeneo ya ziwa ukanda Musoma, Mwanza na UKEREWE hawapatikani tena sijui kwa upande wa BUKOBA. Gogo simjui kwa jina lingine zaidi ya hilo,
 
Ahsante kwa maelezo HAYA mkuu
Huna hata picha ya mitandaoni?
NINGU, SOGA, NEMBE, NGELE hawa wanapatikana hapa ukerewe ila kwa nadra sana
 
GOgogo ni wa ziwa victoria.
Ni watamu sana hasa wakiwa na mafuta na mayai.
Anafanana na mumi lakini pale kwenye ndevu za mumi yeye ana mifupa miwili migumu (mmoja kila upande).
Wanapendeza zaidi wakipikwa mchemsho.
Wanapatikana zaidi visiwani kama ukerewe
 
Mwaka 2022 nilibahatika kumpata Ningu kutoka fresh water, alikua mkubwa, kichwa tulimla supu, kiwiliwili mboga. Mpaka leo sijabahatika kumpata tena, ni Adimu mno.
Ni mtamu sana.
 
Mmmh hawa morogoro kipindi cha mvua tulikuwa tunawavua kwenye vimito vidogovidogo kwenye matope, nahisi ni jamii ya kambale, tulikuwa tunawaita helicopter. Huyu ukimla mfupa wake unatakiwa uuchome moto, otherwise ukiukanyaga shughuli unayo, kwanza unakama msumeno hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…