Sam Mahela sasa ndani ya TBC1

Leo katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku nimemuona mshikaji aki report kutoka TBC1

Mshikaji sasa kapotea wazi wazi.
Kwa mtu ambaye ameshafanya kazi media za Bongo sidhani kama anaweza mlaumu Sam kama unavyofanya wewe.Licha ya kuwa ni mtangazaji Mahela pia ni baba wa familia.Maisha ya Media Tanzania yanajulikna...mfano ile TV ya kanda ya ziwa unaweza ukakaa miezi 5 hujalipwa,sasa ukiitwa TBC ambako mshahara 95% ni uhakika unaanzaje kukataa?
 
Ni ukweli usiopingika kwamba ITV imekuwa ikitoa watangazaji mahiri lakini pia ni ukweli usiopingika kwamba huenda pia maslahi hayakua mazuri na ndio maana unaona wimbi kubwa la wao kuhamia vituo vingine. Nani asiyependa maisha mazuri?
Unatoka FEZA school unaenda kufundisha Tandahimba Kayumba school eti kisa ni ajira ya uhakika !
 
unaweza kuta ana malengo yake. kuna yule dada anaitwa Vumilia Mwasha alikuwa anatangaza habari za biashara itv pia aliamia tbc
 
Inasemekana ajira za serikali zina security ya kazi. Labda kaona bora aende kupata huo usalama.
Security ilikua enzi hizo.
Nowadays hio kitu hamna kabisa. Tumbua tumbua hii haitawaacha salama wasiowajibika! Wenzao akina Fatma Almasi na Rehema Salim wanaenda Azam tv (digital), wao wanarudi analog (TBC1)
 
Atalikuta li Gabriel Zakaria huko cha moto atakiona, aende amwulize Barwaan Muhuza!!
Gabriel Zakaria alikuwaga Star tv kabla ya kuja TBC, vp jamaa ni mnoko au?
 
Security ilikua enzi hizo.
Nowadays hio kitu hamna kabisa. Tumbua tumbua hii haitawaacha salama wasiowajibika! Wenzao akina Fatma Almasi na Rehema Salim wanaenda Azam tv (digital), wao wanarudi analog (TBC1)
Ok
 
Kwahiyo ITV ndio wanalipa vizuri?
 
Hadi umejadili humu jua kuna mtu kamuona kupitia TBC1, so ulitaka aende TV unayoangalia wewe?

Mfano mimi habari naangalia Azam TWO, lakini kuna wengine wanaangalia ZBC, etc. Muhimu apate mshahara wa kuendesha maisha yake
 
anafikiri huko atateuliwa ukuu wa wilaya ha ja ja
 
Sio yeye tu hata belinda semmtandi sijui na yule sami sago wangepita kwenye interview tungewaona pale TBC .Watz wengi ni wachawi sana sijui mlitakaje?
 
Acheni unafki Kila mtu anapofanya kazi anaangalia Maslahi yake binafsi pengine Huko Itv hakuwa na mkataba Wa kudumu. Watu mshaingiza siasa duh.......
Umesema kweli mkuu..tatizo wengine wanaangalia kwenye nyanja za umaarufu labda na ndio tatizo sugu tulilonalo kwa kuenda kazi zenye attention alafu wanaacha kazi nzuri ambazo hazina attention kwenye jamii ila zina hela za kutosha kabisa bila zengwe
 
Umesema kweli mkuu..tatizo wengine wanaangalia kwenye nyanja za umaarufu labda na ndio tatizo sugu tulilonalo kwa kuenda kazi zenye attention alafu wanaacha kazi nzuri ambazo hazina attention kwenye jamii ila zina hela za kutosha kabisa bila zengwe
Kabisa Mkuu na wengi wenye Akili hiyo ni vijana ambao bado wanalishwa kwao Au anasubir bum litoke afanyie nalo Laana bado Hawajajua maisha vizuri. Km mtu Unayejitafutia ugali wako mwenyewe huwezi mshangaa jamaa Kwa maamuzi aliyoyachukua. Bora mtu usiwe maarufu lakini bank balance inasoma kuliko umaarufu njaa ambao watanzania wengi ndio wanao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…