Saluti kwako Lema: Zitto, Kitila na Mwigamba walitaka kugeuza CHADEMA tawi la CCM

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Nampa saluti Mh. Godbless Lema aliyepambana kuhakikisha kuwa Mwigamba anadhibitiwa wakati wa mkutano wa CHADEMA na laptop yake ikadukuliwa ili kuonyesha mipango ovu ya Mwigamba, Zitto na Kitila kutaka kuigeuza CHADEMA kutoka chama kikuu cha upinzani na mtetezi wa wananchi kuwa tawi la CCM.

Mipango ya wasalitii ilikuwa na nia ya kudhoofisha harakazi za kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa “mkoloni” mweusi CCM na kuwapatia uhuru na maendeleo ya kweli wananchi wa Tanzania.

Juhudi za Lema zimesaidia wasalitii hao kugundulika na kujiunga rasmi na CCM kupitia tawi lao la ACT-Wazalendo. Kama isingekuwa ujasili wa Lema, leo hii
CHADEMA ingekuwa tawi la CCM, kama ilivyo ACT-Wazalendo.

Sasa ni wajibu wa UKAWA na CHADEMA kupanda majukwaani kwa nguvu zote ili kuwafahamisha wananchi wengi wa Tanzania kuwa
ACT-Wazalendo ni tawi la CCM wala siyo chama cha upinzani.

Itakuwa kosa kubwa ikiwa UKAWA na Chadema watachulia poa propaganda za
ACT-Wazalendo kuwa ni chama cha upinzani kumbe ni tawi la CCM.

UKAWA na CHADEMA watumie nguvu ileile waliyotumia kuwaelezea wananchi kuhusu uzuri wa rasmu ya pili ya katiba ya Warioba, na ubaya wa rasmu ya CCM yaani katiba pendekezwa, kuwaeleza kuwa
ACT-Wazalendo ni CCM, na kwamba vyama vya upinzani ni CHADEMA na umoja wa UKAWA.

Wasipofanya hivyo, upotoshaji wa
ACT-Wazalendo utaendelea na CCM watahuishwa na ACT-Wazalendo, na inaweza kuwafanya UKAWA na CHADEMA kutumia nguvu kubwa zaidi baadaye kuondoa upotoshaji wa ACT-Wazalendo kuliko kama wakifanya mikutano sasa kuwaeleza wananchi rangi halisi ya ACT-Wazalendokuwa ni tawi la CCM.
 
Siyo wote mkuu hasa wa vijijini ambako hamna vyanzo vya kutosha vya habari.

Ni kweli maana hapa Dar,watu ni wajanja sana hawataki kusikia CCM wala CUF(CCM B),NCCR-Mageuzi(CCM B)Wanaipenda CHADEMA Tu na majimbo yote WAMECHUKUA maana wamejitambua kama watu wa KILIMANJARO/ARUSHA kule ambako majimbo yote ni CHADEMA.CHADEMA Oyeeeeee!Watu wa vijijini hawajui chochote mfano huko kwa WASHAMBA Kigoma majimbo yote ni CCM.
 
mmmmh siongei sana kuhusu ACT maana nimekula burn za kutosha, hata sijui kola langu ni lipi. Mods wame nifundisha kitu, na nimeijuwa rangi yao. Mungu ibariki tanzania.
Unakumbuka Mh. Tundu Lissu alivyomwambia Mnyika mbunge wa Ubungo, pamoja na mkosamali kuwa siyo vizuri kukata tamaa katika mapambano ya kuikomboa nchi. Leo hii Afrika ya kusini ingekuwa bado chini ya ubaguzi wa rangi kama akina Mandela wangekata tamaa. Maana walikuwepo wasalitii walioungana na makaburu lakini haikuwakatisha tamaa wapambanaji na misemo yao ya Umkonto we Sizwe kupinga ubaguzi wa rangi. Uwe kama Mandela usikate tamaa, uhuru kamili kutoka mikononi mwa CCM na vibaraka wake, utapatikana tu.
 
mmmmh siongei sana kuhusu ACT maana nimekula burn za kutosha, hata sijui kola langu ni lipi. Mods wame nifundisha kitu, na nimeijuwa rangi yao. Mungu ibariki tanzania.

Hata mimi nimejifunza kitu ....."CCM kumbe ni wavumilivu sana"
 
Mkuu,,nadhani watz wangependa kujua ni jinsi gani ukawa wanaweza kuwaondoa kwenye umaskini. Ukawa waeleze nini agenda yao wakipewa nchi.
 
Kama ilivyo jina lako unajitahid kustabilize upepo na kimbunga kikali cha Act dhidi ya chadema.

Upepo upi hivi unawajua vizuri watanzania wa leo au umeamua tu kujitoa ufahamu a.c.t ikipata hata wabunge wawili mwaka huu nahama nchi.
 
Mkuu,,nadhani watz wangependa kujua ni jinsi gani ukawa wanaweza kuwaondoa kwenye umaskini. Ukawa waeleze nini agenda yao wakipewa nchi.
Yote yanatakiwa kwenda pamoja. Uaona CCM wanavyotumia mbinu lukuki kubaki madarakani. Wanatumia bunge, wanatumia bunge la katiba, wanatumia ukabila, udini, polisi, mahakama, vyama vya siasa vinavyoanzishwa na kufadhiliwa na CCM kama hiki cha ACT. UKAWA na Chadema wanatakiwa pia kutumia (a combination of strategies) njia tofauti za kuwaelemisha wananchi ikiwemo kuwaeleza kuwa CCM ni ACT na ACT ni CCM.
 
Mkuu,,nadhani watz wangependa kujua ni jinsi gani ukawa wanaweza kuwaondoa kwenye umaskini. Ukawa waeleze nini agenda yao wakipewa nchi.

UKAWA watasema agenda yao soon .Maana kwa mujibu wa NEC bado mambo ya Kempeni maana hata CCM agenda yao bado anayo Wassira sasa kuwa mvumilivu
 
Unakumbuka Mh. Tundu Lissu alivyomwambia Mnyika mbunge wa Ubungo, pamoja na mkosamali kuwa siyo vizuri kukata tamaa katika mapambano ya kuikomboa nchi. Leo hii Afrika ya kusini ingekuwa bado chini ya ubaguzi wa rangi kama akina Mandela wangekata tamaa. Maana walikuwepo wasalitii walioungana na makaburu lakini haikuwakatisha tamaa wapambanaji na misemo yao ya Umkonto we Sizwe kupinga ubaguzi wa rangi. Uwe kama Mandela usikate tamaa, uhuru kamili kutoka mikononi mwa CCM na vibaraka wake, utapatikana tu.
Day Dreams.....!!!
 
Kama ilivyo jina lako unajitahid kustabilize upepo na kimbunga kikali cha Act dhidi ya chadema.

ni kweli kabisa mkuu. tusipostabilize mambo sasa tutakuja kulipa gharama kubwa sana kukanusha upotoshaji unaofanywa na ACT. saa ya kuweka mambo sawa ni sasa.
 
UKAWA watasema agenda yao soon .Maana kwa mujibu wa NEC bado mambo ya Kempeni maana hata CCM agenda yao bado anayo Wassira sasa kuwa mvumilivu
Nakubaliana na wewe ila kazi za kuimarisha Chadema na UKAWA ni kazi endelevu ya vyama vya siasa inabidi iendelee, ikiwemo kuwadadavulia wananchi kuwa ACT ni mkono wa CCM.
 
Ni kweli maana hapa Dar,watu ni wajanja sana hawataki kusikia CCM wala CUF(CCM B),NCCR-Mageuzi(CCM B)Wanaipenda CHADEMA Tu na majimbo yote WAMECHUKUA maana wamejitambua kama watu wa KILIMANJARO/ARUSHA kule ambako majimbo yote ni CHADEMA.CHADEMA Oyeeeeee!Watu wa vijijini hawajui chochote mfano huko kwa WASHAMBA Kigoma majimbo yote ni CCM.

mbona povu, umeyatutika nini?
 
Back
Top Bottom