Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Nyankumbu, mkoani Geita, Septemba 16, 2025 alisema Mpambano uliopo kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) uchaguzi wa mwaka huu Oktoba 2025 ni wa Mustakabali wa Maisha yetu na siyo kama Mchezo wa Simba na Yanga ambayo ni burudani tu
"Hata ikishinda haikuletei chakula utasononeka wee lakini haikuletei chakula, Simba itashinda tutafurahi haituletei mkate nyumbani, haituletei sukari nyumbani ni burudani tu. Lakani Mpambano wa CCM na CHAUMMA siyo burudani ni Mpambano wa Mustakabali wa Maisha yetu, wa kuchagua njia gani tunataka twende miaka mitano tunataka tuwe wapi kama Taifa, tujiulize, vijana wenzangu tujiulize" amesema Salum Mwalimu