GE2025 Salum Mwalimu mgombea urais na Devotha Minja mgombea mwenza kupitia CHAUMMA

GE2025 Salum Mwalimu mgombea urais na Devotha Minja mgombea mwenza kupitia CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimemteua Salum Mwalimu kugombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025.

Salum alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar kabla ya kuhamia CHAUMMA.

1754573743750.png

Wakuu,

Leo ndo tutajua nani atachaguliwa na CHAUMMA kuwa mgombea wake wa Urais.

Kumekuwa na tetesi kuwa baada ya kutuma wanae, leo Mwamba ndo ataibuka rasmi kwenye chama hicho na huenda akachaguliwa kuwa mgombea Urais

Kaeni karibu na uzi huu kujua nini kitajiri

===================================

Kinachoendelea Chaumma Mlimani City Dar

Ni wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) wakisalimiana na kujadiliana katika makundi kwenye Ukumbi wa Malimani City, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Agosti 7, 2025.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utapokea na kupitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025/2030 na kuchagua au kumthibitisha mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar.

chaumma.png

View: https://www.youtube.com/watch?v=DBvaWPPGArE

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mhe. Hashimu Rungwe amewasili katika ukumbi wa Mlimani City katika Mkutano Mkuu wa CHAUMMA Kuteua Mgombea Urais wa chama hicho.

Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo ambaye pia mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mwanga bwana Lawrence Mchome katika Mkutano Mkuu wa CHAUMMA Kuteua Mgombea Urais wa CHAUMMA

Mrema kuhusu ilani ya chama

"Mrema amesema kuwa CHAUMMA kwenye ilani yake imezingatia kikamilifu mahitaji ya watu wenye ulemavu kwahiyo ilani yetu itakapotoka tunaomba muipitie"

Maduu Wiliam kilio kikubwa cha Asasi za kiraia ni ulinzi wa haki za binadamu

Ndugu Maduu Wiliam kwa niaba ya kituo cha sheria na haki za biandamu akitoa salamu katika mkutano wa CHAUMMA Amesema kilio kikubwa cha Asasi za kiraia ni ulinzi wa haki za binadamu kwa nguvu zote na ulinzi wa utawala wa sheria.

Lawrence Mchome kuhusu naibu Mwenyekiti wa CHADEMA

akiwa nje ya Ukumbi mwakilishi wa CHADEMA kwenye mkutano wa CHAUMMA Lawrence Mchome amesema kuwa amejaribu sana kumshauri Heche lakini kiongozi huyo hashauriki.

Chama cha Ukombozi wa umma CHAUMMA kimemchagua Salum Mwalimu kuwa mgombea urais

Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA kimemtangaza Salum Mwalim Juma kuwa Mgombea wao wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Hayo yamejili leo hii katika mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea mda huu katika ukumbi wa Mlimani City.
1754572700724.png

Attachments

  • 2025-08-07 12-58-42.mp4
    22.6 MB
Wakuu,

Leo ndo tutajua nani atachaguliwa na CHAUMMA kuwa mgombea wake wa Urais.

Kumekuwa na tetesi kuwa baada ya kutuma wanae, leo Mwamba ndo ataibuka rasmi kwenye chama hicho na huenda akachaguliwa kuwa mgombea Urais

Kaeni karibu na uzi huu kujua nini kitajiri

===================================

Kinachoendelea Chaumma Mlimani City Dar

Ni wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) wakisalimiana na kujadiliana katika makundi kwenye Ukumbi wa Malimani City, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Agosti 7, 2025.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utapokea na kupitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025/2030 na kuchagua au kumthibitisha mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar.

View attachment 3434743

View: https://www.youtube.com/watch?v=DBvaWPPGArE
View attachment 3434805

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mhe. Hashimu Rungwe amewasili katika ukumbi wa Mlimani City katika Mkutano Mkuu wa CHAUMMA Kuteua Mgombea Urais wa chama hicho.
View attachment 3434821
Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo ambaye pia mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mwanga bwana Lawrence Mchome katika Mkutano Mkuu wa CHAUMMA Kuteua Mgombea Urais wa CHAUMMA

takataka...aibuk asiibuke shauri lake....takataka
 
Mbowe ni muasisi wa Chadema. Hawezi kukihama. Mgombea atakuwa Mwenyekiti wa Chaumma.

Amandla...
 
Ila Mbowe atawaunga mkono na kuwasaidia wagombea wa Chaumma na ACT-WAZALENDO. Hamna conflict of interest kwa sababu Chadema haitashiriki kwenye uchaguzi.

Amandla....
 
Miaka ya nyuma mikutano kama hii ya CHAUMMA hakuna aliyefuatilia, ghafla wamekuwa umaarufu.

Hata Man City kabla ya kununuliwa na waarabu haikuwa maarufu. Kinachoifanya iwe maarufu ni CHADEMA, ni kama ACT ya Zitto 2014/2015
 
Baada ya Kamanda Mbowe kuchomoa rasmi sasa Salum Mwalim ateuliwa kuwa mgombea Urais wa Chaumma.
 
Chama cha CHAUMMA kimempendekeza Salum Mwalimu kugombea Urais wa Jamhuri kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
FB_IMG_1754572279698.jpg

Source:NipasheDigital
 
Back
Top Bottom