Salome: Diamond Platnumz ft Rayvanny - General Views

Video ni ya studio zaidi angeifanya na mazngra ya nje kidogo vimsonge vile, tumkimbizano twa vichakani ingenoga mara mia yake, ila kitu kikali hadi aibuuuuu
 
Hii ngoma ni kali mno...Tulitegemea ule nisamehe wa Baraka na Ali ungekuwa mkali ila walituangusha wale jamaa...Diamond anajua kutumia nafasi kwa hili dude majamaa wamekuja kuivunja vunja Nisamehe.

Ila inaniuma kusema hivi maana mapenzi yangu kwa King Kiba ni makubwa mno ila Hapa no naacha unafiki.

Raymond ni nyokoo huyu mtoto...kwa mtazamo wangu kamfunika Boss wake kwenye hii ngoma.

[HASHTAG]#TeamKariakoo[/HASHTAG]
 
Ila wimbo wame cover wa Saida Karoli, kama hawakuelewana kuna kesi hapa.

Hii hata si sampling, hii ni cover version.

Huu wimbo wa Saida Karoli kila mtu anayefuatilia muziki anajua, mpaka kuna movie moja ya Kimarekani ya Tyler Perry inaitwa "Peeples" umepigwa kama soundtrack.
 
Reactions: MC7
Mavazi ya kitanzania yakoje?
Ina maana hujui mavazi ya makabila ya Kitanzania?? Ingawa hatuna vazi rasmi khanga, rubega, kaniki, vitenge vingeweza kutuwakilisha zaid kuliko hizo less na Kente za West Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…