Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Na Heckton Chuwa, Moshi
MKE wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete amesema anawajibika kumkampenia mumewe kwa kuwa yeye ni msaidizi mkubwa wa rais katika masuala ya kimaendeleo.
Mama Salma aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na wanawake wa Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, ambapo pamoja na mambo mengine alimnadi Rais Kikwete, mgombea ubunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, Bw. Justin Salakana na wagombea wote wa udiwani wa manispaa ya Moshi kwa tiketi chama hicho.
"Mimi kama mwenzi wa Rais ni msaidizi wake mkubwa katika masuala ya maendeleo ya kijamii kupitia taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na huu ni utaratibu wa kimataifa ambapo wenzi wa viongozi hufanya kazi za kijamii," alisema.
Mama Salma ambaye ameshutumiwa na wapinzani kwa kutumia raslimali za serikali kumkapmeni mumewe, aliendelea kusema kuwa taasisi ya WAMA imechangia masuala mengi ya kimaendeleo, yakiwemo kuwasomesha watoto yatima na wasio na uwezo wa kuchangia eimu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila ubaguzi wa aina yoyote.
"Hata hapa Kilimanjaro mna watoto ambao taasisi hii imewachangia katika elimu na tayari wapo ambao watahitimu kidato cha nne mwaka huu na zaidi ya haya tumeanzisha shule kule Rufiji iitwayo WAMA na KAYAMA na ambayo ina watoto kutoka kila sehemu hapa nchini," alisema.
Aidha alisema taasisi hiyo ya WAMA pia imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuwaendeleza wajasiriamali mbalimbali hususan akina mama jambo ambalo limewasaidia kuinua hali zao za maisha.
Kuhusu kampeni zinazoendelea, Mama Salma aliwataka wanaCCM kuepuka kampeni za matusi na kashfa na badala yake wanadi sera za chama hicho tawala.
Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, Bi. Mwantumu Mahiza, alisema ataweka kambi katika jimbo la Moshi Mjini ili kuhakikisha linampata mbunge kwa tiketi ya CCM.
"Wenzangu wa Moshi Mjini mmemkwaza Rais Kikwete kwa kumchagua mtu ambaye si rahisi kufanya naye kazi kutoka jimbo hili la Moshi Mjini, jamani mwaka huu badilikeni," alisema.