Sally/Sarah Mugabe, mke wa kwanza wa Robert Mugabe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Sally_Hayfron.jpg

Sarah Francesca (Hayfron) Mugabe alizaliwa tarehe 6, June 1931 na alifariki tarehe 27 Janurary 1992. Alijulikana kama Sally Mugabe na alikuwa mke wa kwanza wa Robert Mugabe rais wa Zimbabwe kuanzia 1987 mpaka wakati wa kifo chake 1992 alikuwa First Lady wa Zimbabwe. Wazimbabwe walimuita Amai maana yake Mama.

Alizaliwa 1931 Ghana wakati huo wakoloni wa-Ingereza waliita Gold Coast, Sally na pacha wake Esther walikulia katika familia ya wanasiasa, katika mhemuko wa siasa za uzawa ndani ya Gold Coast chini ya ukoloni. Alikwenda shule ya Seconday Achimota baadae chuo kikuu alikosomea shahada ya ualimu.

Alikutana na mchumba wake ambae alikuja kuwa mume wake Robert Mugabe nchini Gold Coast (Ghana) katika Chuo cha Ualimu Takoradi ambako wote walikuwa wanafundisha, alimfuata Robert Southern Rhodesia ambayo ndiyo Zimbabwe ya leo na ndoa yao ilifungwa mjini Salisbury mwezi April 1961.

Mwalimu aliyelinda nafasi yake kama mwanasiasa na mpigania haki, Sally aliongoza maandamano ya wanawake wa ki-Afrika kupinga utawala wa kimabavu Rhodesia ya Kusini. Alikutwa na hatia na alihukumiwa kufungwa jela miaka mitano ingawa hakumaliza kifungo chote.

Mwaka 1967, Sally aliomba ukimbizi London na aliishi Ealing Broadway, Magharibi ya London; ukaaji wake nchini Uingereza ulifadhiliwa na British Ariel Foundation hii ni charity iliyoanzishwa 1960. Charity hii ilishirikiana kwa karibu sana na serikali ya Uingereza ambayo iliona elimu ya juu Uingereza kama ni njia ya kuwashawishi kizazi kijacho cha viongozi wa Afrika. Alitumia miaka nane akipigania kufunguliwa kwa viongozi wa ki-Afrika waliowekwa ndani nchini Zimbabwe wakati huo ikiitwa Rhodesia. Mume wake akiwa mmoja wa viongozi hao waliowekwa jela kwa miaka kumi. Mtoto wao wa pekee Nhamodzenyika, ambae alizaliwa 1963 wakati huo baba akiwa gerezani alipata malaria kali sana na alifariki nchini Ghana mwaka 1966. Mugabe hakuruhusiwa kushiriki mazishi ya mtoto wake. Baba yake Sally alifariki 1970.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilijaribu kum-deport mwaka 1970, lakini mume wake akiwa bado gerezani, Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Harold Wilson akishirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuia ya Madola walimpatia haki ya ukazi nchin Uingereza; jitihada hizi zilifanikishwa na mbuge wa Labour Mourice Foley na mfadhili wa Conservative Lord Lothian.

Robert Mugabe aliachiwa kutoka gerezani mwaka 1975 na alifanikiwa kukimbilia Mozambique pamoja na Edgar Tekere, Sally alimfuata mume wake mjini Maputo. Hapa alijijengea taswira kama mama na kiongozi wa maelfu ya wakimbizi wa Vita vya Msituni
vya Zimbabwe na kuanzi hapo alijulikana kama Amai.

1978 alichaguliwa kama katibu msaidizi wa Wanawake wa ZANU-PF. Mwaka 1980 alikuwa na taswira mpya ndani ya nchi kama mke wa Waziri Mkuu wa kwanza Mwafrika nchini Zimbabwe. Rasimi alikuwa mke wa rais wa Zimbabwe mwaka 1987 wakati mume wake alipokuwa rais wa pili wa Zimbabwe pia alichaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Jumuia ya wanawake ya ZANU-PF katika mkutano mkuu wa 1989.

Alianzisha Haki ya mtoto kuishi nchini Zimbabwe. Sally Mugabe alianzisha pia Umoja wa Wanawake wa Zimbabwe ulioitwa Akina Mama wa Afrika, uliokuwa na makao yake mjini London. Umoja huu ulizingatia maswala ya wanawake wa ki-Afrika nchini Uingereza.

Hayfron alifariki January 27, 1992 kutokana na figo kushindwa kufanya kazi. Kaburi lake limewekwa katika sehemu ya mashujaa wa Zimbabwe. Mwaka 2002 katika kuazimisha miaka kumi ya kifo chake, Zimbabwe ilichapisha toleo maalum la stamp, kwa picha zake mbali mbali. Wazimbabwe wanamkumbuka kwa upendo na ucheshi wake na mpaka leo anaheshika kama mama wa Taifa.
sallyrobert.jpg

Siku ya harusi yake na Robert Mugabe

mugabe-and-Sally.jpg

Akiwa na mume wake ndani ya vazi la asili yake kente

hqdefault.jpg

51e001_7b665c9a68434a9590401cbaac7985b2~mv2.jpg
 
Sally_Hayfron.jpg

Sarah Francesca (Hayfron) Mugabe alizaliwa tarehe 6, June 1931 na alifariki tarehe 27 Janurary 1992. Alijulikana kama Sally Mugabe na alikuwa mke wa kwanza wa Robert Mugabe rais wa Zimbabwe kuanzia 1987 mpaka wakati wa kifo chake 1992. Wazimbabwe walimuita Amai maana yake Mama.

kimada ndo kimemponza mgabe,hata mimi ninge stop kuwa na mke hapo
 
Story nzuri ila umekosea kusema alikuwa mke wa Mugabe 1987-1992
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom