Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,460
Habari dada jirani Mwema,
Nakuita jirani mwema kwa kuwa umekuwa ni mwema kwetu, kila siku kuja kuisalimia familia yangu ni upendo wa hali ya juu. Ila nimeijua tabia yako ya kuja kuisalimia familia yangu kumbe haikuwa na nia njema sana kwetu, na ninakueleza kama ifuatavyo:
1) Kumbe umekuwa na tabia ya kupiga picha na gari langu na kwenda kujibandika kwenye mitandao yenu ya kijamii sijui Instagram, Twitter na Facebook na kuandika maneno yenu ya 'Thanks God I Got It' ili watu wakupe hongera huku ukijua wazi kuwa ni uwongo mtupu na si la kwako. Tabia hii imefanya tukiwa na magari yetu mjini watu kufikiri kuwa ni ya kwako kwa kuwa wewe ni maarufu hapa mjini na wakati mwingine hunifuata na kuniuliza ulipo, awali sikujua kwa nini maana sina undugu wala urafiki wa karibu na wewe lakini nimekugundua unatangaza ni lako kupitia kupachika picha kwenye mitandao ya kijamii .
2) Tabia yako ya kupiga picha getini kwetu (naishi mimi na familia yangu) na kuandika kwamba ndo unawasili au ndo unaondoka nyumbani wakati hauishi kwenye nyumba yetu ni ubazazi wa hali ya juu dada jirani mwema. Tafuta nyumba ingine ya kufanya hivyo kwa kuwa picha za nyumba yetu zimejaa sana huko kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii na sasa tuseme imetosha. Na kwa nini usipige kwako? Ridhika na ulichonacho bana
3) Ulichokifanya jana kimeniudhi sana, umekuta watoto wanaosha gari yangu kwa kuwa wamekuzoea ukawalaghai na kupigia picha na simu yako kana kwamba unashuka au unaingia huku umevaa minguo myekundu na ukatoa maua kwenye mikoba ukaweka na kupigia picha as if ni lako na umelipamba kwa ajili ya Valentine na kama haitoshi leo asubuhi sana umezituma mitandaoni kuwawish watu Valentine njema! Kwa nini usipigie picha kwako dada jirani, kama huna omba Mungu na ufanye kazi kwa bidii utapata na wewe?
Najua umekuwa ukitumia fursa ya ujirani kutimiza malengo yako kwani hatukukugundua tabia yako ila baada ya kupata taarifa na kuzifuatilia akaunti zako tumeona live matendo yako yanavyoihujumu familia yangu. Sisi wenyewe hatuna tabia hizo kwa nini wewe utufanyie namna hii?
Kama ni maisha pambana utayapata na si kujifanya unamaisha ya juu kwenye mitandao ya kijamii kumbe maisha yako halisi ni duni sana na kwa kuwa unapretend kuwa nazo hutaweza kufanikiwa kwani unaspend kuliko uvunacho ili kujionesha kwa wenzio.
NB: Nimetumia JF najua ujumbe utakufikia course najua una akaunti huku JF na liwe onyo kwa wote wenye tabia ya kupretend maisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia mali za watu.
Happy Valentine wana JF woote especially wana MMU
Nawasilisha