Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

kiwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
1,341
Reaction score
2,218
Ni mvurugano tu. Mbona makabila hayana hii salamu watu wote wanatumia salamu moja iwe mdogo au mkubwa. Inasemekana hii salamu imetokana na maisha ya utumwa. Kwa nini tumeishikilia kama salamu rasmi ya Kiswahili?

Hivi unajuaje kama mtu uliyekutana nae mara ya kwanza unastahili kumpa shikamoo kwa kumwangalia kwa macho? Ni mtu aliyekuzidi miaka mingapi anastahili hii salamu?

Solution itafutwe salamu moja ya Kiswahili itakayotumiwa na watu wa rika zote kama ilivo salamu za kidini, lugha za kigeni na lugha za makabila yetu. Tuondoe huu mvurugano kwenye jamii. Kama Serikali haina mbadala wa hii salamu itangaze mashindano wananchi wapendekeze mbadala.

C.c. Wizara ya Sanaa na Utamaduni
C.c. BAKITA
C.c. TATAKI
 
Shikamoo ni ujinga na utumwa sijui kwa nini tumeamua kuenzi kitu ambacho hata hakihusiani na tamaduni zetu!? Tuna salamu za makabila yetu ambazo ni nzuri, ni vema tukatafuta salamu ya Kiswahili kutokana na makabila yetu.

Maprofesa wa mambo ya lugha na utamaduni kazi kwenu kuweka mambo sawa. Shikamoo yenyewe haitumiki na hao wageni kama tunavyotumia sisi!
 
Kwa kweli hata wageni ukiwaelezea maana ya shikamoo hawakuelewi wanaona ni bogus kabisa.
Shikamoo ni ujinga na utumwa sijui kwa nini tumeamua kuenzi kitu ambacho hata hakihusiani na tamaduni zetu!? Tuna salamu za makabila yetu ambazo ni nzuri, ni vema tukatafuta salamu ya Kiswahili kutokana na makabila yetu. Maprofesa wa mambo ya lugha na utamaduni kazi kwenu kuweka mambo sawa.
 
Shikamoo ni ujinga na utumwa sijui kwa nini tumeamua kuenzi kitu ambacho hata hakihusiani na tamaduni zetu!? Tuna salamu za makabila yetu ambazo ni nzuri, ni vema tukatafuta salamu ya Kiswahili kutokana na makabila yetu. Maprofesa wa mambo ya lugha na utamaduni kazi kwenu kuweka mambo sawa. Shikamoo yenyewe haitumiki na hao wageni kama tunavyotumia sisi!
Marhaba (jokes)
 
Uamuzi ni wako sio kila kitu uamuliwe na serikali. Kuna kabila wana mambo ya jando mpaka zama hizi, na wengine wanazaliwa mpaka kifo hawajasikia kitu kinaitwa jando.
 
Back
Top Bottom