Salamu kwa 1st year.

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Hii ni kwa wadogo zangu wanaotegemea kuanza kusoma vyuoni.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza kuchaguliwa katika vyuo mbalimbali. Maana ni wengi walitamani kufikia hatua mliyopo ila kutokana na changamoto mbalimbali hawakufanikiwa. Hivyo MNA bahati sana na Mungu ana mipango mikubwa juu yenu kwa ajili ya taiga lenu.

Tofauti na maisha ya secondary, vyuoni ni sehemu ambayo utakuwa huru sana. Hakuna atakaye kuchunga mipaka yako ipo kichwani mwako. Chuoni ni sehemu ambayo utakutana na watu wa kila aina, maskini, matajiri, wenye hekima, wapumbavu, wahuni, wastarabu, n.k.

Kikubwa nawaomba msipende kuiga maisha ambayo hampaswi kuishi. Kuwenu wavumilivu na wenye subira. Msipende kutumia fedha vibaya kwa starehe na anasa. Kumbukeni mlikotoka.

Mkipata fedha kwa ajili ya matunizi ya kila Sikh zitumieni kwa hekima. Jigunzeni kuweka bajeti...ili mtakapomaliza muwe angalau nq pesa hata ya kuanzishia mtaji. Maana siku hizi suala la ajira limekuwa gumu sana.

Jiepusheni na starehe za kijinga. Hili hasa hasa kwa wadogo zangu wa kike. Rizikeni na mlichonacho. Sio lazima kuishi maisha ghali sana na wakati maisha rahisi mnayaweza.

Msijiingize kwenye ngono zembe. Madhara yake ni makubwa kuliko raha yake. UKIMWI bado upo.

Mtangulizeni Mungu katika kila jambo. Ombeeni familia zenu.


NB. Samahani sana kwa kutumia lugha mbaya hapo mwanzo.

Nakuheshimu sana mkuu MLEVi Mmoja . na wengine wote mliochujizwa na lugha hiyo.

Ikifikia hatua MLEVi Mmoja akasema nimekosea. Hakika nimekosea.
BOB OS
lukubuzo Samsis
Shombe la Kisomali
Kastoryalfred
Smart911
ngebo
Esrom makono
mlima wa mizeituni
kurlzawa
Mr Devil
Seneta Wa Mtwiz
 
Kheri humu ndani,

Kuna kipindi kinafika naanzaga kuaminigi kile kisa cha watoto wa Nuhu kumchungulia. Kama ukijui soma kitabu cha Mwanzo.

Ujio wa smsrtphone nchini Tanzania umeendana sambamba na ujio wa ujinga wa kiwango cha juu Tanzania.

Unakutana na litoto la maskini linasoma chuo cha serikali, linalipwa pesa kila baada ya miezi kadhaa...badala ya kusaidia nyumbani hats kidogo. Linanunua Simu Apple (IPhone), Laptop ya ya Apple na kofia ya Apple. Eti linajilinganisha na watoto wa matajiri ambao kwao pesa zipo tele.


Unakutana na lidada jingine, limeenda chuo na nguo za heshima, sketi nzuri na magauni ya heshima. Linakutana na misekandi iya na masedi iya. Makrumbembe yaliyoshindikana, linaanza kuinga maisha ya kishamba waishio watu wa mjini hasa hasa madangaji. Linaishia kupewa mimba na maradhi juu. Eti linaanza na kubagua vyakula na wakati kwao milo mitatu ya maviazi paper la maths.

Kuna baadhi ya majinga, yanakuja JF kulalamika eti maisha magumu na wakati kila siku liko online sijui linazipata wapi hizo hela za kununua bando.

Tufanyeni kazi jamani, majungu na lawama sio issue.
Kama unastress pita tu hata usi comment...ntakushushia....
WANAKUJA KUKUPA MWONGOZO MKUU.
 
Yaaan umetudhalilisha(waswahili, sijui ndo inaandikwa hvyo..) Tunaosoma vyuo vya serikali..

Sasa kama mtu miaka yote nyuma alikuwa anaisikia tu smartphone sijui Apple,, leo hii kapata hela si ananunua namna hyo.. Mbona nyodo jamani
 
"Kuna baadhi ya majinga, yanakuja JF kulalamika eti maisha magumu na wakati kila siku liko online sijui linazipata wapi hizo hela za kununua bando"
unaijua freebasics?
Hahaha labda haijui mpe link hadi kui download ni free pia mwambie..😀
 
Back
Top Bottom