Salaam kwa Mh. Edward Lowassa na wenzake

Maelezo hayo umeshindwa kuleta vilelezo na ushahidi unajitosheleza,pole sana naona unaingia ktk mkumbo ambao mwisho wa siku utakuja kujuta ambapo wenzako utakuta washahesebiwa,wewe na huyo mtangazania wako mnatakiwa kujenga hoja za namna ya kuwasaidia watanzania lakini sio hizo sera za kupakana matope ambazo zimeshachuja na watanzania sasa wanajua ukweli na uongo kwa hizo tuhuma za uongo dhidi ya Lowassa hatudanganyiki kwani sie chaguo letu ni White hair in white house 2015.

Acha kuwa bongo lala hakuna kilichopitwa na wakati lowasa ni mnyonyaji fisadi mkubwa tatizo mshakula vya watu hivyo lazima msifie hata ujinga
 
Mie sina itikadi ya chama yoyote ila namkubali sana Lowassa hapa issue sio kubadili chama bali kubadili mfumo mzima majuzi report ya CAG imeonyesha jinsi chadema walivyoponda ruzuku ya chama halafu unataka niwe chama fulani?mie naitaji mtu mithili ya Kagame na huyo hapa kwetu ni Lowassa tu

wezi wazoefu tu nyie mnatumia jina la mwizi mwenzenu kutuibia. UKAWA yatosha Lowa hasa mwizi wa nini?
 
samahani mkuu , kuuliza si ujinga hivi huyu mzee kisori yuko hai kweli mpaka leo ?
Alisha wahi kutishiwa mara kibao na vibaraka wa mafisadi, lakini walimshindwa! yupo nyumbani kwake Arusha akipumzika! Muulize mkuu Ngongo nadhani ni jirani yake.
 
Nia ya Mzee Kasori hapa ni kuchafua jina la Lowasa ili asipate nafasi ya Urais - period. Kwahiyo strategically kwake huu ni wakati muafaka kuibua tuhuma hizi za Mwalimu za takriban miaka 20 iliyopita potelea mbali kama hakuziibua alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Makala hii ni marudio, ameshaitoa Raia Mwema huko nyuma ila hapa kapachika nukuu ya Bacon ili kuipamba na kuiongezea uzito. Lakini Mwl. Nyerere mwenyewe alisema yeye hakuwa malaika angeweza kukosea kama binadamu mwingine. Sasa kuhusu hizo mali za Lowasa alizozungumzia Nyerere, Mzee Kassori hazitaji, lakini hata akizitaja hatuna ushahidi kuwa Lowasa alizipata kwa njia haramu! Ni kweli Mwalimu aliwachukia sana viongozi wanaopenda mali, lakini ni ukweli pia kwamba kwa msimamo huu he was in the tiny minority. Watanzania wengi na viongozi wote wanapenda mali. Nina imani majority of current CCM and government leaders are milllionaires by Tanzania standards and this is acceptable because of Azimio la Zanzibar. Na hakuna ushahidi popote duniani kwamba nchi zilizoendelea ni kutokana na viongozi wasiopenda mali. Kwa hiyo Mzee Kasori kumsakama Lowassa kwa vigezo vya Mwalimu ni sawa na kupiga mluzikwenye upepo mkali. Hiyo sakata ya Richmond Lowassa kisha wajibika na kwa dalili za wazi kabisa watanzania wameshamsafisha, bila shaka amejifunza mengi kuweza kuwa kiongozi bora zaidi. The finest steel must go through the hotest fire.
 
Nia ya Mzee Kasori hapa ni kuchafua jina la Lowasa ili asipate nafasi ya Urais - period. Kwahiyo strategically kwake huu ni wakati muafaka kuibua tuhuma hizi za Mwalimu za takriban miaka 20 iliyopita potelea mbali kama hakuziibua alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Makala hii ni marudio, ameshaitoa Raia Mwema huko nyuma ila hapa kapachika nukuu ya Bacon ili kuipamba na kuiongezea uzito. Lakini Mwl. Nyerere mwenyewe alisema yeye hakuwa malaika angeweza kukosea kama binadamu mwingine. Sasa kuhusu hizo mali za Lowasa alizozungumzia Nyerere, Mzee Kassori hazitaji, lakini hata akizitaja hatuna ushahidi kuwa Lowasa alizipata kwa njia haramu! Ni kweli Mwalimu aliwachukia sana viongozi wanaopenda mali, lakini ni ukweli pia kwamba kwa msimamo huu he was in the tiny minority. Watanzania wengi na viongozi wote wanapenda mali. Nina imani majority of current CCM and government leaders are milllionaires by Tanzania standards and this is acceptable because of Azimio la Zanzibar. Na hakuna ushahidi popote duniani kwamba nchi zilizoendelea ni kutokana na viongozi wasiopenda mali. Kwa hiyo Mzee Kasori kumsakama Lowassa kwa vigezo vya Mwalimu ni sawa na kupiga mluzikwenye upepo mkali. Hiyo sakata ya Richmond Lowassa kisha wajibika na kwa dalili za wazi kabisa watanzania wameshamsafisha, bila shaka amejifunza mengi kuweza kuwa kiongozi bora zaidi. The finest steel must go through the hotest fire.

mkuu hapa unaandika pumba sana. hivi kweli kwa akili yako unafikiri kuna mtu anachukia kuwa tajiri? Kama tulivyo watanzania leo, isipokuwa watanzania wachache tu waovu kama wewe, mwalimu hakuwa anachukia mtu kupata mali bali alikuwa anachukia mtu kupata mali kwa njia ovu na hasa njia ovu hizo zinapokuwa ni zile za kukwapua mali za umma.

Hueleweki unaposema hakuna ushahidi wa wizi wa mamvi huku ukifahamu kuwa kwa muda wote wa maisha yake ya kazi amekuwa ni mwajiriwa, "mtumishi" wa umma. Hakuna mahali popote tumewahi kuona au kusikia mamvi akifanya biashara japo hata ile ya kuuza mapera au malimao. Hivi huyu mzee, kwa mali zinazotajwa anazo, analipwa shillingi ngapi kwa mwezi na umma wa watanzania hadi aweze kujikusanyia utajiri wote huo? na ujue unapozungumzia mshahara wa mamvi maana yake unazungumzia kodi za watanzania ambao wengi wao ni maskini hohehahe, unazungumzia kodi anayokatwa bibi na babu yangu kule kijijini anapoenda dukani kununua mafuta ya taa au kibiriti au mafuta ya kupikia nusu na robo. Hizo ndo zinakusanywa kwa pamoja ndo mamvi, kama mtumishi wa umma, analipwa mshahara. Hivi ni vikodi hivyo ndo vimemtajirisha huyu fisadi? Kama si hizo ni biashara gani anafanya au amewahi kufanya huyu mzee kiasi cha kujikusanyia hizo pesa anazogawa Kila mahali Tanzania kwa nia ya kununua ikulu ya nchi hii?

Ni kweli kama ulivosema kuwa nchi zilizoendelea si kwa sababu ya viongozi wasiopenda mali, sawa kabisa. Hata hivyo wewe, kilaghai na kiuovu, unatwist maneno ili yasuit context yako. Sentensi sahihi ni kuwa nchi zilizoendelea si kwa sababu ya viongozi wasiopenda mali bali ni kwa sababu ya viongozi wasiopenda mali za wizi hasa wizi wa mali za umma.

Yaani wewe sijui hata unaandika pumba za wapi?!! kwa hiyo unataka kuhalalisha wizi wa mali za umma eti tu kwa sababu, afta all, viongozi wengi wa ccm wanaiba? akili za wapi hizo?!! au ni za ki-uvccm?

Nakushauri Acha kutumia vibaya elimu yako kutetea ujinga kwa faida ya watu wachache au faida ya muda mfupi. Mamvi ni mwizi, hafai kabisa kuwa kiongozi, ni mfano mbaya sana kwa watoto, wajukuu zetu na kizazi kijacho cha Tanzania. Achilia mbali kuwa Rais hata hiyo kutangaza tu nia hakustahili. Ukiachilia mbali wizi hata afya yenyewe ni mgogoro ulio dhahiri. Huhitaji daktari kudhibitisha, ukimwangalia tu hata jukwaani unaona kabisa. Anajitahidi kweli kujikakamaza lakini ukwel ni ukweli tu, sepeto ni sepeto na kijiko ni kijiko tu. huwezi kuficha uhalisia wa sepeto kwa kuliita kijiko kikubwa badala ya kuliita kwa jina lake halisi SEPETO

Akapumzike na wajukuu zake huyo.
 
hizu makala za kinafiki zulikua wapi kama kweli huyu mzee na wengine mnaobwabwaja humu MNA mapenzi mema na hii nchi?tufike pahala tukubali kumpata ati MTU sahihi mwenye hana dosari ndani ya ccm na nnje ya ccm sio rahisi hata kidogo so hayo mapovu yanayowatoka hapa jaribuni kuwa na kiasi lowasa upepo unamwelekea acheni apepee
 
Wewe unaweza kuhoji maoni ya Mwl Nyerere.Kweli nimeamini kupenda kweli upofu.Unataka facts zipi zaidi alizotoa Mwl Nyerere kwenye NEC !.Kwahiyo Mwl Nyerere alikuwa na chuki binafsi na Lowassa Ndossy.

Mwl. Nyerere angeweza kuhojiwa msimlishe Nyerere Maneno!
 
KIONGOZI anachaguliwa na WANANCHI....sio Mwl. Nyerere...hujui hata hilo...Nyerere hakuwa na haki ya kuchagua Rais, wala sio malaika... na alikuwa anatoa his personal views...ila sio ndio ANACHAGUA RAIS WA NCHI...!!! Wananchi wakisema NO ni No...wakisema Yes ni Yes...!!! Ww mbona toilet cleaner A-town sisi hatusemi...!? Sbb umeamua na unaipenda kazi yako...!!! na kura yako utaamua utampa nani...!!! Majority ndio watasema nani atakuwa Rais...!!!
thanks brave man
 
Jambazi sugu na fisadi papa lowasa kamwe hawezi kuwa rais wa tz. Ni mwizi ana fitina hana hoja hawezi kujieleza. Hana ubobezi wa aina yoyote.
Nguvu yake kubwa ni kinunua watz kwa nguvu ya pesa.
 
Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, “NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO” mwisho wa kunukuu. Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH).

Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira.Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira “ ANGER ”.

Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)“there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man’s life.The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul.

Men must not turn bees” Mwisho wa kunukuu.
Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa.Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA.

Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema “si mkweli hata chembe moja”.Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je?Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?



Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma’.

Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.

Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”.

Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli).

Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu?

Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli.

Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi.
Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.


Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu.

Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?

Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…


Sasa wewe Kasori ulikuwa mwandishi wa mwalimu kwa muda mrefu. Serikali ilimwekea utaratibu wa kupata huduma zote ikiwemo na kuletewa magaze,vitabu na majarida aliyopenda kusoma na wapo wa kufanya kazi hizo.Sasa wewe kuacha majukumu yako na kuingia mitaani kusakanya gazeti lenye uteuzi wa Lowassa kama waziri ni kujipendekeza kwa boss au ulitaka asononeke zaidi? Ulikuwa na chuki gani na mh. Lowassa ambayo hadi leo bado unayo kwa kuleta chapisho hili? Sasa mwanae ametangaza nia mwombee mafanikio ukaendeleze ajira yako lakini nina wasiwasi umeshaachwa na umri.
 
Na kweli nimepoteza mda wangu kusoma post ndefu, isiyo na maana yoyote. Umri mwingi huondoa hadi akili mtoa mada baki ucheze na wajukuu, ushapitwa na wakati. El ndio jibu.

ukizoea kujisaidia kwenye kichaka siku kikifyekwa utajisaidia kwenye nguo
 
Moshdar unawajibika kujibu hoja kwa mantiki na busara na siyo jazba inayotawaliwa na chuki yako dhidi ya Lowasa. Hivi aliyekwambia mwajiriwa wa umma/serikali haruhusiwi au hatarajiwi kuwa na mali ni nani hasa baada kufa azimio la zANZIBAR? Je? waajiriwa hawa hawaruhusiwi kuwa na vitega uchumi? Hawaruhusiwi kupangisha nyumba walizojenga kihalali (pengine kwa mikopo)? Are you coming from Mars? Wewe mapato, uwekezaji na vitega uchumi vya viongozi wa Tanzania unavijua? Ninachosema mimi ni kuwa hii stori ndefu ya Kasori haina maana yoyote, na inatakiwa iangaliwe katika mazingira ya azimio la zanzibar (la CCM) na ukweli kuhusu mali walizonazo viongozi wetu hasa tangu utawala wa Mwinyi. Kasori asitishwe mzigo wa kumshauri Lowassa eti asinunue Ranchi. Mbona Mkapa, Sumaye na wengine wanayo mamia ya ekari za mashamba. Au ni ile hadithi ya ndege na bundi???? Ukweli maelfu ya Watanzania wanaomuunga mkono Lowasa wanajua ukweli na hali halisi ya siasa na viongozi wa TZ. Hatuchagui Rais malaika - hayupo popote duniani. Ndiyo maana changamoto kubwa inayotukabili kama taifa ni kuwa katiba inayodhiti/punguza madaraka ya Rais na kuimarisha taasisi zinazojitegemea ili kukabiliana na rushwa. Haya mambo ya Richmond wote walihusika na ilikuwa kwa nia njema kupambana na mgao wa umeme - ufisadi was just a by-product of an already precarious national emergency.
 
Ndugu Kasori,

Nami nimemaliza kuisoma hii makala yako na sasa naweza kutoa maoni yangu. Kwanza nikupongeza kwa makala nzuri, na zaidi kwa kudiriki kujaribu kusema ukweli. Ninajua kuna wana CCM wengi wenye habari nzito kuhusu nchi na viongozi wetu lakini hawawezi kuthubutu kuzisema kwa sababu ya kukosa ujasiri na hivyo wameamua kufa na habari walizo nazo. Basi nikupongeze kwa ujasiri na uthubutu wako kwa kutoa habari na kujaribu kusema na kuetetea ukweli.

Hata hivyo kuna mambo ningependa tujadiliane kidogo na usaidie kuyaweka sawa hapa.

i) Umetuonyesha vizuri sana jinsi ambavyo ndugu Edward Lowasa ni 'hatari' kwa nchi yetu kwa kupenda kwake kujilimbikizia mali kwa njia ya ufisadi. Ninaamini habari ulizo nazo wewe ndio hizo walizokuwa na walizonazo viongozi wazito ndani ya CCM akiwemo Rais Kikwete. Sasa naomba uwe mkweli. Je, huoni kwamba kitendo cha Rais Kikwete cha kumteua Lowasa kuwa Waziri Mkuu huku akijua uhatari wake kwa Taifa letu, kwa kiwango ulichotueleza hapa, kinamfanya Rais Kikwete awe hatari zaidi kwa taifa letu kuliko hata huyo Lowasa? Je, utakubaliana nami kwamba Rais Kikwete aliipoteza nafasi muhimu ya kuushinda ufisadi kwa kumteua Lowasa kuwa waziri mkuu wa nchi yetu?

ii) Umetueleza vizuri sana kuwa Mzee wetu Nyerere (rip) alipatwa na mshangao na kubaki anacheka baada ya kusikia kuwa Rais Mkapa alikuwa amemteua ndugu Lowasa kuwa waziri. Naomba uwe mkweli tena hapa. Je, unafikiri Mzee Nyerere, kama alishtushwa kwa kuteuliwa Lowasa kuwa waziri tu, angejisikiaje kusikia Rais Kikwete amemteua Lowasa kuwa waziri mkuu?

iii) Katika makala yako umejitahidi kumtenga Lowasa na Kikwete, huku ukijua wazi kuwa Lowasa asingefika alipofika na pengine asingefanya aliyoyafanya bila kubebwa na Kikwete. Sasa nakuuliza, huoni kwamba na wewe unaingia kwenye kundi hilohilo la wakwepa ukweli? Hebu nitoe wasiwasi. Hivi karibuni familia na watu waliokuwa karibu na mwalimu Nyerere wanafanya bidii kuwa karibu na Kikwete kwa kumuonyesha kwamba yeye ni tofauti sana na wengine. Kwa kufanya hivi wamekuwa wakiwashambulia viongozi waliostaafu au ambao wameng'oka madarakani. Sasa hebu nitoe wasiwasi, je nitakuwa nimekosea nikisema kuwa kuna kajitahada mnakokafanya kakujipendekeza kwa Kikwete ili mrudi kundini? Je, na nyie mnajaribu kukwepa ukweli?

iv) Hili ni la kwetu sote watanzania. Kuna tabia ambayo tumeijenga ambayo pia imethibitika kwenye makala ya ndugu Kasori. Nayo ni kuogopa kuwasema viongozi wetu wakiwa madarakani lakini mara wanapoondoka ndipo tunapata nguvu za kuwabebea mabango. Tulifanya hivi kwa Mkapa; tulimsifia sana Mkapa akiwa madarakani na wana CCM kama Kasori waliandaa kila aina ya makongamano na maandamano ya kumpongeza kuanzia lile la kumpongeza kwa kufanikisha nchi yetu kufutiwa madeni pale Ubungo Terminal hadi lile la kumpongeza kukuza uchumi pale Mnazi Mmoja. Na tena Butiku na Mwalimu Nyerere Foundation walimsifu sana Mkapa wakati ule angali akiwapa pesa za kuendesha foundation. Lakini mara alipotoka, tulimrushia mawe mpaka huwezi kuamini kwamba ni yuleyule. Sasa tunafanya yaleyale kwa Lowasa. Wana CCM hawa hawa wanaomchamba Lowasa leo baada ya kutoka madarakani ndio hawahawa ambao walikuwa hawachoki kutukumbusha ujemadari wa Lowasa alipokuwa waziri mkuu.

Na sasa tunamkwepa Kikwete, tunasubiri tuje tumvurumshie matope akitoka madarakani.Tafsiri ya yote haya ni maneno mawili kwa kiswahili: Woga na Unafiki. Wenzetu hawafanyi hivi. Wenzetu wanashughulika na viongozi wao wakiwa madarakani, hawahangaiki na wastaafu. Ndivyo walivyofanya kwa Blair kuhusu vita ya Iraq na sasa wameachana naye baada ya kuondoka na wana-deal na Gordon Brown. Ndivyo walivyofanya na wanavyoendelea kumshughulisha George Bush kuhusu Iraq lakini wataachana naye mara baada ya Rais mwingine kuapishwa hapa January 2009.

Ukweli ni kwamba tunaelekeza nguvu zetu pasipo. Lowasa tulishindwa kumshughulisha alipokuwa kwenye madaraka. Tutamchukia na kumsuta sana sasa hivi lakini ukweli ni kwamba hili halitabadili kitu madamu yeye sasa hana alichoshikilia ambacho kinatusaidia au kutuathiri sisi kama taifa. Ushauri wangu ni kwamba tushughulike na waliopo madarakani. Na wito wangu mkubwa zaidi ni kwamba tushughulike na Rais Kikwete na serikali yake. Ninachosema ni kwamba tufike mahala watanzania tuache woga na unafiki.

Hongera Ndugu Kasori kwa makala yako.

Nakuunga mkono sana kwa mawazo yako.Huna haja ya kupoteza nguvu kupambana na nyoka asie na sumu badala yake poteza nguvu kumshughulikia mwenye sumu kwani ana uwezo wa kudhuru na kuua. STRIKE THE IRON WHEN IT IS HOT.Kuendelea kutuletea yaliyopita na mliyoshindwa kuyashughulikia mkiwa madarakani hayatusaidii kitu. Kama ulivyosema wewe mwenyewe ni kiongozi yupi mwenye huo uthubutu wa kuyahoji hadharani maovu yanayotendeka kwenye serikali iliyopo madarakani na abaki salama? Hao waliothubutu leo hii bado tunao? Wakikupenda sana watakupa cheo uwe sehemu ya serikali yao bado huo uthubutu utaendelea kuwa nao?Sasa na wewe mzee Kasori ufisadi ulioujua ni wa Lowassa tu katika awamu zote? Nao ulithibitishwa na mahakama gani? Ni kweli katika uongozi wa boss wako hakuna maovu yaliyotendewa taifa hili? Mbona huyasemi? Tuwaachie wananchi wanajua wampendae kuwaongoza kwani sio lazima atoke ccm.
 
Moshdar unawajibika kujibu hoja kwa mantiki na busara na siyo jazba inayotawaliwa na chuki yako dhidi ya Lowasa. Hivi aliyekwambia mwajiriwa wa umma/serikali haruhusiwi au hatarajiwi kuwa na mali ni nani hasa baada kufa azimio la zANZIBAR? Je? waajiriwa hawa hawaruhusiwi kuwa na vitega uchumi? Hawaruhusiwi kupangisha nyumba walizojenga kihalali (pengine kwa mikopo)? Are you coming from Mars? Wewe mapato, uwekezaji na vitega uchumi vya viongozi wa Tanzania unavijua? Ninachosema mimi ni kuwa hii stori ndefu ya Kasori haina maana yoyote, na inatakiwa iangaliwe katika mazingira ya azimio la zanzibar (la CCM) na ukweli kuhusu mali walizonazo viongozi wetu hasa tangu utawala wa Mwinyi. Kasori asitishwe mzigo wa kumshauri Lowassa eti asinunue Ranchi. Mbona Mkapa, Sumaye na wengine wanayo mamia ya ekari za mashamba. Au ni ile hadithi ya ndege na bundi???? Ukweli maelfu ya Watanzania wanaomuunga mkono Lowasa wanajua ukweli na hali halisi ya siasa na viongozi wa TZ. Hatuchagui Rais malaika - hayupo popote duniani. Ndiyo maana changamoto kubwa inayotukabili kama taifa ni kuwa katiba inayodhiti/punguza madaraka ya Rais na kuimarisha taasisi zinazojitegemea ili kukabiliana na rushwa. Haya mambo ya Richmond wote walihusika na ilikuwa kwa nia njema kupambana na mgao wa umeme - ufisadi was just a by-product of an already precarious national emergency.

acha kutwist sentest kihunihuni ili kukidhi matakwa yako ya kibinafsi. hakuna anayekataa viongozi wa umma wasiwe matajiri. tunachokataa na vingozi wa umma kuwa matajiri kwa kuiba mali za umma. Kiongozi wa umma ukiwa na mali zinatakiwa ziwe justfiable, uweze kueleza ulivozipata hatua kwa hatua. ni tofauti na kina bakheresa au mengi, wao wakiwa na mali zao, na maadam hawajakamatwa wakimwibia mtu, hakuna atakayehoji. lakini si kwa kiongozi wa umma kama mamvi ambaye, kwa kodi zetu maskini wa nchi hii, tunamhudumia, kisheria na kikanuni, kwa kila kitu mpaka kijiko cha kulia ubwabwa nyumbani kwake.

halafu hii logic yako ya kihuni ya kwamba eti lowasa hapaswi kuhukumiwa kwa mali zake za wizi kisa tu eti mbona na viongozi wote wa ccm wanaiba? huo sasa ni n uhuni. acha uhuni.

Ningekuelewa kama ungesema kuwa, afta all, viongozi wote wa ccm ni wezi na kwa hiyo, logically, ccm yote haifai..hapo walau tungefanya mjadala. ungeeleweka. sasa hii logic yako ya kwamba eti maadam wanaccm wote ni wezi basi na tumchukue aliye mwizi hodari kuliko wote huyo ndo tumpe uongoz mkuu wa nchi ni sawa na kusema "aha, bhanaee, kama mbwai basi na iwe mbwai tu...yaan kama moja limeshaharibika basi potelea mbali, acha yaharike yote kabisa tujue moja"....sasa hiyo ni kuponya au kuangamiza? unatushauri turekebishe kosa kwa kufanya kosa jingine? Achilia mbali watu kama sisi hata watu wa vijijini tu siku hizi hawawezi kukubaliana na ushauri uchwara kama huo wa kwako. watakupinga tu.

tena koma kabisa kusema eti lowasa ana watu wengi, watu wengi wapi? yeye ana watu wa kununua kwa pesa za wizi.

na tena ujue ukishakuwa kiongozi au mtendaji wa umma huishi ishi tu unavopenda wewe, kuwa ukiamua tu, mathalan, kufanya biashara unafanya, ukiamua kuimba tu unaimba....noooooo, kuna utaratibu wake. kiongozi na/au mtendaji wa umma anaongozwa kwa sera, sheria, kanuni na taratibu za uongozi na utendaji wa umma. kuna sheria za kazi na kuna miiko ya uongozi...ukizivunja unashughulikiwa kwazo na, kisheria, hakuna utetezi wa kusema eti mtu asihukumiwe kwa wizi just because na yule pale kaiba?!!!!! what is that wewe??????!!!!!

mzee mamvi akupumzike richmonduli na wajukuze.
 
Watakuja wajinga watabisha ingawa muhusika hawezi kubisha kwani hayo maandiko yapo kitambo muhusika hajawai kukanusha ila wagalatia walivyo wasahaulifu watatetea mpaka mwisho
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom