Salaam kwa Mh. Edward Lowassa na wenzake

Yaliyosemwa waziwazi kumhusu Lowasa ni mazito; lakini pia tusisahau mengi mazito yaliyosemwa kiustaarabu bila ya kutaja majina moja kwa moja.

Tofauti tu ya yaliyosemwa kwenye makala hii na yale ambayo siku zote tumekuwa tukiyazungumzia hapa JF, ni moja tu, kwamba mzee katoa mfano dhahiri ya jambo lililomhusu Lowasa. Mengine yote, hasa kuhusu CCM na udhaifu wa viongozi wetu kulinda maslahi ya wananchi wetu tumeyasema kwa njia mbalimbali.

Kwenda kufanyia kikao Butiama hakutakuwa na maana yoyote kama hakuna dhamira ya dhati ya kutaka kukisafisha chama kiondokane na viongozi walafi, wasema uongo, wachoyo, wanafiki, n.k.

Inabidi sasa Kikwete akubali kuukata muungano wake na watu hawa bila ya kusita tena. Asipoonyesha ujasiri huo, nafasi yake katika historia ya uongozi wa taifa la Tanzania itakuwa ni hafifu, na pengine atatupeleka katika machafuko kabla ya mwisho wa uongozi wake. Nafasi hii ni yake, inafaa aitumie ipasavyo.
 
Uozo wote tunaozungumzia, tatizo na sababu kuu ni JK. Yeye ndio ameweka mbolea kwenye ufisadi na anazidi kuupalilia na kuumwagilia maji. EL Monduli watamchagua tu, labda CCM wasimpitishe au yeye mwenyewe asigombee. Ndivyo tulivyo.
 
Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa
J.K.Nyerere
0754 372141

Ahsante Kasori,
This is the moment of truth!! This could probably be the thread of the month. However, katika kutoa shukurani, "Namshukuru Rais Kiwete", nigependa kukushauri kuondoa hilo kwa sababu, Raisi Kikwete alifanya kosa kubwa kumweka huyu fisadi katika nafasi ile,knowing that the guy is a crook!! Kama ulivyonukuu vifungu mbalimbali vya katiba ya CCM,then huu ni wakati wa kumshauri mhe. raisi kuwaomba radhi "kwa unyenyekevu" watanzania. I hope you won't stop there, certainly, there is a lot you can share with us here in the future
 
dah nilikuwa nachanganya na vitu vingine thank you for pointing that out...

niliiona ile, ikabidi tu niwe mdogo na kujiuliza hivi kumbe kabinti ka 1995 kumbe saa hii katakuwa kanafaa kwa matumizi ya nyumbani!!! kwikwikwikwikwi kumbe ni fuzzy math......unaweza kuwasababishia watu kesi mkuu. LOL.
 
Hii mada ni nzito. Nimesoka kisha nimeshika kichwa. Kumbuka swala zima la Lowassa na Mwalim ndani ya mwaka 1995, na mkuu alivyotupa hizo quotations ndio nimebaki speech less. I have to take a day off kuichambua hii mada.

Good staff mheshimiwa. I hope wachangangiaji kama hawa watakuja every recently ili watupe juicy staff.

It about time, Tanzania need to move forward. Not with people who against CCM only, but with every body who believes Tanzania need to be up there.
 
Ndugu Kasori,

Nami nimemaliza kuisoma hii makala yako na sasa naweza kutoa maoni yangu. Kwanza nikupongeza kwa makala nzuri, na zaidi kwa kudiriki kujaribu kusema ukweli. Ninajua kuna wana CCM wengi wenye habari nzito kuhusu nchi na viongozi wetu lakini hawawezi kuthubutu kuzisema kwa sababu ya kukosa ujasiri na hivyo wameamua kufa na habari walizo nazo. Basi nikupongeze kwa ujasiri na uthubutu wako kwa kutoa habari na kujaribu kusema na kuetetea ukweli.

Hata hivyo kuna mambo ningependa tujadiliane kidogo na usaidie kuyaweka sawa hapa.

i) Umetuonyesha vizuri sana jinsi ambavyo ndugu Edward Lowasa ni 'hatari' kwa nchi yetu kwa kupenda kwake kujilimbikizia mali kwa njia ya ufisadi. Ninaamini habari ulizo nazo wewe ndio hizo walizokuwa na walizonazo viongozi wazito ndani ya CCM akiwemo Rais Kikwete. Sasa naomba uwe mkweli. Je, huoni kwamba kitendo cha Rais Kikwete cha kumteua Lowasa kuwa Waziri Mkuu huku akijua uhatari wake kwa Taifa letu, kwa kiwango ulichotueleza hapa, kinamfanya Rais Kikwete awe hatari zaidi kwa taifa letu kuliko hata huyo Lowasa? Je, utakubaliana nami kwamba Rais Kikwete aliipoteza nafasi muhimu ya kuushinda ufisadi kwa kumteua Lowasa kuwa waziri mkuu wa nchi yetu?

ii) Umetueleza vizuri sana kuwa Mzee wetu Nyerere (rip) alipatwa na mshangao na kubaki anacheka baada ya kusikia kuwa Rais Mkapa alikuwa amemteua ndugu Lowasa kuwa waziri. Naomba uwe mkweli tena hapa. Je, unafikiri Mzee Nyerere, kama alishtushwa kwa kuteuliwa Lowasa kuwa waziri tu, angejisikiaje kusikia Rais Kikwete amemteua Lowasa kuwa waziri mkuu?

iii) Katika makala yako umejitahidi kumtenga Lowasa na Kikwete, huku ukijua wazi kuwa Lowasa asingefika alipofika na pengine asingefanya aliyoyafanya bila kubebwa na Kikwete. Sasa nakuuliza, huoni kwamba na wewe unaingia kwenye kundi hilohilo la wakwepa ukweli? Hebu nitoe wasiwasi. Hivi karibuni familia na watu waliokuwa karibu na mwalimu Nyerere wanafanya bidii kuwa karibu na Kikwete kwa kumuonyesha kwamba yeye ni tofauti sana na wengine. Kwa kufanya hivi wamekuwa wakiwashambulia viongozi waliostaafu au ambao wameng'oka madarakani. Sasa hebu nitoe wasiwasi, je nitakuwa nimekosea nikisema kuwa kuna kajitahada mnakokafanya kakujipendekeza kwa Kikwete ili mrudi kundini? Je, na nyie mnajaribu kukwepa ukweli?

iv) Hili ni la kwetu sote watanzania. Kuna tabia ambayo tumeijenga ambayo pia imethibitika kwenye makala ya ndugu Kasori. Nayo ni kuogopa kuwasema viongozi wetu wakiwa madarakani lakini mara wanapoondoka ndipo tunapata nguvu za kuwabebea mabango. Tulifanya hivi kwa Mkapa; tulimsifia sana Mkapa akiwa madarakani na wana CCM kama Kasori waliandaa kila aina ya makongamano na maandamano ya kumpongeza kuanzia lile la kumpongeza kwa kufanikisha nchi yetu kufutiwa madeni pale Ubungo Terminal hadi lile la kumpongeza kukuza uchumi pale Mnazi Mmoja. Na tena Butiku na Mwalimu Nyerere Foundation walimsifu sana Mkapa wakati ule angali akiwapa pesa za kuendesha foundation. Lakini mara alipotoka, tulimrushia mawe mpaka huwezi kuamini kwamba ni yuleyule. Sasa tunafanya yaleyale kwa Lowasa. Wana CCM hawa hawa wanaomchamba Lowasa leo baada ya kutoka madarakani ndio hawahawa ambao walikuwa hawachoki kutukumbusha ujemadari wa Lowasa alipokuwa waziri mkuu.

Na sasa tunamkwepa Kikwete, tunasubiri tuje tumvurumshie matope akitoka madarakani.Tafsiri ya yote haya ni maneno mawili kwa kiswahili: Woga na Unafiki. Wenzetu hawafanyi hivi. Wenzetu wanashughulika na viongozi wao wakiwa madarakani, hawahangaiki na wastaafu. Ndivyo walivyofanya kwa Blair kuhusu vita ya Iraq na sasa wameachana naye baada ya kuondoka na wana-deal na Gordon Brown. Ndivyo walivyofanya na wanavyoendelea kumshughulisha George Bush kuhusu Iraq lakini wataachana naye mara baada ya Rais mwingine kuapishwa hapa January 2009.

Ukweli ni kwamba tunaelekeza nguvu zetu pasipo. Lowasa tulishindwa kumshughulisha alipokuwa kwenye madaraka. Tutamchukia na kumsuta sana sasa hivi lakini ukweli ni kwamba hili halitabadili kitu madamu yeye sasa hana alichoshikilia ambacho kinatusaidia au kutuathiri sisi kama taifa. Ushauri wangu ni kwamba tushughulike na waliopo madarakani. Na wito wangu mkubwa zaidi ni kwamba tushughulike na Rais Kikwete na serikali yake. Ninachosema ni kwamba tufike mahala watanzania tuache woga na unafiki.

Hongera Ndugu Kasori kwa makala yako.
 
Mkuu Kitila,

Heshima mbele mkuu, maneno yako ni mazito mno hayabebeki, hawa kina Kisori, ndio mtakuwa na taabu sana mbele ya Mungu wa haki, kwa sababu mlikuwa na hizi habari muhimu za kuweza kulinusuru taifa na Richimonduli, lakini mkanyamaza nazo wakati zinatakiwa,

Yes, I said it kwa sababu ni maneno mengi ya kumshambulia Rostam, wakati wa uchaguzi wa rais uliopita, ndio yaliyosababisha aogope uongozi wa juu, I mean ninajua kuwa kuna manofikiri haikusaidia kitu, lakini think kwamba angepewa uwaziri wa hazina, ambao alikuwa akiuutaka sana, ingekuwaje? Sasa haya ungeya-raise wakati wa uchaguzi, au hata kuwapa upinzani ingetusaidia sana kumng'oa Lowassa, mapema kama Rostam,

Mkuu Kisori, ninaunga mkono hoja ya Mkuu Kitila, kuwa habari yako na uzuri wake wote, not only kwamba ni too late, ila ina raise a question of what are the motives behind your article? wananchi, taifa, au tumbo lako?

Bravo Kitila!
 
Now, wait a minute.

Kuna wanaojiita kuwa wao ni 'CCM damu.' Sometimes I wonder, what type of CCM do they belong to!

Na kama hao wazee hawakusema kitu wakati mwafaka ili kubadili mambo ndani ya chama, hawa 'ccm damu' wamefanya nini ndani ya chama?

Badala yake tunaona urukaji wa vihunzi tu kila kona bila ya kuwa na msimamo unaoeleweka. Ndio maana wengi hatuamini kuwa hawa 'ccm damu' wana jipya, ila ni opportunists tu kama hao wengine. Wanasubiri zamu yao ifike wakaendeleze maovu tunayoyaona leo hii.
 
FMES, Kitila na Kalamu mmenikata maini.
Honest i couldn't see in other way, you guys flip it and make headlines news concern that issue. Bravo wakubwal. That is what i called critical thinkers. What is behind the closet? That is a million dollar question? Why now and not then? Another million dollar question.

I saw Butiku when he came public and condem Mkapa, and that was smell fishy. Swala la CCM orginal kumsakama Lowassa baada ya Richmond ni unafiki. JF hapa tulisema kwamba serikali ya JK imeingizwa ICU na JK mwenyewe soon baada ya kumchagua Lowassa kama PM.

Jakaya alijua fika kabisa Lowassa ni kilafi, lakini aliamua kumchukua Boyz II Men mwenzie ili wamaintain status quo. Sasa we're in deep nightmare ndio watabiri wanatokea na kusema tulisema. Kama tungepata hizi news za Lowassa 2005 haya ya Richmond tusinge yaona kwa sasa.

I hope Mh atakuja every now and then kutupa current staff ambazo zitasaidia kuwabana wezi.

Mungu ibariki Tanzania, Mwalim RIP
 
Now, wait a minute. Kuna wanaojiita kuwa wao ni 'CCM damu.' Sometimes I wonder, what type of CCM do they belong to!

You got it right mkuu, ni mimi CCM Damu ya njano.

Na kama hao wazee hawakusema kitu wakati mwafaka ili kubadili mambo ndani ya chama, hawa 'ccm damu' wamefanya nini ndani ya chama?

Mimi CCM damu, sikuwa na hizi habari za Kisori, ningekuwa nazo kungewaka moto, kumbuka BCS nilivyokuwa nikiwasha moto kuhusu mtandao, na ni mimi niliyekuwa wakwanza kukwambia kuwa kuna kundi linaitwa mtandao no body knew about it, na unakumbuka nilivyotukanwa kuwa tunatka rais kijana.

Badala yake tunaona urukaji wa vihunzi tu kila kona bila ya kuwa na msimamo unaoeleweka.

Msimamo wangu hapa JF unaeleweka, na sina majina mia hapa forum, moja la CCM, moja la Chadema, lingine kutukania watu, lingine kwenye Obama thread huo ndio unaita msimamo na kutruka viunzi?

Ndio maana wengi hatuamini kuwa hawa 'ccm damu' wana jipya, ila ni opportunists tu kama hao wengine. Wanasubiri zamu yao ifike wakaendeleze maovu tunayoyaona leo hii.

Unawezaje kuamini positively na majina yote haya mkuu kwenye mijadala muhimu ya taifa? Kama kawaida huwezi kujadili taifa kwa mapana maana sijui kama hata una idea ya yanayosemwa hapa, nimekuambia kule kwenye thread ili uaminike hapa achana na personal na mimi, jadili taifa na tumia jina moja kama mimi ili uheshimike, maana huo ndio msimamo.

Wenye msimamo hutumia jina moja tu hapa kama mimi, na kukata ishus bila kuogopa upande upi, wala kijifunika mablanketi ya uvyama maana ndio chqanzo cha kuwa na majina mengi ili ukubalike kila kona, real man na politicians kama mimi CCM damu, hatufanyi hivyo, husimama hapa kwa jina moja na kusema bila uoga tunayofikiri,

got it?.

Ahsante Mkuu, ninakusubiri tuendele kumkoma nyani!
 
You got it right mkuu, ni mimi CCM Damu ya njano.



Mimi CCM damu, sikuwa na hizi habari za Kisori, ningekuwa nazo kungewaka moto, kumbuka BCS nilivyokuwa nikiwasha moto kuhusu mtandao, na ni mimi niliyekuwa wakwanza kukwambia kuwa kuna kundi linaitwa mtandao no body knew about it, na unakumbuka nilivyotukanwa kuwa tunatka rais kijana.



Msimamo wangu hapa JF unaeleweka, na sina majina mia hapa forum, moja la CCM, moja la Chadema, lingine kutukania watu, lingine kwenye Obama thread huo ndio unaita msimamo na kutruka viunzi?



Unawezaje kuamini positively na majina yote haya mkuu kwenye mijadala muhimu ya taifa? Kama kawaida huwezi kujadili taifa kwa mapana maana sijui kama hata una idea ya yanayosemwa hapa, nimekuambia kule kwenye thread ili uaminike hapa achana na personal na mimi, jadili taifa na tumia jina moja kama mimi ili uheshimike, maana huo ndio msimamo.

Wenye msimamo hutumia jina moja tu hapa kama mimi, na kukata ishus bila kuogopa upande upi, wala kijifunika mablanketi ya uvyama maana ndio chqanzo cha kuwa na majina mengi ili ukubalike kila kona, real man na politicians kama mimi CCM damu, hatufanyi hivyo, husimama hapa kwa jina moja na kusema bila uoga tunayofikiri,

got it?.

Ahsante Mkuu, ninakusubiri tuendele kumkoma nyani!

Standard response. I don't know where you get all that from! What, and why different names?

Fact is,dalili zote za ufisadi zipo wazi. Ni jambo la wakati tu ufike; endapo kama waTanzania tutaendelea kuwakumbatia viongozi wa aina hizi. The prognosis is quite clear.
 
Ndugu Kasori,

Nami nimemaliza kuisoma hii makala yako na sasa naweza kutoa maoni yangu. Kwanza nikupongeza kwa makala nzuri, na zaidi kwa kudiriki kujaribu kusema ukweli. Ninajua kuna wana CCM wengi wenye habari nzito kuhusu nchi na viongozi wetu lakini hawawezi kuthubutu kuzisema kwa sababu ya kukosa ujasiri na hivyo wameamua kufa na habari walizo nazo. Basi nikupongeze kwa ujasiri na uthubutu wako kwa kutoa habari na kujaribu kusema na kuetetea ukweli.

Hata hivyo kuna mambo ningependa tujadiliane kidogo na usaidie kuyaweka sawa hapa.

i) Umetuonyesha vizuri sana jinsi ambavyo ndugu Edward Lowasa ni 'hatari' kwa nchi yetu kwa kupenda kwake kujilimbikizia mali kwa njia ya ufisadi. Ninaamini habari ulizo nazo wewe ndio hizo walizokuwa na walizonazo viongozi wazito ndani ya CCM akiwemo Rais Kikwete. Sasa naomba uwe mkweli. Je, huoni kwamba kitendo cha Rais Kikwete cha kumteua Lowasa kuwa Waziri Mkuu huku akijua uhatari wake kwa Taifa letu, kwa kiwango ulichotueleza hapa, kinamfanya Rais Kikwete awe hatari zaidi kwa taifa letu kuliko hata huyo Lowasa? Je, utakubaliana nami kwamba Rais Kikwete aliipoteza nafasi muhimu ya kuushinda ufisadi kwa kumteua Lowasa kuwa waziri mkuu wa nchi yetu?

ii) Umetueleza vizuri sana kuwa Mzee wetu Nyerere (rip) alipatwa na mshangao na kubaki anacheka baada ya kusikia kuwa Rais Mkapa alikuwa amemteua ndugu Lowasa kuwa waziri. Naomba uwe mkweli tena hapa. Je, unafikiri Mzee Nyerere, kama alishtushwa kwa kuteuliwa Lowasa kuwa waziri tu, angejisikiaje kusikia Rais Kikwete amemteua Lowasa kuwa waziri mkuu?

iii) Katika makala yako umejitahidi kumtenga Lowasa na Kikwete, huku ukijua wazi kuwa Lowasa asingefika alipofika na pengine asingefanya aliyoyafanya bila kubebwa na Kikwete. Sasa nakuuliza, huoni kwamba na wewe unaingia kwenye kundi hilohilo la wakwepa ukweli? Hebu nitoe wasiwasi. Hivi karibuni familia na watu waliokuwa karibu na mwalimu Nyerere wanafanya bidii kuwa karibu na Kikwete kwa kumuonyesha kwamba yeye ni tofauti sana na wengine. Kwa kufanya hivi wamekuwa wakiwashambulia viongozi waliostaafu au ambao wameng'oka madarakani. Sasa hebu nitoe wasiwasi, je nitakuwa nimekosea nikisema kuwa kuna kajitahada mnakokafanya kakujipendekeza kwa Kikwete ili mrudi kundini? Je, na nyie mnajaribu kukwepa ukweli?

iv) Hili ni la kwetu sote watanzania. Kuna tabia ambayo tumeijenga ambayo pia imethibitika kwenye makala ya ndugu Kasori. Nayo ni kuogopa kuwasema viongozi wetu wakiwa madarakani lakini mara wanapoondoka ndipo tunapata nguvu za kuwabebea mabango. Tulifanya hivi kwa Mkapa; tulimsifia sana Mkapa akiwa madarakani na wana CCM kama Kasori waliandaa kila aina ya makongamano na maandamano ya kumpongeza kuanzia lile la kumpongeza kwa kufanikisha nchi yetu kufutiwa madeni pale Ubungo Terminal hadi lile la kumpongeza kukuza uchumi pale Mnazi Mmoja. Na tena Butiku na Mwalimu Nyerere Foundation walimsifu sana Mkapa wakati ule angali akiwapa pesa za kuendesha foundation. Lakini mara alipotoka, tulimrushia mawe mpaka huwezi kuamini kwamba ni yuleyule. Sasa tunafanya yaleyale kwa Lowasa. Wana CCM hawa hawa wanaomchamba Lowasa leo baada ya kutoka madarakani ndio hawahawa ambao walikuwa hawachoki kutukumbusha ujemadari wa Lowasa alipokuwa waziri mkuu.

Na sasa tunamkwepa Kikwete, tunasubiri tuje tumvurumshie matope akitoka madarakani.Tafsiri ya yote haya ni maneno mawili kwa kiswahili: Woga na Unafiki. Wenzetu hawafanyi hivi. Wenzetu wanashughulika na viongozi wao wakiwa madarakani, hawahangaiki na wastaafu. Ndivyo walivyofanya kwa Blair kuhusu vita ya Iraq na sasa wameachana naye baada ya kuondoka na wana-deal na Gordon Brown. Ndivyo walivyofanya na wanavyoendelea kumshughulisha George Bush kuhusu Iraq lakini wataachana naye mara baada ya Rais mwingine kuapishwa hapa January 2009.

Ukweli ni kwamba tunaelekeza nguvu zetu pasipo. Lowasa tulishindwa kumshughulisha alipokuwa kwenye madaraka. Tutamchukia na kumsuta sana sasa hivi lakini ukweli ni kwamba hili halitabadili kitu madamu yeye sasa hana alichoshikilia ambacho kinatusaidia au kutuathiri sisi kama taifa. Ushauri wangu ni kwamba tushughulike na waliopo madarakani. Na wito wangu mkubwa zaidi ni kwamba tushughulike na Rais Kikwete na serikali yake. Ninachosema ni kwamba tufike mahala watanzania tuache woga na unafiki.

Hongera Ndugu Kasori kwa makala yako.

Splendid!!!!.....Kitila........Daaaaah..................thats why I love JF!!......
 
Hata leo wengi wako aware na some dirty deals zinazoendelea serikalini. lakini wako kimya, they will come out after ten years...tuliyajua haya na blah blah kibao.... Watanzania tuna matatizo gani?

Jamani tufike point tukubaliane kwamba wote ni wana wa TANZANIA we are fighting for this precious land. Why cant we work together? Fahari gani hawa mafisadi wanaamua kuwa na millions of $$$ Geneva na Doha, wakati watanzania wenzao hata aspirin hawana?

Kwa nini tusisadiane kuwakomboa hawa ndugu zetu zaidi ya asilimia 80% walio kwenye umasikini wa kutupwa? tutaendelea kuwa source ya statistics za umasikini mpaka lini?

Nimesoma hii thread but I really feel bad in my heart! Hawa watawala wetu waambiwe kwa lugha gani kusudi waelewe kwamba we are not happy with the way they run our country?
Waungwana kweli nimechoka uvumilivu unatushinda sasa!

We shall never know the value of the peace and love we have in Tanzania till when it escapes through the window! Naomba tusifike huko.
 
Masanja:
Kwanza, itabidi tuondokane na huu utamaduni wetu mbovu wa unafiki, uzandiki,kutafuta upendeleo kwa wakubwa na kuoneana aibu. Utamaduni huu pamoja na kuwa na woga vinaturudisha nyuma sana.

Kukatishwa tamaa kama ulivyokuelezea hapo chini ni kishawishi kikubwa kwa wengi, lakini hiyo sio suluhu. Kwani kama ujuavyo, palipo na kukata tamaa matokeo yake huwa ni mabaya zaidi.

Njia iliyo bora ni kuendelea kufahamishana na kufundishana, bila shaka yoyote wakati utafika ambapo wananchi wengi tutaanza kuamini na kuamua.

Kuakata tamaa? Hapana. Mapambano yataendelea.
 
Masanja + Kalamu,

unajua kwanza huyu bwana Kasori anahitaji kupongezwa kwa atleast ujasiri wa kuyasema aliyoyasema.......na please tujaribu sana kuangalia alichoandika kuliko kuliko ku-judge hatua yake.........otherwise kwa wenzake walio wengi hii habari still ni classified......tuwasamehe hawa wazee wetu wakati mwingine huzungumza out of frustrations........ndio maana kama unaweza ku-read btn the line Mzee Kasori anamshukuru JK..................one would wonder for what!!!......jaribu ku-read btn the line

....anyhow Kitila said it loud and clear to "Typical Kasoris"......wao waanze kuwa wakweli kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele kwa kutoka na kusema kweli yale yanayoturudisha nyuma siku zote + wahusika wake ili tule nao sahani moja.........
 
Fact is,dalili zote za ufisadi zipo wazi. Ni jambo la wakati tu ufike; endapo kama waTanzania tutaendelea kuwakumbatia viongozi wa aina hizi. The prognosis is quite clear.

Facts are very clear kuwa sisi wananchi wa Tanzania tunafanana na viongozi wetu, tumejaa wivu, chuki, unafiki, na uongo. Viongozi mafisadi hatuwataki lakini ukweli tumewaweka sisi wenyewe wananchi. Dalili za ufisadi ni kupigia kelele watu usiowajua na wasiokujua kwenye internent na kuwasingizia maneno mengi ya uongo, just because wanayaona matatizo ya taifa kutoka kwenye angle tofauti na yako, that is pathetic thinking, kama sio syco,

I mean nimekuachia kwa muda mrefu sasa mkuu, lets put the bread kwenye meza hapa JF, exactly kinachokufanya wewe uwe more of a revolutionist hapa Jf au kwenye taifa letu kuliko sisi wote hapa ni nini hasa?

Mkuu msiammo wangu ninasema hivi maneno ya Kisori at this time ambapo Lowassa tayari ni ex-PM ni waste of time no matter how much amusing they are, kwa sababu as a nation sasa hivi tumempa mabenzi mawili bure alikiyokuwa akiyatumia kama waziri mkuu, tunampa nyumba mbili moja Dodoma, nyingine Dar bure, walinzi wawili personal, walinzi 24 hours kwenye nyumba zote mbili, magari mawili mapya kila mwisho wa mwaka, watumishi wawili wa ndani na nje kwenye nyumba zote mbili, safari za ,majuu mbili kila mwaka yeye na mkewe, now get this mkuu haya yote ni mpaka siku anakufa, sasa maneno ya Kisori at this time yatasadia nini? Ninasema angeyasema kabla ya Lowassa kupewa u-PM huenda ingetusaidia as a nation kujenga hoja nzito against yeye kupewa hayo madaraka, kama vile alivyojengeewa haoja znito Rostam, mpaka akakimbia uwaziri ambao alikuwa anautaka sana.

Futhermore, ninasema kuwa baadhi ya hoja za Kisori ni suspect kwa sababu haiwezekani kuwa yeye kama mtu wa karibu wa Mwalimu, alujua tu ishu ya Mwalimu against Lowassa, lakini not what Mwalimu ishu was against Muungwana, wakati sisi wananchi wote tunajua kuwa Mwalimu, aliwaengua wote wawili kwenye kinyang'anyiro cha urais, sasa kama nia ya Kisori ni njema kwa taifa, basi angesema mabaya yanayowahusu wote wawili sio mmoja tu ambaye ametolewa tayari kwenye power, na kumsafishia aliyeko kwenye power hiyo hoja au motive behind it inakuwa suspect. Ninasema in the future wale wote wenye hizi kind of info waziseme pale zinapotakiwa, lakini sio kusubiri wakati zimepitwa na wakati kama vile timing ya huyu mkuu Kisori.

Sasa mkuu hii ndiyo hoja yangu on this ishu, je yako ni ipi iweke hapa tuichambue badala ya kujaribu kuleta personal ambazo huwezi kuzithibitisha, mimi sina noma kujadili hoja wewe weka tu hapa mkuu tuvine ngoma ya wachawi, maana hoja hujibiwa kwa hoja, mimi sio bendera fuata upepo kama huamini wake hoja yako hapa tuvine!

Ahsante Mkuu.
 
SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA

Nimemsoma Askofu Mokiwa kuhusu uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa serikali. Nianze kwa nukuu ya Sir Francis Bacon; samahani kwa kuileta kwenu kwa kiingereza, One of the schools of the Grecians, examines the matter of Truth and is at a stand to think what should be in it, that men should love lies, where neither they make for pleasure, as with poets, nor for advantage, as with the merchants but it is for the lies sake.
TRUTH is a naked and open daylight that does not show the masks, and mummeries and triumphs, of the world half so stately and daintily as could lights. Truth may perhaps come to the price of a pearl, that shows best by day but it will not rise to the price of a diamond or carbuncle, that shows best in varied lights. A mixture of a lie does ever add pleasure…Truth is the sovereign good of human nature.

The first creature of God, in the works of the days was the light of the sense; the last was the light of reason and his Sabbath work ever since is the illumination of his Spirit. First he breathed light upon the fore of the matter or chaos, then he breathed light into the fore of man and still he breathes and inspires light into the face of his chosen. It is a pleasure , to stand upon the shore and to see ships tossed upon the sea, a pleasure to stand in the window of castle and to see a battle, and the adventures thereof below. "But no pleasure is comparable to standing upon the Vantage ground of TRUTH (a hill not to be commanded and where the air is always clear and serene) and to see the ERRORS, wanderings, and mists, and tempests in the valley below, so always that this prospect be with pity and not with swelling or pride. Certainly, it is heaven upon earth, to have a man's mind more in charity, rest in providence and turn upon the POLES OF TRUTH."

To pass from theological and philosophical truth, to the truth of civil business, it will be acknowledged, even by those who do not practice it, that clear and sound dealing, is the honor of man's nature; and that mixture of falsehoods, is like a alloy in coin of gold and silver, which may make the metal work the better but it embaseth it. For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes barely upon the belly and not upon the feet. There is no vile , that does so cover a man with SHAME as to be found FALSE and PERTIFIDIOUS". Mwisho wa kunukuu.

Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, " NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO" mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH). Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira. Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira " ANGER ". Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)"there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man's life. The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees" Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa. Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema "si mkweli hata chembe moja". Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo: "Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma". Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali". Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?. Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?". Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge. Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?". Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri. Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!! Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa "Natural Justice" hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli? Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) " kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena "For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet! There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious" Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia. Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao. Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.

Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.

Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty. Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje? Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?

Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him. There is also a compelling case that is in Tanzania's self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government. Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu? Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about. It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can't, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages. Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded. These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu. The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi. Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.

BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- " Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu" ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.

Namalizia kwa kusema "Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI". Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha. Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge.

Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.

Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.

Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari "Salaam kwa Mawaziri" Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.

Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji . viongozi wabovu wawajibishwe tu. Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kutu tetea leo kwa matatizo yote haya.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Africa.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa
J.K.Nyerere
0754 372141


Nyani hukomwa mchana kweupe na wala sio gizani. Maneno mazito hayo.
 
Mzee kasori, heshima mbele mkuu! Huyu Lowassa aliangushwa vibaya sana mwaka 1995, na hakuna alietarajia kuwa angerudi katika ulingo wa kisiasa! FISADI alirudi kwa kishindo na akapanda ngazi alizozipanda hadi kuwa Waziri mkuu! achilia mbali mali alizojilimbikizia mara tu baada ya CCM kuwa na uelekeo wa ki-fisadi! Maneno uliyoyatamka hapa umeyatoa wakati muafaka sana maana tayari alikwisha andaliwa madaraka mapya!! Mzee wetu kasori NAKUSHUKURU SANA KWA KUINUSURU NCHI YETU!... Ewe Fisadi LOWASSA this time HAKUNA KURUDI... TOKAAA EWE PEPO MCHAFU UNYONYAE WANYONGE WA NCHI HII!!!!!!GO GO NEVER EVER COME BACK!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom