William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
4. Mimi ninavyojuwa na tunavyoambiwa ni kwamba Mapinduzi yale yalikuwa ni ya Wazanzibari, kwamba kiongozi wa Mapinduzi alikuwa Mzee Abeid Amani Karume na wenzake kina Said Washoto. Tunaambiwa ni Wazanzibari ndio waliofanya Mapinduzi, au sio? Haya Kikwete ni Mzanzibari? Mimi ninavyojuwa na Profesa (Lipumba, ambaye ni Mnyamwezi na kimila ni mtani wa Kikwete) kwamba Kikwete ni Mkwere. Zanzibar haimuhusu shikio wala ndewe. Leo vyereje Kikwete asema: Tutayalinda Mapinduzi yetu! Vyereje!?
Na Mwandishi Wetu
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele
WAKATI Rais Jakaya Kikwete anajua kwamba Zanzibar kuna mgogoro, hata kama anaupaka rangi na kuuita mpasuko; na mgogoro umeleta maafa kisiasa, kiuchumi na kijamii, kauli zake akiwa ziarani Pemba zimepanua ufa.
Rais ameshangaza na hasa amesikitisha kila mpenda amani ya kweli kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
hawawezi kujenga hoja bila vitisho?
- Aibu ni kuyazima na kujidai hayapo, wakati yapo na ndio hasa siasa za Seif, ndio maana Kikwete amesema atalinda Muungano kwa nguvu zote, ninakumbuka siku Mwalimu alipofariki, tulikuwa kwenye mkutano na kiongozi mmoja wa Visiwani ambaye sasa ni waziri wa muungano, aliongea maneno siwezi sahau hata siku moja na ndio siku mawazo yangu yalipobadilika kuhusu Zanzibar na siasa zao, infact at onepoint yule mkuu alikuwa akitoa hotuba huku akitoka machozi kumlilia Mwalimu na kwamba wanaofikiri kufa kwake kutawapa mwanya wa kuichukua Zanzibar ni ndoto tupu, toka siku hiyo mkuu sizitizami siasa za huko kama zamani, lakini samahani kama mtizamo wangu haufikii level yako ya kuficha ficha kuwa hayapo, huku Sumaye a former PM akiandika wazi jinsi udini na urangi ulivyotawala uchaguzi wa rais mwaka 2005.
- Tafuta ile article ya "CCM tumekula nyama ya mtu", utayakuta yote ninayosema wazi hapa!
Thanxs!
there is this Kenyan fella who had the cheek to say that Tanzania one huge BEACH. That we are all a bunch of lazybones and compared to rather hard working Kenyans. I slapped him right away and reminded him about the history of the East African coast all the way from Somalia and well into Kilwa and beyond under the rulers who had MAD eyes. Look into Maalim Seif and the same characteristic is there! No wonder Mzee Mkapa had at one time said, Tunatoa salamu kwa mababu za hao wapinga Mapinduzi, vijukuu vyao, vitukuu vyao hawatawali hapa. (salamu za Mkapa katika sherehe za mwaka 2002 za Mapinduzi ya Zanzibar) By the way men with mad eyes is an expression favoured by republicans to describe current Iranian rulers and their likes. To me, the likes of Maalim Sefu are exactly bonafide residents of that hypothetical huge beachland described above. Very PAROCHIAL minded Tanzanians!
Ndio kawaida yao lakini mwanakijiji hebu chukua picha Ya seif ulinganishe na picha ya mfalme Qabus wa oman then tell me the diference and similaritieshawawezi kujenga hoja bila vitisho?
- Ameanza vizuri, lakini hap[o kwenye kubaka anasema uongo na hana sababu kwani wote tunajua kwua wananchi waliuliwa siku hiyo, lakini ya kubaka ni kuongeza chumvi for what?
- Huyo sasa anazidi kuharibu, maandamano hayakupewa kibali na serikali kwa hiyo yalikuwa ni maandamano haramu, swali ni je serikali ilikuwa right kwenye kuwawua wananchi hao? hapana ilikuwa ni excessive na un-necessary force na linaweza kujadiliwa legally kuhusu makosa ya Mkapa kuruhusu mauaji, lakini Seif hana sababu ya kubadili ukweli kwa sababu ya ku-score cheap na short term popularity ambazo in the long run haziwezi kuwasiadia wananchi wa huko Visiwani, kwa sababu yeye aksiema uongo kama anavyofanya so far kwenye hii hotuba, then anawapa nafasi ya kujibiwa uongo na watawala!
FMES!!
Punguza ushabiki please; ushahidi upo tena ukitaka utapelekwa nyumba hadi nyumba ukawaone/ukawahoji waliobakwa.
Huo ukoko wako uliolishwa na CCM usikudhuru kiasi hicho; turn back ur feelings,
hivi lile tukio la 2001 lingekukuta wewe either mama au dada yako angebakwa (achilia mbali kuuliwa) ungekuwa unaongea huo ugoro wako? Kama umefundishwa kuwa mtukanaji mzuri kwa maalim seif hatushangai, maana hata huku Unguja watu kama wewe wapo tena wengi sana. Ila hilo la kudai hakuna aliebakwa ila Maalim au CUF wanatafuta huruma ya jamii ni kuvuka UTU Thanx
-
- Hawawezi kuiba kura Unguja kwa sababu hakuna wa kumpigia kura Seif kule Unguja, huwa wanaiba kura za Pemba tu, ubaguzi upo na ni lazima uemwe wazi, hapa ndicho kinachomsumbua Seif, na hatutampa nafasi kuleta siasa zake za ki-Pemba kwenye Muungano.
Kubali au USIKUBALI ukweli ni kwamba jamaa hakuna sehemu wanakoiba kura kwa wingi kama UNGUJA ushahidi upo; kuna maeneo wao wenyewe wanachama na wapenzi wa CCM ukikaa nao wanshangaa wameshindaje wakati wanajua kuwa hawana chao!!!
CCM kwa wizi wa kura hawawezi kukataa hilo maana kama wanaweza kuibiana ktk chaguzi za ndani ya chama chao watashindwa kuiba kura ktk chaguzi zinazoshirikisha wapinzani?
NIlibahatika kushiriki Uchaguzi mmoja jimbo la Ubungo mwaka 2005 nikiwa ni mwangalizi, katika pitapita zetu mitaani tulifika eneo la Manzese, kuna kituo kimoja kama nakumbuka ni kata ya manzese/midizini. Ilivyokuwa inaonekana ktk kata hiyo kulikuwa na wafuasi wengi wengi sn wa CUF na mazingira yalikuwa yanaonyesha jamaa wanashinda tena kwa kasi ya ajabu sn.
Kuanzia mida ya saa 1 jioni tulianza kushuhudia defender 2 za askari waliovaa kiraia wazungukaaaa badae wakaondoka. Saa 4 ucku matokeo yakatangazwa CUF walishinda kata hiyo but CCM wakagoma na wakaomba hesabu zirudiwe tena, wkt marudio ya hesabu yanaanza umeme ukazimwa eneo lote; kwa bahati watu walikuwa tayari tayari zikaletwa taa za karabai, rechargable na chemli so kazi ikaendelea; nusu saa nyingi zikaja defender km 6 na kuanza kumwaga risasi hewani kama mvua; watu wakasambaratika hadi msimizi wa kituo hakuonekana. Wakaonekana askari waliovaa soksi usoni wakiingiza masanduku ya kuara ktk gari walizokuja nazo na kondoka kwa mbwembwe zote. Alfajiri tukasikia CCM ni washindi!!!
FMES, huo ni ushahidi mdogo tu tena umetokea huko unakosema CUF hawana nguvu - Tanganyika!!! Sasa kama ni huku kwenye wafuasi wa kumwaga unafikiria wanashinda kwa uhalali wa uchaguzi?
Please usitoneshe vidonda kuna watu wana-machungu na mafundo mengi nyoyoni mwao, usiwatoneshe!!!
Thanx
Kubali au USIKUBALI ukweli ni kwamba jamaa hakuna sehemu wanakoiba kura kwa wingi kama UNGUJA ushahidi upo; kuna maeneo wao wenyewe wanachama na wapenzi wa CCM ukikaa nao wanshangaa wameshindaje wakati wanajua kuwa hawana chao!!!CCM kwa wizi wa kura hawawezi kukataa hilo maana kama wanaweza kuibiana ktk chaguzi za ndani ya chama chao watashindwa kuiba kura ktk chaguzi zinazoshirikisha wapinzani?
1. CUF ilishiriki katika sherehe hizo kama chama na Mkapa aliogopeshwa sana na namna umma wa Kizanzibari wenye sare za CUF na CCM ulivyokusanyika pamoja kwa mara ya mwanzo kwenye sherehe kama hizo).
2. Ebo! Wewe badala ya kufurahi kwamba Wazanzibari kwa umoja wao wanasherehekea Mapinduzi kwa mara ya mwanzo, unakasirika.
3. Jakaya Kikwete, kwa hili kashtushwa sana na mshikamano wa Wazanzibari. Kashtushwa sana na umoja wa Wazanzibari. Wazanzibari sasa hivi wamekuja juu kusema kuwa tutalinda nchi yetu, Zanzibar ni nchi na itabaki kuwa nchi mpaka Kiama. Wazanzibari wameshikamana kulinda rasilimali zao, hasa za mafuta. Sasa Kikwete hili linamuuma sana.
4. Linamuuma sana tu, kwa sababu wao wamo katika kutekeleza mkakati tangu aliouwacha Julius Nyerere kwamba Zanzibar itoweke katika ramani ya dunia.
5. Sasa mshikamano wenu Wazanzibari unawafanya wao wasifanikiwe. Kwa hivyo, alilokuja kufanya Kikwete ni kujaribu kuwagawa tena Wazanzibari kwa kutumia wimbo wa Mapinduzi. Tena, mimi nashukuru Mungu, kasema Mapinduzi yetu, katumia wimbo wa Mapinduzi yao. Mapinduzi yao si Mapinduzi ya Wazanzibari, jamani. Mujuwe hilo!
6. Kwa hivyo, anataka kutumia wimbo huo atugawe, lakini kachelewa. Kachelewa. Hatugawiki tena ngo! Tena namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete akome, akome, akome! Akome kutuletea fitna katika nchi yetu. Akome, akome kuja kutugawa Wazanzibari. Fanya chokochoko zako huko huko Bara. Namna gani, bwana!?
1. Hotuba kama hiyo ya Seif ni udhaifu wa sera bora ambazo zitawaletea tija na faida wananchi wa ZNZ na Bara pia.
2. kwa sera na hotuba kama hizo kweli itawachukuaa muda ,maana hata mzee Mwinyi Jana pale TMK kasema bila unazi kuwa vyama vya upinzani bado vina 20% toka 1995 mapka leo na CCM wamebaki na 80% na wataendelea na hizo 20% kama hawatakuwa na sera nzuri mbele ya wanachi.
3. Muungano lazima tuulinde kwa nguvu zote kwani unafaida nyingi sana kwa taifa letu la TZ kuliko hasara wanazo ziona wanaCUF.
Naamini sii msimamo wa Wazanzibari wote ..ni wakina Seif na baadhi ya wanachama wa CUF...na mawazo kama haya basi Seif hawezi kuaminika kuiongoza Zenj!
Mbona Bara Wazanzibari wapo wengi tu wanapeta na biashara zao? Kariakoo na juzi nilikutana nao Mbarali-Mbeya wakifanya biashara ya mchele kule?
- Mkuu wangu kumbe ulikuwa hujui hilo? Kwamba anayetengenezewa njia ya utawala na Seif ni huyo kjana Sultan aliyeko London? Ukienda kwenye archives za JF utakuta tumewahi kuyajadili sana hapa infact kuna topic moja hata picha yake huyo Sultan iliwekwa hapa, Ndio maana tunaomjua vizuri Seif huwa hatumtiliii maanani sana maana tunajua nia yake, hayo maneno hawezi kuyasema akiwa Mbeya, ndio maana anakimbilia kuyasenma Visiwani siku zote, akiwa Bara anakuwa kimyaaa.
- Ni wajibu kikatiba kwa rais wa Muungano kuulinda kwa nguvu zake zote kama alivyosema Kikwete hapa hilo sio suala la mjadala, hata Seif alipokuwa Waziri wa CCM, aliapa maneno hayo hayo, again hapa Seif hana hoja ila uchochezi kwa wananchi.