johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 718
- 703
Ndugu waziri nakuletea salaam zangu kutoka nakatunga wilaya ya Ngara, ambazo kwa hakika zimebeba mtazamo wa wilaya yote.
Ndugu waziri, wanaomkumbuka Kalemani hadharani na moyoni sio kwamba wachuki na wewe, bali wanaangalia utendaji wako ukilinganisha na kalemani.
Hapa Rusumo kuna mradi wa ujenzi wa umeme kutokana na maporomoko ya maji kutoka nchi tatu, Tanzania, Burundi na Rwanda.
Kalemani alikuwa akifanya ziara za mara kwa mara, kukagua maendeleo ya mradi huu wa kuzalisha megawati 90. Ndugu waziri, tangu umechukua nafasi hiyo hujafika kukagua na hatuna taarifa utakamilika lini, ibgawa kwa kalemani tuliambiwa utakamilka April hii.
Ndugu waziri, hapa Ngara umeme ni anasa! Hauwaki siku mbili bila taarifa na ukipatikana huwezi kutumia mashine ya kunyoa nywele. Umeme mdogo.
Ndugu waziri, matokeo yake huduma za msingi hakuna nawe upo ofisini, mbaya zaidi hatuelezwi tatizo ni nini na litaisha lini, ingawa za chini chini tunaambiwa kuna nguzo imeanguka wilsyani biharamulo.
Ndugu waziri, sababu hii inayoungwa mkono na tanesco wilaya haiingii akilini. Nguzo ianguke tatizo lidumu zaidi ya miezi miwili?
Ndugu waziri juzi umeme ulikatwa saa 10 jioni , hakuna taarifa. Msemajj wa Tanesco mkoa hapokei simu, namba ya meneja ni sawa na nyara za serikali, nikamtafuta Naibu waziri kwa namba..., hapokei, nikatuma sms hakuna majibu hata sasa!
Ndugu waziri, nimesema huduma zimekosa sitanii, mashine za kusukuma maji hazifanyi kazi, pale hospitali ya rulenge ambayo ndio pekee wilaya hii yenye huduma za x-ray, huduma haziwezi kufanyika na hali ilikuwa mbaya zaidi siku nne nyuma pale mafuta yalipofichwa.
Ndugu waziri, nisikuchoshe kwa ujumbe mrefu lakini toka ofisini, njoo huku kwetu kama alivyofanya mtangulizi wako, kuiga kitu kizuri sio ujinga.
Wasalaam.