Sala ya 'HILI NI FUMBO LA IMANI 'ya Kanisa Katoliki ina fumbo gani kwa Siasa za Ulimwengu huu?

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Ipo Sala maarufu sana isaliwayo na wana Katoriki baada tu ya matoleo inayofahamika kama, 'HILI NI FUMBO LA IMANI'.Sala hiyo inafikirisha sana!

Mfano, Siasa hasa za ULIMWENGU huu zimejaa mafumbo na kutokufahamika hasa ni nini hatimaye kesho Wafanya Siasa wataamua huku tukizingatia Siasa hubadili mwelekeo wa Taifa lolote lile kimfumo,maendeleo na bila kusahau mazoea ya kile kilichozoeleka katika jamii yeyote ile.NI FUMBO LA IMANI!

Kwa mfano,CCM takribani miaka saba iliyopita kiliamua kuja na dhana ya 'KUJIVUA GAMBA' dhana ambayo ilipelekea tuliowazoea na walizoeleka kutokutajwa,kuzungumzwa na hata kutuhumiwa-walituhumiwa.Kitendo kile kwa hakika kilibadirisha mazoea ya Siasa tulizozizoea za wale wasiozoelewa,walizoelewa.LILIKUWA NI FUMBO LA IMANI!

Hatimaye,dhana ile ya KUJIVUA GAMBA ilipelekea kushuhudia mabadiriko makubwa kwa kiasi ndani ya Siasa za CCM.Baadhi ya Magwiji ndani ya Chama kile walijihudhuru nyadhifa zao .Kwa mfano mtu maarufu sana ndani ya Chama hicho Ndugu Rostam Aziz aliachia ngazi zote alizopata kuwa nazo kama Ujumbe wa Halmashauli Kuu ya Chama na Ubunge pia alipokuwa akiwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Igunga.LILIKUWA FUMBO LA IMANI!

Kwa muktadha huo huo wa FUMBO LA IMANI CCM bila kutarajiwa katika Vikao vya kumteua Mwanachama ambaye alitakiwa kugombea nafasi ya Urais kilikata jina la Mwanachama maarufu kuliko wote waliokuwa katika mbio hizo EDWARD LOWASSA.Haikutarajiwa!Ajabu ya kweli alipitishwa mtu ambaye japo tu kwenye tano bora hakutarijiwa-FUMBO LA IMANI!

John JOSEPH POMBE MAGUFULI alishinda kinyang'anyiro kile japokuwa alikuwa akitamkwa tamkwa lakini hakupewa nafasi ya kuwashinda Magwiji kama kina Lowassa na Membe.Magufuli alipata ushindi ndani ya Chama chake na alishinda u-Rais na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.LILIKUWA NI FUMBO LA IMANI!

Leo,yapata miaka minne ya u Rais wa Magufuli mambo mengi ya ki FUMBO LA IMANI yametokea na yanaendelea kutokea. Kwa hakika hata nikiamua kuyaainisha hapa itanichukiwa mda mwingi usiotosheleza.

Pamoja na yote hayo kutukia bado hakuwa-hakuwepo baina yetu sote tuliohisi ama kuota kuwa hayo ya leo yangekuwa.Ndiyo maana nauliza hiyo Sala ya FUMBO LA IMANI ina nafasi gani katika ULIMWENGU WA SIASA!?

Magufuli
 
Alikataa uwepo wa corona..FUMBO LA IMANI
Walifariki wanazuoni wakubwa,watumishi waandamizi wa serikali nao walipoteza kwa changamoto za pumzi....bado akakataa kuwa hakuna corona.... FUMBO LA IMANI.
Hatimaye alifariki Rais wa JMT...FUMBO LA IMANI
 
Back
Top Bottom