Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,826
- 730,269
Kwa waamini na waaminio,
Maisha yetu ni sawa na utando wa buibui cobweb! Yakiwa yana nguvu asili ya Kimungu (kwa waamimio)kutoka katikati, siku zote timeshikliliwa na nguvu hiyo na ndio inayotusaidia kuweza kusonga mbele.
Kuna hili la sala na dua kufuatana na imani zetu, hili jambo lina nguvu kubwa mno ya kutuokoa toka kwenye majanga mengi. Hapa sizungumzii utaratibu wa kawaida wa ibada zetu bali maombi na dua za kimya za mtu binafsi popote alipo na lolote alifanyalo ukipanda gari ukiingia mahali popote ukila chochote ukiongea chochote, piga dua yako ya kimya kisha fanya utakalo(lisiwe baya tu lakini).
Sala yako na dua yako kwako binafsi na kwa wengine ni tiba kwako na kwa wengine ni msaada mkubwa kwa ulimwengu wa roho.
Tunakutana na kesi nyingi za ajabu matukio ya kushangaza mno, inatokea ajali mbaya unasalimika au hata kama umepata majeraha unasaidika kwa haraka na vitu vyako vya thamani havipotei hata kimoja.....matukio ni mengi mifano ni mingi.
Inatosha tu kusema dua na sala yako ya kimya ni tiba na uhai wa dunia. Kwa kila neno moja utakaloomba kwa sala ama kwa dunia unaleta matokeo chanya katika ulimwengu wa roho.
Basi hapo ulipo sasa na unapofungua uzi huu fanya sala/dua ya kimya ukiomba amani ya ulimwengu na ustawi wa dunia...bila kuisahau familia yako, ndugu zako jamaa na rafiki, taifa lako na wale wote wanaopitia nyakati ngumu sasa.
Kwakuwa wakati uki JF ukiperuzi na kugombana na watu kuna watu wako hospital katika hali mbaya magonjwa ya ajabu yasiyotibika, wengine mahabusu wengine gerezani kwa kesi za chuki visasi na kusingiziwa, wengine wako kwenye mtanziko mkubwa wa madeni na mambo magumu mno.
Omba sasa fanya dua sasa ikimbuke na JF.