Kusaini mkataba ni suala lingine na utekelezaji ni mwingine.Natty alitakiwa atumie busara kuvunja mkataba sio kwa kua kasaini mwingine basi akae kimya.Nati amekutwa tu na ngozi ya chui wakati alieua chui ni mwingine.Isitoshe serikali inajua kuliko kubenea.
kweli chadema wamekua watetezi wa mafisadi
Hapo utakuwa umetumia kitovu kufikili,kama unadhani uvunjaji wa mikataba ni rahisi kama mnavyovunja makazi ya watu kwa kutumia buldoza,mwambie makomeo aliyerithi mikataba ya kifisadi katika sekta za mafuta,gesi na madini aivunje.
Kuwa mwanafamilia wa chama cha majipu kusikutoe ufahamu.Mikataba yote yenye kulinyonya Taifa letu imehifadhiwa Ikulu ya magogoni,kwa nini huyo "ngariba" wa majipu asianze na majipu yaliyo sebleni kwake badala ya kuokoteza vijipu uchunguzi vilivyo mbali?
Tumekua Taifa la mizaha ili kujipatia umaarufu ilihali Wadanganyika tukiendelea kuusaka mlo wa siku kwa tochi.Haiwezekani nchi yenye kila rasilimali leo hii miaka 54 ya kujitawala bado kuna majuha wa aina yako wanaowakatia viuno watawala na kuwafunga gidamu za viatu vyao ili wahongwe pepo.
Hadi pale tutakapouchukia umaskini kwa dhati ya mioyo yetu,ndipo tutakapoanza kuwa na hasira juu ya wale wote walioigeuza nchi yetu kuwa shamba la bibi.
Hii haikuwa nchi ya kuendeshwa kwa kutegemea kodi.Mungu alitupa kila kitu,lakini kwa vile tumekuwa vipofu wa akili,hatuwezi kung'amua ushenzi na uhayawani unaofanywa na tuliowapa dhamana.
Hapa KAHAMA kila Alhamisi Ndege ya Buzwagi inatua na kuondoka na shehena ya matofari ya dhahabu toka migodi ya Buzwagi( Acacia) na Bulyanhulu.Serikali Sikivu ya Chama Cha Majipu chini ya "Ngariba" bingwa wa kutumbua majipu ipo tu imestarehe Ikulu ya magogoni inakimbizana na wafanyabiashara na kuwafungia mageti watumishi wa Umma.Kama wao ni watu wa kazi kama wanavyojisifu kwa nini wasiione mianya hii ya uporaji wa utajiri wetu badala yake tunaridhika na mlabaha wa 3%?
Kubana matumizi bila kuwa na nidhamu katika mikataba ya maliasili zetu ni sawa na mtu anayejaribu kuokoa muda kwa kusimamisha saa.Ukizima saa asubuhi usidhani itaendelea kuwa asubuhi,dunia itaendelea kulizunguka jua na kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake,tahamaki usiku utaingia.Hatuwezi kuendelea kuwa Taifa la wapumbavu tunaoruhusu utajili wetu ubebwe na wageni huku sisi tukiendelea kubanana na wawekezaji wa ndani ambao wanatafuta kwa jasho lao na kuwaacha wageni ambao wanachuma utajili wetu.
Hadi sasa hakuna tulichoweza kukisimamia kama Taifa huru,ni mara ya Pili sasa Wazungu wanaingilia na kuinusuru nchi katika ulafi na uporaji wa wachache.Ni Wazungu waliorudisha chenji ya Rada baada ya wajanja wachache walioliingiza chaka Taifa kwa kupiga cha juu na kuficha vijisenti ughaibuni.Ni Wazungu haohao sasa hivi wapo vitani wakipambana kuturudishia chenji yetu ambayo mkwere aliiita "pesa ya mdafu" baada ya wajanja wachache kujiongezea cha juu katika malipo ya mkopo wa Taifa kupitia Stanbic bank.Leo hii kuna watu wanaipongeza Serikali sikivu ya ngariba wa majipu ilihali ni Wazungu waliolibumbulusha dili hilo.Acha tuendelee kusomeshana namba ili walau tuwe na uwezo wa kujua KKK.