Sakata la watanzania kufukuzwa Kenya; Spika asema Charles Njagua hana hadhi ya kujibiwa na Serikali. Balozi wa Kenya asema sio kauli ya Serikali

I think that guy was drunk or under influence...pressurised and in panic.
 
Kelele zote Watanzania wameteka soko la mitumba Nairobi(Gikomba). Biashara ya mitumba imeshamiri Kenya hivi karibuni baada ya wananchi wengi Kenya ku kubali mitumba kutokana na bei rafiki,fashion na quality.
 
Hiko ni moja ya kielelezo cha ugumu wa maisha na roho ya korosho
Hakuna watu wana roho mbaya duniani kama wakenya
 
Matunda ya kuwapa ubunge darasa la 7/mtu aliyekua kondakta kama Jaguar tumeanza kuyaona.
 
Huyu Jaguar anyimwe visa ya kuingia Tanzania katika kipindi hiki cha mpito na TZ wasipige nyimbo zake mpaka aombe radhi.
Akikanyaga Tanzania polisi Wala serikali msihangaike naye wanamchi mtaani tutajua Cha kumfanya Mimi nimeshanunua Nondo,panga, shoka,petroli lita 20 na kibiriti namsubiria siku akiweka mguu wake Tanzania
 
Serikali kumjibu mvuta bange mvaa mlegeze ni kujishusha hadhi yule ujibiwa Na Musiba au lemutuz tu.Si kauli ya serikali ya Kenya duniani nzima INA wageni ufanya shughuli zao ukienda China,India,ufaransa,uk ,Dubai Wakenya,watz wapo wanachuma wanaleta nyumbani.Huyo mropokaji alitaka kugain umaarufu tu,anapewa makavu live kwenye Insta page yake
 
Ukijaribu kuwaza kwa mbali binafsi naona ni hatar sana.heb imagine Jaguar akaja bongo recently halaf muhun mmoja toka kenya au nchi yoyote akamlamba shaba!huo moto utakao waka utaunganishwa moja kwa moja na kauli yake.na hapo itakayotazamwa ni bongo na mgogoro wa kidiplomasia utaanzia hapo
 
Uko timamu?

Nadhani huyu mkuu hafahamu athari za ma ‘rable rousers’ kama huyo Jaguar na jinsi zinavyohatarisha maisha ya watu waishio ugenini. Hata wakenya walioko Tanzania hwawezi kuwa na amani bila kauli za huyo lofa kufanyiwa kazi na serikali zote husika.
 
Katika Kila Jambo linaonekana kutoa hofu na kuhatarisha usalama wa wananchi wetu tunapaswa kulijibu vikali Pasipo kuchelewa ..
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri mkuu kutoa tamko kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha mbunge wa Kenya akiwataka Watanza walioko Kenye kuondoka ndani ya Saa 24.

Jana mbunge wa Kenya Charles Njagua alimaarufu Jagwa alieimba kibao cha maarufu wa Kigeugeu alionekana akiihamasisha serikali kuwatimua wageni wote walioko Kenya wakiwemo watanznia

Na kwamba serikali isipofanya hivyo yeye atahamasisha wananchi kwenda kubomoa maduka yao na kuwafukuza kwa lazima.

----------

Spika:
Asubuhi Mchengelwa aliomba mwongozo kuhusiana na matamshi yale ya Mbunge wa Kenya, yale matamshi ya ajabu sana na hovyo sana. Nimekuwa nikifikiria jambo hili, napata tabu sana kuitaka Serikali iseme chochote, sijui ushauri wenu ila ni kwa sababu matamshi yale yametamkwa na Mbunge huko mtaani sasa Serikali kumjibu naona tunampa hadhi. Sijui ushauri wenu. Nilikuwa nadhani alitakiwa apate wabunge wasema hovyo tu wamjibu hana hadhi ya kujibiwa na Serikali, Mbunge mmoja tu alitakiwa amijibu

Mbowe
Hili jambo ni kubwa na zito, si la kupuuza. Alichozungumza mbunge wa Kenya mimi niliona tangu jana usiku, nilitumia sms baadhi ya marafiki zangu Kenya ambao ni viongozi kuuliza juu ya suala hilo, wengi walikana. Ila sisi kama Watanzania tuliotajwa kwenye ile kauli tunahitaji majibu, sidhani kama kuna sababu ya kupuuza. Ningeshauri Bunge hili litoe kauli ya kukemea na kulaani kauli ile na kauli hiyo itambue kuwa hatuna ugomvi na watu wa Kenya na Serikali yake ila tuitake Serikali ya kenya kutoa kauli kudhibiti kauli kama hizi kutoka kwa viongozi wetu zinazoweza kuchafua mahusiano yetu

Tizeba
Katika mazingira ya kawaida yule mbunge unaweza ukamdharau na tukaachana naye lakini kwa sababu mambo haya yamekwisha tokea hapa Afrika kwa uchochezi mdogo kama huo. Hatuichukulii Serikali ya Kenya kuwa ndio yenye mawazo hayo, lakini Serikali ya Kenya inalo jukumu la kukana hiyo kauli na kusema yale ni mawazo yake binafsi ili sisi tuwe na uhakika kuwa watanzania watakuwa salama huko kenya

Lusinde
Mimi naomba Bunge lifikirie upya namna ya kujadili huu mjadala juu ya mbunge mmoja wa kenya aliyekuwa kalewa mtaani. Yule ni mbunge mmoja ila tunatua muda kumjadili kama nchi wakati majibu yanaweza kutolewa na mbunge mmoja, mimi nina mkutano Jumatatu na mimi nitatoa amri Wakenya wanaofanya kazi hapa tutapiga warudi wako. Japo litakuwa limeisha hilo. Tusitumie kauli ya Bunge kujadili vitu vya namna hii, huu ni uoga Taifa linateketezwa na Wabunge waoga.

Waziri Mkuu
Nawasihi muwe watulivu Watanzania wote juu ya jambo hili, ni kweli Serikali imsikia tangu jana na haukukaa kimya na tumelifanyia kazi. Kwanza tumetambua mzungumzaji ana mamlaka gani ndani ya nchi yao, ni kiongozi wa eneo moja. Na kenya wameingia kwenye uchaguzi hivyo inawezekana kwa namna moja kwa matakwa yake akasema hayo, si jambo zuri. Ila tuna tambua Kenya ni nchi rafiki na jirani sana na viongozi wakuu wanaongea lugha moja. Wananchi Tanzania na Kenya wanaishi kama ndugu, tumezungumza na balozi wa Kenya nchini Tanzania na Balozi wa Tanzania Kenya. Balozi wa Kenya nchini Tanzania amesema ule si msimamo wa Kenya wala kauli ya Serikali wala si msimamo wa Wananchi Kenya bali ni ya mtu mmoja na watachukua hatua mbalimbali

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashaiki walio Bungeni Arusha wamelaani kauli hiyo kwa kauli moja kwani inaharibu uhusiano kati ya nchi na nchi.
Hawataamini,ngoja walipuuze hilo ,watakutana na kitu kikubwa.
 
Back
Top Bottom