Sakata la watanzania kufukuzwa Kenya; Spika asema Charles Njagua hana hadhi ya kujibiwa na Serikali. Balozi wa Kenya asema sio kauli ya Serikali

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,042
Points
2,000

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,042 2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri mkuu kutoa tamko kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha mbunge wa Kenya akiwataka Watanza walioko Kenye kuondoka ndani ya Saa 24.

Jana mbunge wa Kenya Charles Njagua alimaarufu Jagwa alieimba kibao cha maarufu wa Kigeugeu alionekana akiihamasisha serikali kuwatimua wageni wote walioko Kenya wakiwemo watanznia

Na kwamba serikali isipofanya hivyo yeye atahamasisha wananchi kwenda kubomoa maduka yao na kuwafukuza kwa lazima.

----------

Spika:
Asubuhi Mchengelwa aliomba mwongozo kuhusiana na matamshi yale ya Mbunge wa Kenya, yale matamshi ya ajabu sana na hovyo sana. Nimekuwa nikifikiria jambo hili, napata tabu sana kuitaka Serikali iseme chochote, sijui ushauri wenu ila ni kwa sababu matamshi yale yametamkwa na Mbunge huko mtaani sasa Serikali kumjibu naona tunampa hadhi. Sijui ushauri wenu. Nilikuwa nadhani alitakiwa apate wabunge wasema hovyo tu wamjibu hana hadhi ya kujibiwa na Serikali, Mbunge mmoja tu alitakiwa amijibu

Mbowe
Hili jambo ni kubwa na zito, si la kupuuza. Alichozungumza mbunge wa Kenya mimi niliona tangu jana usiku, nilitumia sms baadhi ya marafiki zangu Kenya ambao ni viongozi kuuliza juu ya suala hilo, wengi walikana. Ila sisi kama Watanzania tuliotajwa kwenye ile kauli tunahitaji majibu, sidhani kama kuna sababu ya kupuuza. Ningeshauri Bunge hili litoe kauli ya kukemea na kulaani kauli ile na kauli hiyo itambue kuwa hatuna ugomvi na watu wa Kenya na Serikali yake ila tuitake Serikali ya kenya kutoa kauli kudhibiti kauli kama hizi kutoka kwa viongozi wetu zinazoweza kuchafua mahusiano yetu

Tizeba
Katika mazingira ya kawaida yule mbunge unaweza ukamdharau na tukaachana naye lakini kwa sababu mambo haya yamekwisha tokea hapa Afrika kwa uchochezi mdogo kama huo. Hatuichukulii Serikali ya Kenya kuwa ndio yenye mawazo hayo, lakini Serikali ya Kenya inalo jukumu la kukana hiyo kauli na kusema yale ni mawazo yake binafsi ili sisi tuwe na uhakika kuwa watanzania watakuwa salama huko kenya

Lusinde
Mimi naomba Bunge lifikirie upya namna ya kujadili huu mjadala juu ya mbunge mmoja wa kenya aliyekuwa kalewa mtaani. Yule ni mbunge mmoja ila tunatua muda kumjadili kama nchi wakati majibu yanaweza kutolewa na mbunge mmoja, mimi nina mkutano Jumatatu na mimi nitatoa amri Wakenya wanaofanya kazi hapa tutapiga warudi wako. Japo litakuwa limeisha hilo. Tusitumie kauli ya Bunge kujadili vitu vya namna hii, huu ni uoga Taifa linateketezwa na Wabunge waoga.

Waziri Mkuu
Nawasihi muwe watulivu Watanzania wote juu ya jambo hili, ni kweli Serikali imsikia tangu jana na haukukaa kimya na tumelifanyia kazi. Kwanza tumetambua mzungumzaji ana mamlaka gani ndani ya nchi yao, ni kiongozi wa eneo moja. Na kenya wameingia kwenye uchaguzi hivyo inawezekana kwa namna moja kwa matakwa yake akasema hayo, si jambo zuri. Ila tuna tambua Kenya ni nchi rafiki na jirani sana na viongozi wakuu wanaongea lugha moja. Wananchi Tanzania na Kenya wanaishi kama ndugu, tumezungumza na balozi wa Kenya nchini Tanzania na Balozi wa Tanzania Kenya. Balozi wa Kenya nchini Tanzania amesema ule si msimamo wa Kenya wala kauli ya Serikali wala si msimamo wa Wananchi Kenya bali ni ya mtu mmoja na watachukua hatua mbalimbali

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashaiki walio Bungeni Arusha wamelaani kauli hiyo kwa kauli moja kwani inaharibu uhusiano kati ya nchi na nchi.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
34,509
Points
2,000

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
34,509 2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri mkuu kutoa tamko kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha mbunge wa Kenya akiwataka Watanza walioko Kenye kuondoka ndani ya Saa 24.

Jana mbunge wa Kenya Charles Njagua alimaarufu Jagwa alieimba kibao cha maarufu wa Kigeugeu alionekana akiihamasisha serikali kuwatimua wageni wote walioko Kenya wakiwemo watanznia

Na kwamba serikali isipofanya hivyo yeye atahamasisha wananchi kwenda kubomoa maduka yao na kuwafukuza kwa lazima.
Huyu Jaguar anyimwe visa ya kuingia Tanzania katika kipindi hiki cha mpito na TZ wasipige nyimbo zake mpaka aombe radhi.
 
idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,042
Points
2,000

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,042 2,000
Sidhani kama huo ni msimamo wa wakenya
Ndio maana Bunge limemtaka Waziri Mkuu kutoa Tamko....hii kauli ni nzito sana kutolewa na mbunge.

Usishangae serikali ya Tanzania kumwita balozi wa Kenya kujieleza kuhusu kauli hiyo .

Hivi unadhani watanzania walioko huko wako kwenye hali gani.
 
Los técnicos

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Messages
2,180
Points
2,000

Los técnicos

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2014
2,180 2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri mkuu kutoa tamko kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha mbunge wa Kenya akiwataka Watanza walioko Kenye kuondoka ndani ya Saa 24.

Jana mbunge wa Kenya Charles Njagua alimaarufu Jagwa alieimba kibao cha maarufu wa Kigeugeu alionekana akiihamasisha serikali kuwatimua wageni wote walioko Kenya wakiwemo watanznia

Na kwamba serikali isipofanya hivyo yeye atahamasisha wananchi kwenda kubomoa maduka yao na kuwafukuza kwa lazima.
Mbona hili ni tamko la mbunge tu.
Tamko linalofanyiwa kazi ni la gov tu
 
King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
34,509
Points
2,000

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
34,509 2,000
Siasa zimemlevya amesahau yote kuhusu Tanzania.
Ametu letdown sana wana Afrika Mashariki,apewe adhabu yeye kama yeye mpaka aombe radhi,wa BAN nyimbo zake huku TZ na Visa ni adhabu TOSHA ambayo itaondoa Maziwa mgando kwenye ubongo wake.
 
mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Messages
1,721
Points
2,000

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2011
1,721 2,000
Serikali ya Tz haijihusishi na raia waliopo nje ya nchi ambao hawatambuliki ubalozini.
Yaliyotamkwa na Mb. Jagwa ni maoni take binafsi na si ya serikali ya Kenya. No need to panick, wala serikali yetu isijihangaishe NATO.
Na sisi tuwafukuze na tufunge balozi yao
 
avogadro

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
3,750
Points
2,000

avogadro

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2013
3,750 2,000
In international law, diplomatic protection (or diplomatic espousal) is a means for a state to take diplomatic and other action against another state on behalf of its national whose rights and interests have been injured by that state. Diplomatic protection, is a discretionary right of a state and may take any form that is not prohibited by international law. It can include consular action, negotiations with the other state, political and economic pressure, judicial or arbitral proceedings or other forms of peaceful dispute settlement.
 
adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
10,911
Points
2,000

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
10,911 2,000
Huyo wala sio wakutilia maanani, wakupuzwa tu, tunao hapa kwetu akina Kingu, Msukuma, manyanya, na waliosema wanao ushahidi mbiguni na duniani.

Tunao wengi wakutosha ndani ya bunge letu la JMT kupiga makofi nakuitikia ndiyooooo

Katiba hapana ndiyooo

Bunge live hapana ndiyooo

Mikutano ya siasa hapana ndiyooo

Watoto wakike wanaopata ukakatili hapana Kuendelea na masomo kitombooo

Kuihoji serikali hapana ndiyooo

Sasa kati ya hawa wa ndiyooo na huyo mkenya nani mwenye madhara makubwa kwetu? Si hawa wa NDIYOOO

THIS IS CRAZY.......
 
Timiza

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
5,149
Points
2,000

Timiza

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2017
5,149 2,000
Na sisi tuwafukuze na tufunge balozi yao
Si msimamo wa Wakenya ni msimamo wa mwanasiasa mmoja aliyekimbia shule wakati wenzake wakisoma geography, uchumi Na siasa yeye alikuwa chooni akivuta bangi.Ajui kuwa uchumi wa nchi ujengwa Na wageni
 
Timiza

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
5,149
Points
2,000

Timiza

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2017
5,149 2,000
Kazi ya mwanasiasa ni kutafuta popularity hata kama jamii itaangamia.Jagwa hana tofauti Na Nkamia,lusinde,msukuma Kwa matamko ya hovyo kwenye jamii.Musiba ndo size yake tosha kujibizana nae.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
68,212
Points
2,000

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
68,212 2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri mkuu kutoa tamko kuhusu video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha mbunge wa Kenya akiwataka Watanza walioko Kenye kuondoka ndani ya Saa 24.

Jana mbunge wa Kenya Charles Njagua alimaarufu Jagwa alieimba kibao cha maarufu wa Kigeugeu alionekana akiihamasisha serikali kuwatimua wageni wote walioko Kenya wakiwemo watanznia

Na kwamba serikali isipofanya hivyo yeye atahamasisha wananchi kwenda kubomoa maduka yao na kuwafukuza kwa lazima.
Mungu ibariki Kenya
 
Alexism

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Messages
3,434
Points
2,000

Alexism

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2011
3,434 2,000
Nadhani huyu Jaguar ameiga aya mambo kwetu watanzania asa akina Musiba ,James Hery, Polisi nk kwa wanayoyafanya kwa wapinzani asa CHADEMA kwa maslahi ya CCM . Yupo sawa tu
 
Forum statistics

Threads 1,390,025
Members 528,081
Posts 34,041,243
Top