Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU , Mkoa wa Kilimanjaro imewakamata watendaji wa vijiji 72 wa wilaya ya Hai kwa kosa la kujaribu kuandaa taarifa yenye tarehe za miaka iliyopita ili kuonyesha marehemu waliogunduliwa na kamati ya ulinzi na usalama ktk mpango wa TASAF walikuwa na wategemezi kwa mujibu nyaraka hizo feki zilizokuwa zinaandaliwa kwa Maelekezo ya mkurugenzi mkuu wa TASAF na Naibu katibu mkuu Tamisemi ambaye naye ni mjumbe wa bodi ya TASAF
Watendaji hao wamekamatwa Leo wakiwa wanagushi nyaraka hizo katika ukumbi wa Halmashauri ya Hai chini ya usimamizi wa Watumishi wa TASAF kutoka Makao makuu Taifa waliopo wilayani Hai kwa kazi maalumu.
Watendaji hao inasemekanana walipewa maelekezo kufika halmashauri wakiwa wamebeba mihuri yao ili wasaini documents walizopewa na kuweka muhuri kwenye nyaraka hizo zinazoonyesha ziliandaliwa na kuwekwa sahihi tarehe 01-05-2015, ili kwa nia ya kudanganya kwamba wanufaika hao walikuwepo na kukidhi matakwa yote toka mwaka 2015 Lengo likiwa ni kutekeleza maelekezo ya TASAF Makao makuu kuficha ukweli kuhusu wanufaika waliokuwa wakilipwa pesa miongoni mwao wakiweko marehemu takribani 190.
Wakati wapo ukumbini wakiendelea na zoezi hilo la kusaini nyaraka hizo ndipo Maafisa wa TAKUKURU na Maafisa wa Polisi wakawavamia na kuwatia Mbaroni .
Kamanda Wa Takukuru wa mkoa wa Kilimanjaro amesema upelelezi bado unaendelea.