DOKEZO TASAF kwa sasa haimnufaishi mlengwa. Serikali chunguzeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Natambua kuwa nia ya serikali kuanzisha mfuko huu ilikuwa ni kuwapunguzia makali ya umasikini baadhi ya wananchi wasio na vipato kabisa. Kundi hili ni la wazee, yatima, walemavu, nk.

Utafiti wangu mdogo umenionesha kuwa TASAF imekuwa ikinufaisha zaid wasimamizi/watendaji wa mfuko kuliko kundi hilo lililokusudiwa. Kwanza namna wanatoa au kugawa hizi pesa ni ya kizamani na inayoweza kuleta ushawishi wa kifedha kwa watendaji hao; maana pesa zinagawiwa taslimu. Lakini pili kundi hili la wanaohudumiwa ni watu duni, wenye uelewa mdogo; na hivyo huweza kubabaishwa na kuminywa haki zao.

Naiomba serikali iangalie upya mfumo huu wa kutoa fedha kwa wanufaika wanaostahili.

Hapa ninao mfano mmoja ambao umetokea hivi karibuni katika Manispaa ya Musoma. Wanufaika wameitwa katika kata zao kwenda kupokea fedha hizo. Katika kata moja niliyoitafiti, waliarifiwa kuwa fedha hizo ni za miezi ya Novemba na Desemba mwaka 2023. Baada ya kusainishwa kila mmoja alipewa fedha zake; na ni dhahiri viwango vinapishana maana kuna wengine hushiriki kazi za usafi wa mazingira hivyo kipato chao huwa juu ya wale wasioweza kushiriki.

Baada ya zoezi kukamilika ilihali kila mmoja amepewa fedha zake; ilitokea baada ya saa 2 baadhi ya wahusika waliitwa tena ofisini na kuambiwa warejeshe fedha hizo kwa kuwa hawakustahili kupata chochote! Ilikuwa mshikemshike maana ni wazi ndani ya hizo saa 2 pesa inakuwa imekwishaingia kwenye matumizi.

Swali langu kwa watendaji hao, walishindwaje kubaini tatizo hilo kabla ya kuwaita kusaini fedha hizo; maana kama mnufaika hastahili kupata kitu kwa mwezi huo, kwa nini kumuita ofisini na kumpa fedha, kisha kumdai arejeshe? Na inakuwaje hao watendaji wanashindwa kupiga hesabu ndogo za kujumlisha na kutoa, ili kuwianisha (to balance) mahesabu yao. Hakika wameleta usumbufu na kuwafedhesha sana wazee hao.

Naomba hili lisijirudie, na serikali ifuatilie na ikibidi kubadili mfumo wa ulipaji wa fedha za wanufaika.
 
Uzuri ni kwamba kijijini kwetu hao walengwa wa TASAF, walikiwa hawataki maendeleo ya kijiji ni watu sugu kwenye kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya jamii husika, wakajiandikisha TASAF kwamba ni kaya maskini, ila kukicha wanapigishwa kazi na wanaenda,barabara ndogo ndogo na mitaro imekuwa safi.
 
Back
Top Bottom