Sakata la viungo vya binadamu IMTU, Big picture

Sakata la viungo vya binadamu IMTU, Big picture

Mwanafunzi anajifunza kila kitu ikiwa ni pamoja na wapi atapata hiyo miili ya watu, ataihifadhi vipi, ataiketeza/au ataificha vipi. ANAHUSIKA na ni shahidi na. 1

Unataka kutuambia wanafunzi ndio kazi yao kutafuta hiyo miili ya kujifundishia?, ina maana hata vifaa vingine vya maabara ni kazi yao kuvitafuta?! Kama ndio hivyo uongozi wa chuo utqkuwa na kazi gani?
 
Je wajua Inventor/Discoverer wa Incinerator ni mtanzania?

Anaitwa Prof. Samwel V. Manyelle ambae kwa sasa ni Chief Goverment Chemist.

Sijui Nchi yetu tuna matatizo gani..hatupendi kuwakubali wataalam wetu na kuwatumia...
leo Muhimbili wanadai wataalam wa kurekebisha incinerator yao wanatoka nje ndo maana miezi saba inapita hawajarekebisha hiyo tanuru..

IMTU nao ttzo incinerator..Tuwatumie wataalam wetu wazalendo mambo yaende.
 
ni wale marehemu wanaotumiwa na imtu kufundishia

kadava hawatumiki imtu tu daktari yeyote dunian anapitia hilo kama hauna jibu la maana kaa kimya sio unatoa majibu ya ovyo
 
Mwanafunzi anajifunza kila kitu ikiwa ni pamoja na wapi atapata hiyo miili ya watu, ataihifadhi vipi, ataiketeza/au ataificha vipi. ANAHUSIKA na ni shahidi na. 1

kama haujui tulia dada!! kwa taarifa tu unapoingia cadaver room hauruhusiw kutoka hata na gloves ambazo umezitumia humo ndani kazi ya mwanafunzi ni kuitumia kwa kujifunzia tu suala la kuitafuta,kuihifadhi na kuiteketeza na jukumu la taasisi husika na kwa kesi kama hii sion sehemu ambayo mwanafunzi anakosa!
 
Makubwa sana hayo mkuu, huyu cholera tu au dislocation. ...kama sio deep sitted abscess ya takko
Mkuu watu wanaongea tu kwa sababu ni wazima..ila pakichimbika unafikiri mtu atauliza hata dr kasoma wapi..?!
 
Mwisho wa ubaya aibu,haya ndo matokeo ya urasimu unaokuwa ukifanyika katika nchi hii,vigezo na masharti ya uanzishaji wa vyuo na hospital hauzingatiwi kabisa,cha ajabu ukienda kukagua utakutana na Certificates kibao,sijui ISOO 2006,TBS,TCU,n.k unajiuliza hivi hawa watoaji vibali hivi walizingatia nini?hupati jibu.
 
Unataka kutuambia wanafunzi ndio kazi yao kutafuta hiyo miili ya kujifundishia?, ina maana hata vifaa vingine vya maabara ni kazi yao kuvitafuta?! Kama ndio hivyo uongozi wa chuo utqkuwa na kazi gani?

Sijasema ni kazi yao kutafuta ila ni lazima wajue inapatikana wapi, inatunzwa vipi. Utakuwa mwanafunzi wa ajabu usipokuwa mdadisi na kujua vifaa unavyotumia vinapatikana wapi hasa vifaa vya aina hii..... hata kama wewe si mnunuzi.
 
Wadau mbona mnaumiza vichwa?IMTU Menejiment haiwezi kuwa dhaifu kiasi hicho kiasi cha kufanya upuuzi huo.My take this ningekuwa nahusika na upelelezi wa suala hili wahusika ningewakamata kama panzi.Mind you trace ya kwanza iwe wizara ya afya na pili iwe Muhimbili then mtapata jibu.Swali la kujiuliza hapa Cadaver za mazoezi ya nyuma zilipelekwa wapi?Serikali naomba ijpange kusimamia watendaji kazi wake waachi njaa kwenye inshu sensitive kama hizi.IMTU wapewe onyo kali wasiruhusu tena upuuzi huu.
 
Kwa kweli ni uzembe wa hali ya juu chuo cha udaktari kuendeshwa bila INCINERATOR, uongozi wa IMTU sidhani kama wana lolote la kujitetea!!! afu inakuwaje chuo kinaitwa international wakati kimeshindwa kutimiza hata "local standards"?kama Tanzania ni maarafu kwa ukanjanja basi tusiulete katika afya za binadamu!!!
 
Kumthamini na kuheshimu binadamu mwenzako sio katika uhai tu hata katika kifo.

Hebu jiulize daktari aliyepata mafunzo kwenye chuo ambacho wakufunzi wake wamekosa ethics kwa kiwango kikubwa kiasi hiki ataweza kweli kumthamini mgonjwa akienda kwake kupata huduma!!!!!!!!!!!

Ndio maana professionals wengi siku hizi hawana maadili, wanajifunza from the best waliobobea katika kuiuka kanuni na kuvunja sheria. Wanafunzi wanaona lecturer kafanya jambo fulani and he got away with it, hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake na wao watafanya tu wakijua hakuna adhabu juu yao.

Ndio maana kila mahali unapoenda kutafuta huduma watendaji wako wako tu sio walimu, madaktari, polisi, waandishi wa habari na hata hao wanaotoa matamko kama wangekuwa wanafanya kazi zao ipasavyo sidhani kama kuna institution yeyote ya afya ingekosa incenerator

Hii serikali yetu inashindwa kusimamia vizuri sekta afya ambayo ni muhimu sana!!! Lakini muathirika mkubwa ni mwananchi wa kawaida wao na familia zao wakikooa kidogo wanapanda ndege wanakwenda APOLLO, INDIA
Katika hali kama hii unategemeaje kuwa na taifa lenye uzalendo??
 
Eti serikali imeunda tume ya watu 15 kuchunguza wahusika,hivi kuna haja ya tume hapo?ikiwa dereva aliemwaga wanae,si wamuhoji alitumwa na nani na aliyemtuma aliagizwa na nani, wachukuliwe hatua wahusika, chuo kiendelee mchezo uishe.
Mi hiyo tume naona ni mpango wa kula pesa ya mlalahoi,kila kitu tume tume tume,vingine havihitaji tume.
Na si hesabu zote mpaka utumie calculator kupata jibu.
 
Eti serikali imeunda tume ya watu 15 kuchunguza wahusika,hivi kuna haja ya tume hapo?ikiwa dereva aliemwaga wanae,si wamuhoji alitumwa na nani na aliyemtuma aliagizwa na nani, wachukuliwe hatua wahusika, chuo kiendelee mchezo uishe.
Mi hiyo tume naona ni mpango wa kula pesa ya mlalahoi,kila kitu tume tume tume,vingine havihitaji tume.
Na si hesabu zote mpaka utumie calculator kupata jibu.

Have the really formed a commission, kazi yao itakuwa nini sasa kama sio kula pesa zetu kama kawa
 
Mimi kwa mtazamo wangu, naona kuunda tume ni kuzidi kula hela za walipa kodi tu waziri wa afya ajiuzuru kwanza mambo mengine yatafutwa. mambo ya kuunda tume, kutumia hela ya walipa kodi kwenye hiyo tume, ni sawa na kutupiga tope usoni tu. Mh Kikwete piga chini waziri kwanza kwasababu vijana wake hawajatekeleza majukumu yao ipasavyo badala yake wamekuwa wakipokea mishahara bule.
 
Kama ilivyo kawaida ya Nchi yetu, ni Nchi inayoendeshwa kwa matukio, tukio lililopo kwenye peak kwa sasa ni hili la IMTU na masalia ya viungo vya binadamu, Cadaver remains, si lengo langu kushabikia kile kilichofanyika kwani ni kinyume kabisa na maadili ya kidaktari,Medical Ethics ,na haki za binadamu, Human rights. Hatua stahiki inabidi zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Kumejitokeza mtiririko wa matamko mbalimbali,ikiwemo la MAT, Chama cha madaktari Tanzania, Human Rights Center etc, na tutegemee matamko mengine kufuatia. Siyo kitu kibaya ,wanatimiza wajibu wao kuonyesha wako 'alive",( justification for their existance).

Swali la kijiuliza ni iweje kunapotokea tatizo ndo tuone mtiririko wa matamko, kwanini tusiwe na utaratibu wa kuzuia mapema, iweje chuo na hospitali kubwa kama IMTU isiwe na INCINERATOR, ( ikumbukwe mwanafunzi mmoja wa IMTU analipa karibia milioni 6 za tuition fee, kwa wale wa kozi ya udaktari,kuna wanafunzi karibia 800 wa kozi hii, achilia mbali kozi zingine za maabara na Nursing, kweli hawa jamaa wanashindwa kununua incinerator hadi wategemee ile ya Muhimbili, ambayo tunaambiwa ni mbovu ndo maana wakaishia kwenda kutupa viungo hivi huko Bunju, kweli hawa jamaa wanapiga hela, (BIG PROFIT with low running cost ) mashine ya kuchomea taka, tunajua hospitali ni mahali panapozalishwa taka nyingi, Infectious and Biohazard wastes iweje hospitali iendeshwe bila kuwa na mfumo maalumu wa kuteketeza taka, mamlaka husika zinakuwa wapi, wizara ya afya, wizara ya mazingira, wizara ya elimu,Tume ya vyuo vikuu, Medical Association of Tanzania, MAT na wadau wengine, ikiwemo wa nje ya Nchi, make chuo chenyewe kinajitambulisha kama "International" Medical and Technology University,IMTU, je kinakidhi viwango vya kimataifa au ndo yale yale ya Saint flani flani international academy/ English medium school kama tunavyoona kwa hizi shule za english medium school.

Je hakuna utaratibu wa mara kwa mara kuangalia ubora, frequently quality check up kuanzia kwenye curriculum development and adherence, students recruitment/entry grades,staffing/human resources na miundo mbinu,Infrastructures. Kuna taarifa kulifanyika assessment kwenye hiki chuo,ilifanywa na baraza la madaktari wa binadamu na kinywa la Africa Mashariki, ( Medical Association of East Africa) mwaka 2010, mojawapo ya final recommendation ilikuwa ni chuo kisimamishe huduma hadi pale kitakapokidhi 'minimum requirement criteria, je utekelezaji wake uliishia wapi? au ndo mambo ya Nchi ya kitu kidogo.

Pia kuna hili tamko la kukifungia chuo, inawezekana ni tamko stahiki, lakini je tumefikiria hatima ya wanafunzi waliopo hapo chuoni, kuna karibia wanafunzi 1000, wataenda wapi, tukumbuke kuna walio mwaka wa tano, mwaka wa nne, mwaka wa 3, mwaka wa pili,na wa mwaka wa kwanza, waende wapi, na tukumbuke IMTU ndicho chuo chenye Tuition fee kubwa zaidi kuliko vyuo vyote hapa Nchini, wazazi na wanafunzi wataathirika kwa kiasi gani?, is it fair?

Tafakari.

Mwandishi ni medical professional.
Kwanza chuo kilianzaje bila kuwa na Kichomea taka? Au sheria hiyo haihusiki na Vyuo vya Kidakitari? Huku uraini hauruhusiwi kufungua Dispensary bila incinerator , hivyo kusema kukifungia ni to deal with effect and not the cause. Hakikutakiwa kufunguliwa bila incinerator. Kama kilifuguliwa Mamlaka husika ilitegemea nini?
 
Tatizo nchi yetu huwa hakuna kuwajibika lakini hii ya IMTU ilitakiwa tuone wakurugenzi wa vyombo vya ukaguzi nao wanawajibika
 
Kweli mtoa hoja hapo pana shida ya mnyororo wote kwa kiasi tofauti!!!!!!

Hivi kamati ya bunge inayoshughulikia hii sekta ya afya, mazingira na sheria wamesema lolote???!!!

Ni kweli kabisa, matukio kama haya yanayostua sana wanachi yanaisaidia serikali kupumua kwa kiasi kikubwa sana. Kuna hoja za wizi wa Mabilion ya exc.Account BOT, kuna hoja za Moto kuhusu Katiba Mpya ! Hivyo wajanja wamepata sehemu ya kuwahamisha wanachi toka hoja za kuibiwa 200b BOT, uvurugaji wa Mchakato wa katiba mpya nk nk. kutokea kwa hili la utupaji viungo iwe ni kwa bahati mbaya ama kupangwa ili iwe hivi ilivyo ni faraja kubwa sana kwa serikali.
Daktari aliyeandika uzi huu,amehoji vitu vizito na vya msingi sana,lakini...kwa kuwa utupaji wa viungo hivyo umeisadia jamii kupumbazwa,bado tutegemee matamko mengi huku watoa matamko wakiwa hawana muda wa kujiuliza Maswali kama vile; Ikiwa Incinerator ya Muhimbili haifanyi kazi, Je ? Muhimbili hutumia njia gani SALAMA ya kuondoa/kuteketeza taka ambazo naamini zipo ambazo uteketezaji wake hauwezi kufanywa kwa kuzifukia ardhini au lah.
Kama Muhimbili nitegemeo la Hospital nyingi hapa Jijini linapokuja swala la uteketezaji wa mabaki ya viungo vya binadam ama taka za hospital ambazo ni hatari, kwa sasa nini kinafanyika kufanya kile kilichotakiwa kufanywa na Incinerator ambayo ni mbovu kwa muda mrefu ?
IMTU wametufungua macho, mimi nawapongeza, kwa kuwa iko siku viungo hivi vingetupwa kwenye vianzo vya maji na si ajabu vimewahi kutupwa au kufukiwa maeneo kama hayo, kama incinerator haifanyi kazi kwa muda mrefu hivyo, tuambiwe mbinu ambazo mkemia Mkuu ambaye naye hutegemea Muhimbili kuteketeza taka,anateketezaje take zake ?

Badala ya kujikita kutafuta Mchawi IMTU ni wakati wa kujitathmini kama taifa na kukataa upuuzi wa aina hii.
Ni aibu kwa Hospital ya taifa kutokuwa na Incinerator kwa sababu iwayo yote.
Tungekuwa waungwana wengi wangewajibika si kwa tendo la IMTU bali kwa udhaifu mkubwa uliojionyesha kutokana na kitendo cha IMTU.
 
Back
Top Bottom