Cadaver ni miili ya marehemu au marehemu wanaotumika kufundishia somo la maumbile ya mwanadamu(Anatomy) kwa wanafunzi wa vyuo vya tiba kama MUHAS, KCMC na hawa International Medical and Technological University(IMTU) waliosababisha taharuki kwa kutupa hadharani viungo mbalimbali vya Cadaver, Cadaver hupatikana kwenye matukio ya ajali ambapo wale marehemu wasiotambuliwa na ndugu zao huhifadhiwa kwa muda wa kama mwaka mmoja then kama hamna ndugu yeyote aliyejitokeza kudai huo mwili hutumika kama Cadaver, wengine hupatikana kwa kujitolea wenyewe mfano mtu anaandika 'Will'(wosia) kwamba akifa mwili wake utumike kama Cadaver ya kufundishia wanafunzi wa chuo cha tiba, mambo haya hufanyika kwa siri sana na kuna mbadilishano wa Cadaver kati ya nchi moja na nyingine kuepusha mazingira ya uwezekano wa mwanafunzi kukuta mwili wa ndugu yake kutumika kama cadaver, miili hii hudungwa sindano ili kuzuia kuharibika ili itumike kwa muda mrefu na baadaye huharibiwa kwa kuchomwa moto kwenye matanuru maalumu(incinerators) au kuzikwa kwa usiri sana