Sakata la Richmond na Maoni yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Richmond na Maoni yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by amanijuuyako, Mar 3, 2008.

 1. a

  amanijuuyako New Member

  #1
  Mar 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkasa wa Richmond

  Mkasa huu ulianza wakati Tanzania ilipokua imekumbwa na janga la umeme.

  Rais alitoa agizo kwa wizara kufanya juu chini hili suala la umeme litatuliwe.

  Waziri mkuu ndiye aliyetoa wazo kua tnder wasipewe Tanesco ( Tanesco ipo chini ya Kampuni kutoka South Africa na imegundulika kampuni hii ni wezi an ilikuwa kunamipango ya kuwatoa. Kwa hivyo wangepewa tendar hii ndikama kuwaengezea muda. Hoja ilkuballika na kutafutwa watu wengine)

  Tendar ikatolewa kwa makampuni ya kitaifa na mataifa ; waweze kuleta jibu la kuweza kuleta turbines kwa haraka sana.

  Ununuzi wa turbine hizo nitafauti na ununuzi wa baiskeli au gari.
  Lazima utoe maelezo specification halafu company zianze kutengeneza michoro ndio wakupe bei. Kutokana na muda ulikua mdogo kampuni tatu tuu zika jitokeza ikiwemo Richmond.

  Kampuni ya Richmond ndio iliyotoa uhakika kimaandishi kuwa wataweza kuleta hayo mageneretor kwa wakati unaotakiwa.

  Mkutano wa mawaziri ukafanywa na kuelezwa kilichotokea na kukubalika Richmond wapewe hiyo tenda. Baada muda ulowekwa kufikia na hakuna kilocho fanyika.
  Aliyekua waziri mkuu akaandika barua kutaka mkataba uvunjwe.

  Waziri wa wizara husika na katibu wake na mwanasharia wakenda kummbembeleza aliyekua Waziri mkuu kua asivunje mkataba kwani wawo wamesha zungumza na Richmond na wameomba muda kidiogo ili wapate kutimiza jukumu lao.

  Kikao cha mawaziri kiliitwa nakupashwa habari kua Richmond wamehakikisha kua wataweza kutimiza jukumu.

  Waziri a kapewa go ahead na kikao na mkataba usivunjwe.

  Kima cha Maji ya bwawa yalipo anza kupanda suala lile likaisha nguvu.

  Na hatimaye yakatokea yaliyojiri hivisasa.

  Lowassa alikua najua kinachotendeka na kaona ajitete mapema.
  Baada ya yeye kuiona report yote ndipo aliposhangaa kuona kua yeye ahajaitwa na pili ile barua yake alo muandikia waziri kuhusu kuvunja mktaba haikutiwa wala hakuna maelezo yoyote yale yanohusu kuvunja mktaba.

  Ina semekana kua alimpa Speaker nakala ya barua hiyo
  Kilichotokea bungeni baada ya ripoti kusomwa ni kua speaker hakuongeza kitu ndipo alipoona hakuna haja ya kujitetea Nadahani katika fikra zake ali hisi kua yeye ndie kafara wa sakata hilo kwa hivyo bora jiuzulu.

  Na hayo ndivyo tuonavyo sisi.

  Alokuamo hatoki na asokuamo haingii
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  karibu sana amani jamvini!
   
 3. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Karibu amanijuuyako, Karibu sana JF

  Nadhani unachokifanya hapa ni kujaribu mtetea ndugu Fisadi Lowassa, lakini kumbuka Process nzima ya Richmonduli kupata tender ilielezewa kwenye Kamati teule ya Bunge, na kuonyesha vigezo, (i.e Barua zilizokuwa zinatoka ofisi moja kwenda nyingine), Hivyo maelezo yako yanapishana na yale ya kamati kwa kiwango fulani

  Jaribu kulitetea Taifa lako na wananchi, usipoteze muda kutetea Mafisadi kama akina Lowassa na wengineo please, Tumeshasoma mengi kuhusu Lowassa na tumeelewa kuwa ni Fisadi completelly, hivyo asafishiki hata kwa Magadi

  Karibu sana JF tuangalie jinsi ya kulikomboa Taifa letu tukufu
   
 4. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kwi kwi kwi,

  yaani nimecheka sana hii ya kuwa Lowasa hasafishiki hata kwa Magadi. Mimi ninaongea na bi senti 50 ili anipe contact za Lowasa ili na mimi nianze kupokea mshiko wa kumtetea hapa JF!!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh teh teh Lowassa mwenyewe ameamua kuingia JF, karibu sana Mbunge wa Monduli...nasikia ulighalamikia yake mapokezi hahaha siasa bwana mchezo mchafu, JF itahakikisha unafutika kabisa katika siasa za Tanzania...karibu uchangie
   
 6. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  jamani mbona mmesahau ile hadithi ya karibu mgeni,kwani mgeni siku ya kwanza mpe chai na mkate,tena sema karibu.sasa ninyi siku ya kumi ndio mmeifanya ndio karibu mgeni,tuende taratibu wasijekimbia hapa kwani tunaitaji maoni yao.karibu sana nndugu yetu na ujisikie upo nyumbani
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..amani,

  ..ehe,halafu ikawaje? mbona story yako haina flow nzuri.

  ..kwahiyo,hoja yako ni ipi?
   
 8. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwanza karibu sana jamvini JF na jisikie uko huru kusema utakalo kama ulivyofanya ila uwe tayari kukosolewa bila kutumia jazba.


  Ni kweli ununuzi wa gari ni tofauti na turbines lakini je Hizo Kampuni Richimonduli et al wao walikuwa wanazitengezaje haraka kiasi cha kufanya wengine washindwe???

  Mkataba wowote una timeframe kwamba ikifikia wakati fulani tutakamilisha, baaada ya hayo yote ya kuongeza muda bado walishindwa kutimiza makubaliano alichukua hatua gani huyo unaemtetea?

  Huyo unaemtetea Kwa nini hakutumia mamlaka aliyopewa kikatiba kuvunja mkataba?? ama waziri =waziri mkuu????

  Wewe hujakiri lakini Lowasa amekiri alijua Richimonduli ni matapeli kwa nini hakusema hadi baada ya repoti ya kamati????

  karibu jamvini lakini pitia mada ya richmond yote ujue kilichojadiliwa hapa ili usiendelee kurudia mada.

  Mods kama hamtajali iunganishwe na ile ingine ya richmond
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  karibu sana JF,

  maoni yako tumeyapokea kwa mikono miwili......na karibu sana uelimike.............hapa JF hapendwi mtu, tupe hizo facts hiyo tenda iliitishiwa wapi na nani alifanya evaluation....tunataka kuwafahamu wengi zaidi walioshiriki

  swali..............hivi unajua kwa nini watu(Client/Serikali) inaamua ku-hire services za mtu ili kupata product fulani????....maana wakati mwingine inabidi turudi kwenye BASICS

  pili tunashukuru sana kwa taarifa kuwa Mwanyika alienda kumuomba aliyekuwa Waziri Mkuu kuwa asivunje mkataba (very funny though)

  Je Hiyo barua aliyopewa Spika ndio ile imo kati ya baadhi ya docs ambazo Mwakapugi PS Nishati alimuagiza muwakilishi wake asiwaonyeshe akina Mwakyembe?

  hebu tupe data mwanangu

  na usisahahu kumsalimia Askofu Laizer (anaye toa baraka kwa mafisadi), Ole naiko, Lukaza na Nyari.........tell them JF inawamulika na tutawashia moto wakti wowote!!

  tik tak tik tak tik tak
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Heshima yako Mzee Ogah, maneno mazito sana haya, nimecheka sana....nadhani huyu jamaa hatarudi na utetezi wa kifisadi hapa atakapoenda kukutana na akina Ole, Lukaza, Nyari na baba Askofu wao ataawambia JF hawalei mafisadi....
   
 11. L

  Lione Senior Member

  #11
  Mar 4, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wakuu!,Idumu JF,Walaaniwe mafisadi,na watetezi wao,walaaniwe pia wale waliopewa jukumu kuwaongoza kondoo wa bwana,wakawageuka na kuumbatia ufisadi,nazungumzia viongozi wadini katika hili,naamini mzee wa ukuni uunguao naye hakosi,
  Sasa nianze kuchangia mada!
  Kama ambavyo mkulu mwanakijiji alivyo tudokeza hapo mwanzo juu ya ujio na kusudio la kundi jipya la AGENDA 21,nimeanza kuonza kazi zao humu JF,kama huyu bwana alivyo mtetea bwana lowasa na kumkandamiza bangusilo msabaha.
  Nataka Kumuuliza Anamjua Nyari?kwanini nyari anatumiwa na mamvi?mnakumbuka jinsi ilivyoandikwa kuhusu mapokezi ya el kule monduli?unadhani ni kweli watu wa kule wanampenda vile el?kama unafiri ndio,umekosea,they dont like him,they know that he is not maasai,na anatake advantage yao,kwakua kwao yeye ni mpwa wao tu,pili,ule umati wa watu mliouona,ulinunuliwa,harakati za kutafuta tax bubu kwa ajili ya mapokezi yake,zilifanywa na nyari,akisaidiwa na vijana wake,wakawa wanawalipa elfu kumi,na nusu tank ya mafuta kwa kila gari,na kila ataepeleka watu wa nne,atapewa elfu mbili kwa kila kichwa,uliza vijana wa tax pale arusha mjini watakuthibitishia hili,na uwepo wa askofu laizer pale ilikua kuwavuta tu wengine walioko pale monduli mjini,kwakua katika jamii zetu vgiongozi wa dini wananafasi ya kipekee,so mzee laizer alitumiwa ither kwa kujua ama kutokujua,kwa hiyo kama hakua na hatia asingetumia gharama zoote hizo kukodi watu,ama ndege kwenda kule kwao,na kama kweli anakubalika kule alikodi watu wanini?jibu ni kwamba hawamkubali!
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Naona ndugu yangu Hujui chochote juu ya RICHMOND na labda nukupe dondoo za Ki mathematica unaweza ukanielewa labda

  Data:
  1: Rejea sensa ya watu iliyopita

  Kuna watu wapatao 40 milliona katika Tanzania

  2: Kila siku Tanesco/Serikali inalipa pesa za walipa kodi zipatazo 152 Million kwa Richmond kisha Dowans

  Annalysis:

  Ukichukua total money = 152 Millions/40 Walalahoi Jibu lake ni 3.8 Million/Mlalahoi.

  Ina maana Serikali ingeamua kufumba Macho na Kuchukua Uamuzi wa Kiendawazimu (Labda pengine wa Kishujaa) Kila mlalahoi hadi wewe ungepata 3.8 Millions per day:

  Kumbuka ni mkataba wa miaka miwili ambayo ni siku 365*2 = 730 days

  Ina maana kwa hesabu za darasa la tatu ni kwamba Serilkali ina uwezo wa kuwapa wananchi wake shilingi 3.8 Millions * 730 days= naomba unipe Jibu.

  Sasa kipi bora Serikali kulipa fedha watu wasiojulikana au Ingewapa wananchi hizo Pesa?

  Jibu unalo kaka mimi sipo
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Amani juu yako, vyovyote vile itavyokuwa Lowassa hateteeki kwa hili, he was supposed to be on top of his work, sio atoe amri fanyeni hivi fanyeni vile. Wakati Tanzania iko kwenye Janga kama lile la umeme ilitakiwa awe analishughulikia hilo tatizo yeye mwenyewe na si kuagiza tu.

  Kwa hili mimi naona kama hana makosa direct basi ana makosa indirect na inapaswa awajibike/awajibishwe kama alivyofanya/nywa na asubiri tume ya MP kwa hatua zaidi zinazofuata bila hivyo wananchi hawatokuwa radhi.
   
 14. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kweli JF tumevamiwa, Hivi hizi Hesabu ni za wapi?
  Jamani nisaidie mimi labda sijui
  155 Milioni Shiling/40 milioni population = 3.8 milion shiling/per person/ per day????

  Naomba tuwe makini kwenye kuchangia hizi point jamani, tusiandike tu kwa sababu tunataka nasi tuonekane
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Ina maana jamaa kakosa support? Dah, Lowassa alikuwa na gundu basi! KadaMpinzani pls, kama upo do something buddy :).

  BTW: Mwanzisha mada harejei kutoa mwendelezo wa mada yake? Au ni Mhe. Lowassa aliamua kuingia mwenyewe?
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Maelezo yako na ya Lowasa yanafanana, Lowasa anakiri kufahamu ubabaishaji wa Richmond hata akaandika barua ya kuomba mkataba uvunjwe:

  Swali:

  Kwa nini Lowasa hakujitokeza hadharani KUMSHUSHUA Edward Hosea alipotoka na Report yake ya kuisafisha Richmond?

  Aliunga mkono kwa mbwembwe nyingi, huyu alikuwa anajua alichokuwa anakifanya

  Hatuwezi kumtenganisha na Ufisadi huu
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Mkuu, samehe na saidia bure. Atakuwa alighafirika kidogo. Kumbe uliishtukia sio?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mjomba hapo umechemsha sana tena kwenye mahesabu yako, duhh, halafu unajiita ndege ya uchumi, jibu la hesabu zako ni hili:

  [SIZE=+1]152000000 / 40000000 = 3.8 hizi ni shillingi tatu na senti themanini kwa siku.[/SIZE]


  [SIZE=+1]3.8 * 730 = 2774 hizi ni shillingi elfu mbili mia saba na sabini na nne kwa miaka miwili.[/SIZE]

  Hilo ni jawabu kutokana na figure zako ulizotowa
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mniwie radhi wana JF, nilighafilika kidoogo, nadhani kwa sababu ya Hasira kwa Mafisadi
   
 20. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  nauliza hivi katika mchango aliyotoa dr slaa bungeni wakati wa sakata la richmond alimtaja mwanasheria mmoja mwanamke kuwa alihusika na ufisadi.lakini mbona watu wamekaa kimya na bunge lilikaa kimya? na katika riport ya mwakyembe alitajwa mkurugenzi wa takukuru sasa hawa watu mbona hatusii wakiwajibishwa?
  jamani nisaidieni majibu hatutaki aachwe mtu katika ufisadi wote wawajibishwe
   
Loading...