Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Magufuli achafua hali ya hewa Dar
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli amechafua hali ya hewa na kuingia kwenye mgogoro na wakazi wa Kigamboni, Dar es Salaam baada ya kuwaeleza kuwa ni lazima walipe nauli mpya za vivuko vya Mv Kigamboni na Alina na kama watashindwa, wapige mbizi baharini kuvuka. Kauli hiyo ya Dk Magufuli imekuja siku mbili baada ya wizara hiyo kutangaza viwango vipya vya nauli mnamo Desemba 29, mwaka jana ambavyo vimepanda kwa asilimia 100 na vilianza kutumika jana Januari Mosi nchi nzima.
Akizungumzia tukio hilo, Msemaji Mkuu wa wizara hiyo, Martin Ntemo alisema Waziri Magufuli hakufurahishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumzomea wakati alipokuwa akizungumza... "Amechukizwa na baadhi ya watu kuzomea wakati alipokuwa akizungumza. Alichokuwa akisisitiza ni kwamba nauli mpya lazima ilipwe lakini wapo waliokuwa hawataki kuelewa wakawa wanapinga." Alisema kuna watu walikuwa wamepangwa kufanya mgomo kupinga nauli mpya kitendo ambacho pia kilimkera waziri alipokuwa kwenye ziara hiyo.
Magufuli na waandishiBaada ya kuzomewa Kigamboni, Dk Magufuli alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kwamba, "Kuanzia Januari, Mosi, mwaka huu Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), imeongeza viwango vya nauli katika vivuko vyote vya Serikali nchini." Alisema kwa muda wa miaka 14 iliyopita Kivuko cha Kigamboni kimekuwa kikitoza nauli ya Sh100 kwa mtu mmoja, wakati vivuko vingine vyote nchini, vimepandisha nauli zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1997 kuendana na gharama za uendeshaji. "'Kwa mfano, Kivuko cha Pangani ambako umbali wa uvushaji hauzidi ule wa Magogoni kilikuwa kinatoza Sh 200 na hali ya uchumi kwa wananchi ni ya chini kuliko Dar es Salaam. Kivuko cha Kilombero kilikuwa kikitoza Sh200 ikilinganishwa na Sh100 zilizokuwa zikitozwa hapa Magogoni."
Alisema hilo liliwahi kufanywa na na Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart mnamo Aprili 17 hadi 20, mwaka jana kwa makubaliano na Temesa. "Zoezi hilo liliendeshwa tena Septemba 16 hadi 20, 2010 na Wizara kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi." Alisema Julai, 2011, Temesa iliamua kubadili wakata tiketi na kuajiri wengine akisisitiza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kupambana na matukio ya watumishi wasio waaminifu. Hatua nyingine ni ile ya Temesa kuondoa askari wa kuajiriwa na badala yake kuingia mikataba na kampuni za ulinzi. "Kwa sasa katika Kivuko cha Magogoni, Kampuni ya ulinzi ya Suma JKT ndiyo inayotumika kufanya kazi hiyo," alisema.
Alisema juhudi hizo zimesaidia kuongeza mapato kwa siku kutoka Sh5.5 milioni mwaka 2009 hadi Sh9 milioni kwa sasa katika Kivuko cha Magogoni na kusisitiza kwamba wizara itaendeleza hatua hizi kwa lengo la kubana uvujaji wa mapato na matumizi yasiyo ya lazima kwa vivuko vyote. Magufuli alisema kwa utaratibu, watumiaji wote wa huduma za vivuko wanatakiwa walipie huduma hiyo na kuongeza: "Tunaomba utaratibu huu uzingatiwe isipokuwa kwa wanafunzi waliovaa sare za shule. Tunasisitiza watumiaji wa vivuko waheshimu sheria na taratibu zote za vivuko kwa ajili ya usalama wao na ufanisi wa huduma."
Mbunge achukizwa
Kwa upande wake Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alikiri kusikia maneno ya Magufuli ambayo hayakuwafurahisha wapiga kura wake na kuahidi kuendelea kufuatilia kujua undani hasa wa kauli hizo. Dk Ndugulile alifafanua kwamba baada ya tangazo hilo la ongezeko la nauli, aliwasiliana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki na taarifa alizonazo ni kwamba nauli hizo zimesitishwa.Alifafanua kwamba baada ya kuwasiliana na waziri mkuu, jibu alilopata jana saa 1: 00 usiku ni kwamba mpango huo wa kupandisha nauli umesitishwa hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
"Sasa angalia hivyo vigezo, utaona mwananchi wa kawaida amezidi kuumizwa. Leo hii tayari bei za bidhaa zinazoletwa Kigamboni kutoka sokoni kama Kariakoo kwa kutumia maguta zimepanda. Mtu mwenye gari anapadishiwa bei chini ya mwenye guta, vigezo gani hivi? Baada ya kuona hivyo, niliwasiliana na Waziri Mkuu Ijumaa (Desemba 30, mwaka jana) na jana Mkuu wa Mkoa akanipa jibu kwamba Waziri Mkuu kasema nauli hizo zisipandishwe kwanza. Kwa hiyo mimi na wananchi wangu tunajua hivyo," alisema na kuongeza: "Hili ni jambo la ajabu sana. Yaani Waziri Mkuu anasema hivi halafu waziri wake anafanya vingine! Uko wapi sasa utendaji kazi wa pamoja wa Serikali?"