Sakata la nauli za vivuko: Magufuli asema asiye na nauli Sh. 200 apige mbizi

Inahuzunisha sana pale mmoja wa wachache waliodhaniwa wanajali wananchi anapoonyesha rangi zake za kweli, mwananchi wa kawaida ana wakati mgumu sana Tanzania....Halafu anachukizwa na kuzomewa,amezoea sifa sasa anapokosea anatarajia wazidi tu kumsifia. Dr Faustine tetea wananchi wako hadi kieleweke!
 
" pigeni mbuzi mkishindwa kulipa" hii kauli ya kustusha, kiongozi kupandwa na hasira katika hadhira ya wanchi ambao kimsingi ndo waajiri Wako ni ubinadamu Lakini kutukana, lugha za kebehi, na vitisho hiki ni kiburi,
 
Jamani watanzania wapenda amani na mnaopendana je, msukuma guta ataweza kulipa 1,317,600/= ili aweze kuvuka kivuko cha kigamboni kwa mwaka mzima(3600 x 366) ???
 
Safi, kazi nzuri. Hivi mnapolalamika juu ya huduma mbovu za serikali mnafikiri hela zitatoka wapi? nasema tatizo labda ni kuwa walikaa muda mrefu bila kupandisha na hilo ndiyo tatizo, wananchi kama vile wamefanya ni haki yao, mfano ukiwa unamletea mkaa/mchele baba mwenye nyumba uliyepanga kila unapotoka safari, siku ukiacha atakudai, wananchi kwa hili watazoea!
 
"mtu asiyetaka ni vyema akapiga mbizi kwa kuogelea kutoka Kigamboni hadi ng'ambo ya pili au apite Kongowe kuingia katika katikati ya jiji." Moja ya sifa zinazomjenga kiongozi ni uwezo wake mkubwa wa kuhimili hisia, ambazo zinweza kumpelekea akawa na Jaziba...na mara zote wataalamu wa "Ushuruzi" Psychology husema ukigubikwa na hasira na jaziba huwezi kufikia maamuzi sahihi kwa kuwa utakuwa hutumii akili bali hisia...Sasa leo Waziri anaetumia maneno ya kejeli na ufedhuli didhi ya wananchi wake ni jambo la kutilia shaka uwelewa wa Maghufuli....au kwa kuwa yeye ana VX so hilo halimhusu.....
 
guta 1800 na gari 1500...huu ni upuuzi wa hali ya juu kabisa...
Hili guta linaloongelewa hapa ni lile ambalo liko full na mzigo wake wa viazi juu, labda tujiulize wakati wa kurudi lishashusha mzigo kariakoo linatozwa tena 1800 au ni chini ya hapo?
 
Kwani wakazi wote wa kigamboni ni watumishi wa serikali? kwa nini kigezo cha kupandisha nauli anatumia mishahara ya watumishi wa serikali?
 
Mwenye guta sio mlipaji, mlipaji ni mwenye mzigo. Vivyo hivyo ukikodi tax kwenda nayo kigamboni, mwenye kukodi ndie mlipaji wa ushuru huku mwenye tax akidai gharama zake za msingi. Watu wamekuwa wakiacha kuchukuwa pickup na badala yake kuchukuwa maguta kwa ajli ya urahisi. Sasa wakati umefika wa watu kukodi pickup ambapo kuna faida ya mdishaji kupanda ndani ya gari yenyewe na kuachana na hizi tabia za akina dada na mama zetu kudandia maguta ambayo yamebeba mizigo yao kitendo ambacho kinahatarisha hata usalama wao. Kuna wakati wenye mikokoteni kwa kuzidisha mizigo wamekuwa wakisababisha ajali pale wanaposhindo kuidhibiti kutokana na mizigo mikubwa. Mimi binafsi nina taarifa za majeruhi mbali mbali wakiwamo abiria wa kawaida. Lakini hata wenye maguta na mikokoteni wamekuwa wakiumia.

Endapo biashara hii itawashinda, watafute biashara nyingine. Tena nashaangaa leo tunawatetea wakati humu humu tuliafiki wazo la SUMATRA kuzipiga marufuku kuingia maeneo ya mjini
 
kwani madaraja yaliyovunjika katika mafuriko ya Dar es salaam ukarabati wake au matengenezo yake wakazi wa huko watahusika kwenye gharama?
 
wadau nchi inaendeshwa katika utaratibu wa TRY AND ERROR tutafika tu.
Cha msingi tuombe error zisiwe nyingi.
 
magufuli kwani kutopandisha nauli ya kivuko kwa miaka 14 ni kosa la wakazi wa kigamboni au wizara yako...nani anawajibika kwa hili kosa?
 
Watz wengi hawataki mabadiliko na wanapenda dezo. Baba wenye nyumba kila siku wanapandisha kodi, hatusikii kupiga kelele. Iweje watu wa Pangani na Kilombero walipe nauli kubwa kulko wa Kigamboni??? Huyo Mbunge wao anafagilia kitumbua chake na wala sio uhalisia. Wananchi tubadilike, kila siku gharama za uendeshaji kivuko zinapanda, kwani nauli ibaki palepale
 
Magufuli mbona unazungumzia sana nauli za abiria badala ya zile zilizopanda maradufu? nauli ya kuvuka abilia kutoka 100 hadi 200 si jambo la mjadala sana twende maeneo mengine kama vile Guta kutoka 200 hadi 1800 na bajaj kutoka 300 hadi 1300 na gari dogo kutoka 800 hadi 1500 na watoto wa chini ya miaka 14 kulipa 50 na wa shule akiwa na sale bure hata kama ana miaka 18 lakini yule wa miaka 8 analipa kwa sababu hakuvaa nguo za shule
 
Ndio tabu ya kula na kuvimbiwa, unasahau kabisa kuwa kuna wengine, ni mashuzi tuuuu!!! haya sasa....
 
Hata kama lengo ni kukusanya Kodi, ni vyema tufike mahali tuwe ni huruma kwa wananchi wetu. Nauli zilizotajwa hasa kwa vyombo vya usafiri, Bajaj, Gutta na magari madogo hazilipiki na ni mzigo kwa walio wengi. Ni vizuri suala hili liangaliwe upya.
 
Wanajamii, mngekuwa na uwezo wa kujua bei za vipuri hivi toka kwa wenzetu huko Ulaya vinakonunuliwa kwa Euro na Dola mngeona umuhimu wa kupanda kwa nauli hizo. Najua wengi mtaingiza suala la 10%, lakini bila hilo, vipuri hivyo ni vya ghali. Ingieni kwenye mitandao Muangalie Twin disc manufacturers ambao ni watengenezeji wa gearbox zinazotumika kuendeshea mitambo au Schottel manufacturers watengenezaji wa mifumo ya uendeshaji au kama huko ni mbali, basi mtembelee kampuni ya CAT hapo Nyerere road muone bei za vipuri.

Ni jambo la aibu kivuko cha Magogoni kuendeshwa na pesa za maeneo ya vivuko vingine. Ukweli ndio huo! Kuna kivuko kimoja nasikia kinafanya kazi takriban miezi isiozidi sita kwa mwaka. Miezi mingine husimama kutokana na mafuriko na wakati mwingine maji ya mto kukauka. Lakini Kivuko hicho kina watumishi wanaotakiwa kulipwa mishahara na posho zao. Hawa wanasaidiwa na vivuko vingine na ni haki yao. Lakini Magogoni kusaidiwa ni kisa kuogopa kupandisha tu naulli kufikia 200 ni woga usio na msingi kisa kuogopa kupoteza kura za wananchi. Kwa hili, Hongera Dkt Magufuli umethubutu, na wengine wafanye hivyo!

Naamini hata wakichukua nchi wapinzani, kuna gharama ambazo lazima zichangiwe na wananchi, hili halina ubishi. Kama suala ni kutaka kuwasaidia wafanyakazi, tuone jinsi ya kuibana serikali ili ipandishe mishahara na posho mbali mbali na kwa kufanya hivyo, bado tutakuwa tunaendelea kumkamua mlipa kodi wa kawaida.
 
Nimekaa Kigamboni,
Nauli ya Tsh 100/= kwa hakika ni zaidi ya tangu 1998, kutokana na kupanda kwa gharama na kushuka kwa Shilingi serikali ina haki ya kupansisha hii nauli kuwa Tsh 200/= kwa kichwa,
Tatizo ni kauli ya huyu Ma - Lock ndio shida, asingetumia ubabe angeeleweka tu, but ndio hivyo tena ameshasema wapige mbizi lasivyo wasubiri uchaguzi 2015
 
Poleni wananchi wenzangu mnaoishi kigamboni na wale wenye kufanya shughuli zao za kila siku huko Hao ndio Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi yaani ccm lakini naomba niwakumbushe hayo ndiyo matunda ya kuwachagua viongozi wa ccm wenyewe mnaita ushindi wa kishindo Mbunge wenu alikuwa Mjengoni Dodoma wakati wa Bajeti akaunga mkono Bajeti asilimia 100% yeye ahukujua tatizo hilo litakuja kuwakabili wananchi wa jimbo lake?? Huyo jamaa John Magufuli adivyo alivyo alipokuwa Waziri wa Uvuvi na mali Asili alishindwa kuwatetea wananchi wa kanda ya ziwa Bukoba,Mwanza,Mosoma juu ya Uvuvi wenyewe wanaouita Uvuvi Haramu yaani kutumia Nyavu ndogo na Makokoro leo wanchi wa kanda hiyo wanashindwa kula Samaki kama kitoweo matokeo samaki wanakula Weheshimiwa Wazungu kwa vile ndio wenye uwezo wa kumpa fedha ya kigeni wananchi wanakosa lishe bora lakini wenzetu wankuja hapa kwetu wanafurahi na maisha sisi na watoto tunahangaika tupate wapi lishe bora tulishoruhusiwa ni kula Bichwa la Samaki kwa lugha inayofahamika na wengi ni PANKI ndugu zetu wanayagombea mwaloni Mwanza Bukoba na Mara kwao pale Chato wanakula mapanki kwa kujificha. huyo ndiye John Pombe Magufuli wa ccm mwisho nawaomba wananchi wenzangu wa kigamboni muulizeni huyo Mbunge wenu alichokiunga mkono kule Bungeni mia kwa mia ni kitugani ????????????????????? na leo anawaambia wapiga kura wake nini wakati Serikali sikivu ya chama chake imeishatoa uamuzi juu ya hilo? kutofautiana na Boss wake Waziri Mkuu ni jambo la kawaida wote wanajua kinachoendelea. Anatory Mujwahuzia..........................
 
Tatizo letu watanzania mwanasiasa akifanya jambo moja lenye maslahi kwa wa TZ wengi utackia bac agombee Urais.MFANO (a)Mrema baada ya kuwa mtetez wa wanyonge watz walisuggest hivyo
(b)Amekuja jk 2
(c)nakumbuka sakata la Mkataba wa BUZWAGI na Z.KABWE
(d)LEMA na sakata la kujipeleka Jela
(e)MNYIKA juzijuzi hapa
(f)dr. MAGUFULI na ubomoaji wa majengo pamoja, barabara na samaki wake
(g)dr.MWAKYEMBE na ripoti yake
(h)Mzee c6 na upingaji malipo ya Dowans.
Akili zetu watz zimelalia kwenye Urais tu.
 
mvutano wa magufuli na mbunge wa kigamboni (CCM) unaonyesha kwamba mbunge hakushirikishwa japo katika hatua za awali juu ya gharama hizo ambazo zina madhara kwa maisha ya wapiga kura wake. mbunge hawezi kukwepa maswali ya wapiga kura wake katika hili, hivyo anastahiri kuwa na taaifa za awali ili kutoa majibu sahihi kwa wananchi.
.....Labda ni Mbunge ndiye asiyependa kushirikisha wapiga kura wake. Naamini katika hili kama angekaa na Mzee Masoud, yule Mbunge aliyepigania kununuliwa kwa Pantoni pale kiasi cha kufikia hatua ya kutoa shilingi hadi waziri kujiuzuru, mambo yangekuwa mepesi sana, au hata angemshirikisha mbunge aliyeshindwa mwaka juzi, Mwinchumu ambaye mwaka juzi bei ilipopanda yeye moja kwa moja aliandika malalamiko yake sehemu husika na kilichofuata ni serikali kukubali bei iliyokuwa ikitumika iendelee, hakukuwa na press conference.
Natambua fika bei mpya namna zinavyowaumiza wananchi wa Kigamboni, but the procedures, kuna mambo concrete yanayoikabaili Kigamboni ambayo mbunge angewea kuyaongelea, kama vile kuzuiwa ujenzi na kuuzwa kwa viwanja katika maeneo yote ya Kigamboni, lakini hili la kupanda kwa nauli, lingekuwa limeisha zamani kama lilivyowahi shughulikiwa bila mjadala wala airtime kama kama lilivyo hivi sasa.
 
Back
Top Bottom