Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

kuzaa na uongozi mzuri

hawa watu mimi nilishaondoa katika list ya magazeti nchini namaanisha magaeti makini nchini, ndio maana huwa sijisumbua kusoma habari yoyote waliyoandika hata kama inaniihusu mimi au mtu wangu yoyote wa karibu kwani najua hazina ukweli, wanatumiwa au wameamua kuandika tu ili wauze gazeti lao, hawapo kwa ajli ya kutoa taarifa useful kwa jamii zaidi ya kufanya biahsara na kutumiwa na hao mafisadi walio ktk mchakato wa kujisafisha.

ndio maana me sishangai wao kuandika habari ambazo hazimsaidii mtu yoyote na zaidi hazibadilishi ukweli kuwa Nape anapiga vita ufisadi ndio maana CHUKUA CHAKO MAPEMA wanataka kumuondoka ktk chama chao ili asiwaharibie.

GO NAPE GO NAPE, hata nje ya ccm endelea kupiga vita ufisadi
 
Ndiyo kwanza wanampa martyrdom huyo Nape. Next kwa nini wasiandike kuhusu Miraji Kikwete?
 
...hawa watu mimi nilishaondoa katika list ya magazeti nchini namaanisha magaeti makini nchini, ndio maana huwa sijisumbua kusoma habari yoyote waliyoandika hata kama inaniihusu mimi au mtu wangu yoyote wa karibu kwani najua hazina ukweli...

Unaweza ku-share ni yapi hayo yaliyopo katika listi yako ya magazeti makini Tanzania? Naomba moja. Mawili itakuwa ziada na nitashukuru. Ahsante.
 
Unaweza ku-share ni yapi hayo yaliyopo katika listi yako ya magazeti makini Tanzania? Naomba moja. Mawili itakuwa ziada na nitashukuru. Ahsante.

Tafadhali na wewe share matokeo ya "investigation" yako kuhusu dokta Masau.....
 
hawa watu mimi nilishaondoa katika list ya magazeti nchini namaanisha magaeti makini nchini, ndio maana huwa sijisumbua kusoma habari yoyote waliyoandika hata kama inaniihusu mimi au mtu wangu yoyote wa karibu kwani najua hazina ukweli, wanatumiwa au wameamua kuandika tu ili wauze gazeti lao, hawapo kwa ajli ya kutoa taarifa useful kwa jamii zaidi ya kufanya biahsara na kutumiwa na hao mafisadi walio ktk mchakato wa kujisafisha.

Mkuu Heshima mbele, maneno yako ni mazito sana na ndio ukweli wenyewe, mimi ninamfahamu Nape, kwa karibu sana kwa sababu binamu yangu anaoa dada yake mmoja, na besides Marehemu Mnauye, briefly aliwahi kuwa C.O wangu JKT, kabla hajahamishiwa mako makuu,

Yeye alikuwa kwa dini ni Mu-Islam, alikuwa na wake zaidi ya mmoja legally, na akiwa hai hakukuwahi kuwa any problem, na alikuwa akizunguka kwenye nyumba zake kama ninavyowaona wa-Islam wengi, tena sio lazima kuwa ni viongozi hata wananchi wa kawaida hufanya hivyo,

Now Nape amezaliwa wakati Mnauye, akiwa hai na mkewe mkubwa alifahamu hilo halikuwa siri, na sio siri kwamba bado anao watoto wengine na wake zake wengine, lakini the minute alipofariki tu huyu mama mkubwa akaanza vita vikali kwa ajili ya nothing, kwa sababu Mnauye hakuwa na mali ya kumfanya mtu kupigia kelele kiasi hicho au kwa any of ndugu zake, unless kuna something ambacho hakijasemwa hapa hii habari ni mchezo mchafu tu wa siasa, ambao mafisadi ndicho wanachokijua kwa sababu hata madaraka waliyapata kwa njia hii hii ya kuwachafua kina Salim na Sumaye,

Nape hahitaji ku-worry au hata kujali haya maana ukiona maadui wako kisiasa wanakimbilia none hoja kama hizi, maana yake ni moja tu ni kwamba kwanza hawana uchafu wako kisiasa kwa sababu haupo, na pili umewashika pabaya na wako ukutani, hivi kweli mafisadi waliodai kushinda majuzi kwenye CC, kama kweli walishinda sasa what is this?

I mean to me this sounds like the politics of desparation, unless kuna something I am missing, otherwise Nape hapaswi hata ku-pay mind on this kwa sababu ni pure nonesense! Binafsi ningeshituka kama Nape angitwa fisadi, mwizi, au hana uwezo wa kazi kisiasa na kama wanamini kuwa Nape ana tatizo wangelsiema mapema sana kwa sababu now I am afraid kuwa it is too late, na wananchi wengi wamekwisha washitukia kuwa ni nothing but mafisadi, kama alivyosema Mwalimu ni wala rushwa na wananuka rushwa kila kona wanayopita ni rushwa tu inawafuata, sasa wanajaribu kukimbia vivuli vyao, lakini wapi rushwa mpaka wkenye majengo what a shame!

Nape asisikilize haya, kwa sababu lets say ni kweli, basi ajue kua hata Yesu hakuwa mtoto wa mume wa Maria, yaani Joseph, asimame imara na kusonga mbele kutafuta nafasi za uongozi maana zipo nyingi sana na kuna tunaomfagilia kwa sababu ya uchungu wa taifa letu!

Unajua mfa maji huwa haishi kutapa tapa!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
hauwezi kumpangia ridhiwan marafiki!!!!!hayo ni maisha yake binafsi na yeye ni mwanasiasa hakuna baya hapo,beno ni rafiki na kwa hili ni haki na heshima kumsapoti.Tatizo ni nini au na wewe ni mgombea ulitaka akusapoti akakutolea nje????usilete kushindwa kwako hapa,jipange sawasawa!
 
Nape: Nchi kwanza chama baadaye

Mwandishi Wetu Septemba 17, 2008
Tanzania Daima~Muungwana ni Vitendo

KATIKA kauli ambayo inaweza kuibua mjadala ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), Nape Moses Nnauye, amesema siasa ni utumishi kwa umma na katika hilo anaamini katika uzalendo kwa nchi kwanza kisha chama baadaye.

Akizungumza na Raia Mwema katika mahojiano maalumu, Nape ambaye pia ni mtumishi wa chama hicho amesema uzalendo wake unamsukuma kuamini kwamba chama kinaweza kupita lakini nchi ikabaki milele.

"Tunakuwa na nchi kwanza tunayotaka kuijenga, ndipo tunaunda chama cha kujenga nchi tunayoitaka, kwa hiyo uzalendo kwa nchi unapaswa kuvuka mipaka ya itikadi zetu," anasema.

Kauli hiyo ya Nape ambayo inaweza kuzua mtafaruku mwingine na chama chake, ameitoa huku akiwa katika msigano mkubwa na jumuiya ya vijana ya chama chake ya UVCCM kuhusiana na kauli yake ya kuukosa hadharani mradi wa jengo la umoja huo.

Katika mahojiano hayo ambayo yamechapishwa kwa kirefu ndani ya toleo la leo, Nape anasema suala la mradi wa jengo hilo lililopo eneo la Faya barabara ya Morogoro, Dar es Salaam halina uhusiano na uamuzi wake wa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM.

"Kimsingi kwanza kuna mambo mawili yanachanganywa na kuwa moja. Si sawasawa. Ugombea wangu wa Uenyekiti wa UVCCM na mradi wa ukarabati wa Makao Makuu havihusiani.

"Mradi ule nilivyosema na hata kama nitaendelea kusema ni katika kutimiza wajibu wangu kama mjumbe wa NEC na Baraza Kuu la UVCCM ninayewawakilisha Vijana, lakini pia kama kijana mzalendo wa CCM na Tanzania.

"Naamini matokeo ya vikao viwili vikubwa vya chama yaani, Kamati Kuu na NEC vimeweka wazi ukweli wa mambo wa kile nilichokuwa nikikilalamikia juu ya mkataba mzima na matokeo yake ni kamati ya kina Dk. Abdallah Kigoda, Pindi Chana na Andrew Chenge.

" Naamini wanaoendelea kusema juu ya hili na kutafsiri watakavyo baada ya taarifa rasmi kutolewa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi wana ajenda zao binafsi. Wito wangu kwao tuheshimu maamuzi ya vikao halali vya chama na kuacha kulumbana katika jambo moja, tunayo mengi ya kufanya," alisema.

Nape amezungumzia pia msimamo wake wakati wa mchakato wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2005 kwa kusema kwamba baada ya uteuzi makundi yalikwisha na yeye binafsi alisimama kidete kumpigia debe mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete.

"Msimamo wa chama ni kuwa katika uchaguzi kila mtu ana uhuru wa kuunga mkono mtu anayeamini anafaa kuliko mwingine, isipokuwa baada ya uteuzi wote tunakuwa kitu kimoja. Huu ni msimamo wa chama, hivyo sioni kosa la kuwa na chaguo fulani kabla ya uteuzi.

"Linakuwa kosa uteuzi ukiisha kupita watu wakaendelea na mambo yao kinyume na mteule wa chama. Ndiyo maana baada ya uteuzi ni mimi ndiye nilisimama kidete kwenye radio na hata mikoani kumtetea Kikwete kwamba ndiye chaguo la chama, hivyo anafaa kuwa Rais wa Tanzania," anasema.

Kuhusu uhusiano kati yake na Mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Emmanuel Nchimbi, Nape anasema kwamba hana ugomvi na kiongozi huyo bali wanatofautiana katika baadhi ya mambo tu.

Alisema hana ugomvi binafsi na Nchimbi, wala yeyote ndani ya CCM bali mara nyingi anapishana nao kimtazamo, hali ambayo anasema inachukuliwa kuwa ni msigano.

"Siyo kwamba pia Nchimbi kafanya yote mabaya, hapana, yapo mazuri machache, lakini naamini katika Umoja wa Vijana ambao unajua kuwa hatma ya nchi yao ipo mikononi mwao na kwamba wana wajibu wa kuamua kesho yao iweje na si kuamuliwa na mtu au kikundi cha wachache," alisema na kuongeza;

" Tukatae utaratibu unaoanza kujengeka wa kuviza akili na mawazo ya vijana wa Bara letu, athari za maamuzi yoyote waathirika wakubwa ni vijana na wanaathirika leo na kesho, so they have to be bold to stand for their rights (wanatakiwa kusimama kidete kutetea haki zao). Tujifunze kuacha unafiki, kisu kiitwe kisu, na uma uitwe uma, maana ukiwa mnafiki ujanani uzeeni utakuwa mchawi".
 
Mwanzo mzuri ila sijakuelewa maana una mengi ya kutuambia. Naogopa nisije nikakuamia ghafla ukatukimbia.

Please kama upo habari ndio hii. Good start and ongeza mwendo.
 
Kauli za Nape zinaonyesha ukomavu wa kisiasa in fact huyu ndio aliostahili kuwa naibu waziri wa ulinzi.Kwa kuonyesha kauli za mbusara katika maamuzi yake.
 
Namvulia kofia Nape kwa heshima.Tunahitaji vijana kama hawa ili tutoe taifa letu kutoka kwenye makucha ya mafisaidi hawa.Tusonge mbele Nape!
 
hauwezi kumpangia ridhiwan marafiki!!!!!hayo ni maisha yake binafsi na yeye ni mwanasiasa hakuna baya hapo,beno ni rafiki na kwa hili ni haki na heshima kumsapoti.Tatizo ni nini au na wewe ni mgombea ulitaka akusapoti akakutolea nje????usilete kushindwa kwako hapa,jipange sawasawa!

Cool Gal,

Karibu Jamii Forums.Umenikumbusha yale Maeno aliyoyasema Rostam kwa mtikila..kama sikosei alimwambia hastahili kujibishana na Mtikila,Yes you are like Mtikila na mie nakaa upande wa Rostam...!

sina nia ya kugombea uongozi wa CCM,Vijana wengi wanakimbilia Siasa baada ya kushindwa kupambana na maisha hapa mjini.Mie nilishayaweza Maisha hivyo niko another Level zaidi ya Benno.

Kitu kikubwa usichokijua ni kwamba,Mie namfahamu Benno vizuri sana na ni mmoja wa wadogo zangu ninawapa ushuri.

Kwa mawazo yako ni jambo gani niliongopa??Je Benno siyo ragiki wa Riz?Je hawakukaa chumba kimoja Walipokuwa Mlimani,ukiachilia mbali kusoma chuo kimoja.

Labda wewe ndiyo unamtaka beno??is up to you!

Gembe!
 
Anazungumzia nchi gani? Hii hii tanzania inayojengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno?
 
Huko upande wa pili kuna vita vipya kati ya Makamba na Komba, saafi sana sasa waseme ukweli wanachogombnia ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom