Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Nyambala.. alipokuwa Dodoma yeye alijitangazia tu nia yake hiyo kumbe hakuzungumza na wanasheria wake. Wanasheria wake walipopitia ushahidi wakamuambia next time utuambie mapema kabla ya kupiga watu mikwara.

Mwanakijiji hapa naona ulisahua kuwa "Hoja Hujibiwa kwa Hoja" hahaha
 
Du kweli EL sasa anatapatapa.........Na hii inatuthibitishia watanzania kwamba huyu ni mtu hatari sana no wonder bado kuna watu wanafikiria kumsafisha............ Well maybe asipochafuka atajifunzaje????????????? (OMO ad.)
 
Hivi akina Lowasa bado hawajajifunza tuu kuhusu ku-sign kitu? wanakuwa wamelewa mvinyo au na akili timamu? Yaani unawezaje kumuamini mtu na ku-sign kitu bila kusoma au kushirikisha mwanasheria? Lowasa jifunze (sio lazima uingie darasani) sio unakurupuka tuu na ku-sign vituu. Ukipewa uraisi si unaweza kuiuza nchi kwa ku-sign bila kusoma mikataba.!!
 
Sio kwamba hakuusoma mkataba. Anachokitaka Subhash kwa gharama yoyote EL tunayemfahamu kwa kuzisaka njuluku aache kusaini kweli?
 
Kikwete amliza Lowassa

• Asema mkataba hauna maslahi
• Aelekea kuunga mkono Nape
• Masilingi: Ni mkataba ‘ovyo'


Na Saed Kubenea

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete amesema mkataba wa mradi wa ujenzi wa kitegauchumi cha Umoja wa Vijana (UV-CCM), una dosari nyingi na haukubaliki kama ulivyo, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa za ikulu zinasema rais ameagiza utekelezaji wa mkataba usitishwe hadi dosari hizo zitakapoondolewa.


Katika mawasiliano rasmi na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, ya 3 Julai 2008, rais ameelekeza yafanyike mazungumzo baina ya Makamba, Mwenyekiti wa UV-CCM Emmanuel Nchimbi na Kaimu Katibu Mkuu Isack Francis kuweka msingi wa kurekebisha mkataba huo.


Hatua ya Kikwete inalenga kuzuia UV-CCM kutumbukia katika mgogoro wa kisheria na kuweka mbele "maslahi ya Umoja wa Vijana."


Rais amesema mkataba umebainika kuwa na mapungufu mengi ya kisheria ambayo lazima yarekebishwe "ili tusipoteze maslahi katika mradi huu."


Barua ya Kikwete kwenda kwa Makamba, ambayo gazeti limeona nakala yake, inahusu mkataba wa ukarabati/upanuzi wa Jengo la Umoja wa Vijana na ujenzi kwenye viwanja Na. 108/2 vilivyoko Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.


Mjumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Nape Nnauye alisema tarehe 22 Julai mwaka huu kwamba Baraza la Wadhamini la umoja wao, chini ya Edward Lowassa liliingiza UV-CCM katika mkataba unaonuka ufisadi na usio na manufaa kwa umoja huo.


Alisema baraza la Lowassa halikuwa na madaraka ya kufikia maamuzi hayo kwa sababu "Baraza Kuu la UV-CCM, lenye mamlaka ya uamuzi wa mwisho, lilikuwa halijaridhia mkataba huo."


Kwa mwezi mmoja sasa kumekuwepo kutupiana lawama kati ya wajumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM na Baraza la Wadhamini chini ya mwenyekiti wake Lowassa.


Wakati Baraza Kuu limesema halikuhusishwa katika suala la mkataba kati ya UV-CCM na mfanyabiashara Subhash Patel kwa ajili ya ujenzi wa mradi unaokadiriwa kufikia Sh. 40 bilioni, Makamba na Lowassa wamekuwa wakidai kuwa mkataba haujafikiwa wala kuwekwa saini.


Hata hivyo ujenzi unaendelea kwenye viwanja husika na tayari rais amesema mkataba hauna manufaa kwa umoja huo hadi utakapofanyiwa marekebisho.

Mara ya kwanza MwanaHALISI lilipoandika taarifa kuhusu mkataba wa UV-CCM, Lowassa alitishia kushitaki gazeti akisema "limezidi" kumzulia uwongo. Hajaenda mahakamani.

Dosari ambazo zimemstua rais ni pamoja na ile ya kukiuka Sheria ya Ardhi. UV-CCM wameridhia asilimia ya miliki ya ardhi (kiwanja) kuhamishiwa kwa wabia kabla shughuli yoyote ya ujenzi kuanza.


Utaratibu ni kwamba kabla hatua hiyo haijachukuliwa, sharti Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali atoe kibali kwa ajili ya uhamisho wa aina hiyo.


Yote haya yalifanyika bila kumfahamisha rais; bila kupitishwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM na bila kupelekwa na kubarikiwa na Baraza Kuu la UV-CCM.

Mkataba wa ujenzi wa mradi huo ulioenda kwa kichwa kisomekacho: "Development Agreement" ulisainiwa tarehe 2 Januari 2007 kati ya UV-CCM na makampuni mawili ya M.M. Integrated Steel Mills (MMISML) na Estim Construction Company Limited (ECCL).

Kasoro nyingine ambayo ilimstua rais ni uhamisho wa miliki ya ardhi kutokuwa na ukomo wa muda wa miliki. Mkataba unaacha eneo hilo kama kwamba uhamisho ni wa milele na milele.


Aidha, mkataba ambao rais ametilia mashaka na kukataa hadi utakaporekebishwa, hauonyeshi nafasi ya UV-CCM katika uendeshaji wa mradi pale ujenzi utakapokuwa umekamilika.


Lingine ambalo linaoenekana kuwa chanzo cha mitafaruku katika siku za usoni, ni uhusiano kati ya mbia mmoja – MMISML na mwingine, ambaye hakika ni mkandarasi wa ujenzi – ECCL.


Kinachostahili hapa ni kufafanuliwa kwa kina nafasi ya mbia na mkandarasi ili maslahi ya UV-CCM yasiingie kwenye mgogoro.


MwanaHALISI limesoma mkataba wa UV-CCM kwa makini na kugundua kuwa hauelezi kiasi cha uwekezaji kutoka kwa wabia ambacho kinaweza kutumika kueleza mgawo wa asilimia 25 ambazo inadaiwa UV-CCM watachukua.


Wataalam wa sheria wanasema ilibidi mkataba ueleze asilimia 25 ni sawa na eneo lipi la ardhi ya sasa au vitegauchumi vipya vinayotarajiwa kujengwa.


Mradi wa vijana, katika hali ambayo haiwezi kuelezeka kitaalam, hauna ufafanuzi wa matumizi na mapato hatua kwa hatua; jambo ambalo linaonyesha kutokuwa makini au kuashiria ghiliba katika mahusiano ya wabia.

Vilevile mkataba hauelezi iwapo ubia ni wa miliki ya pamoja au itaundwa kampuni tofauti ya kuendesha kitegauchumi.

Gazeti hili limeona barua ya Makamba ya 9 Julai 2008 inayopendekeza kikao kati yake na viongozi wa UV-CCM wiki moja mbele, lakini ujenzi bado unaendelea hadi sasa; takriban mwezi mmoja baada ya Rais Kikwete kuingilia kati.


Katika hatua nyingine, Mbunge wa Muleba Kusini Wilson Masilingi amekana kushiriki maamuzi yaliyoingiza UV-CCM katika mradi wenye utata.


Masilingi alikuwa akijibu swali kwa nini hakutoa ushauri kwa umoja huo wakati yeye ni mjumbe wa Baraza la Wadhamini. "Sikiliza bwana, mimi sijui lolote. Sikushirikishwa katika hilo. Niliposikia kelele zinaanza, nikamwona Lukuvi (William, Mkuu wa Mkoa Dodoma) na kutaka tukutane na kujadili," alisema Masilingi.


Alisema Lukuvi alimwambia kuwa yeye siyo mjumbe tena wa Baraza; "kwamba niliishatolewa na nafasi yangu amechukua Karamagi (Nazir, Mbunge Bukoba Vijijini)."


Hata hivyo Masilingi amesema kinachomsikitisha ni kuona waliomweka (Baraza Kuu la UV-CCM) siyo waliomwondoa na hivyo vijana wanamwona kama alishiriki kutoa maamuzi.


"Sina barua ya kuniondoa. Walioniondoa hawakunipa hata barua ya kunishukuru. Kinachoniuma ni vijana kufikiri kuwa hata mimi ni mmoja wa walioandaa mkataba wenye utata," alisema Masilingi.


Masilingi anasema alipokutana na Mwenyekiti wa UV-CCM Nchimbi, na kumuuliza mbona hakushirikishwa katika suala la mkataba huo, alimjibu kuwa anakwenda kuangalia kwenye orodha kama bado yupo, lakini akaongeza, "nadhani ulikwisha badilishwa."


Nchimbi alimkumbusha Masilingi kuwa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wanabadilishwa baada ya miaka mitano, "lakini nikashangaa, mbona wenzangu niliongia nao bado wamo?" alihoji Masilingi kwa kicheko.


Kuhusu mkataba wenyewe, Masilingi amesema, "Katika dunia sijawahi kuona mkataba ovyo kama huu, usiokubalika katika misingi yoyote ya maadili."


Masilingi anasema hati za kimila zinatambulika benki; itakuwaje hati rasmi za serikali za kiwanja kilichoko katikati ya jiji kama viwanja vya UV-CCM.


Anasema Umoja wa Vijana wangechukua hati yao; wakaenda benki kukopa; wakapata fedha na kumpa mkandarasi yeyote, hata Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwajengea na "siyo kuingia katika mkataba wa kijinga kama huu."


Masilingi, mmoja wa wanasheria wanaoaminika nchini, anasema ameona nakala ya mkataba na amejiridhisha kuwa kilichosainiwa na kuwezesha wabia kuanza ujenzi, ni mkataba halisi na si vinginevyo.


SOurce: MwanaHALISI
 
Ni kigezo kipi ambacho hutumika kuteua wajumbe wa baraza la udhamini la UVCCM? Mafisadi naona wanazidi kupangana kwenye nyadhifa zote muhimu ili wahakikishe kwamba wanalinda maslahi yao.

Ni sababu ipi iliwafanya wamtoe Masilingi na kumuweka Karamagi?

Unajua ukiangalia mambo yanavyokwenda ndipo unaweza kugundua kwamba ni kweli kabisa Lowassa, Rostam, Karamagi na wengineo wamejipanga ili kufanya kile wanachofikiria kukifanya.

Nitamshangaa sana JK iwapo ataendelea kuwaangalia wakijipanga kufanya wanayoyataka pasipo yeye kuchukua hatua yoyote. CCM imeishatekwa na mafisadi na hapa ndipo unapoweza kuona kila kona ya Jumuiya za Chama kuna wapambe wa mafisadi ama wao wenyewe wamejikita ili kuhakikisha mafisadi wanaendelea kulindana ndani ya chama.

Ni wakati muafaka kwa JK kutumia rungu lake la uenyekiti. Hata kama hao mafisadi walimsadia kuingia Ikulu lakini inatakiwa afike mahali aseme kwamba sasa inatosha na ni wakati wa kuwatosa.
 
Ni kigezo kipi ambacho hutumika kuteua wajumbe wa baraza la udhamini la UVCCM? Mafisadi naona wanazidi kupangana kwenye nyadhifa zote muhimu ili wahakikishe kwamba wanalinda maslahi yao.

Ni sababu ipi iliwafanya wamtoe Masilingi na kumuweka Karamagi?

Unajua ukiangalia mambo yanavyokwenda ndipo unaweza kugundua kwamba ni kweli kabisa Lowassa, Rostam, Karamagi na wengineo wamejipanga ili kufanya kile wanachofikiria kukifanya.

Nitamshangaa sana JK iwapo ataendelea kuwaangalia wakijipanga kufanya wanayoyataka pasipo yeye kuchukua hatua yoyote. CCM imeishatekwa na mafisadi na hapa ndipo unapoweza kuona kila kona ya Jumuiya za Chama kuna wapambe wa mafisadi ama wao wenyewe wamejikita ili kuhakikisha mafisadi wanaendelea kulindana ndani ya chama.

Ni wakati muafaka kwa JK kutumia rungu lake la uenyekiti. Hata kama hao mafisadi walimsadia kuingia Ikulu lakini inatakiwa afike mahali aseme kwamba sasa inatosha na ni wakati wa kuwatosa.

Nadhani upekuzi zaidi unahitajika usikute wajumbe wa bodi ya udhamini wana hisa ndani ya makampuni ya M.M. Integrated Steel Mills (MMISML) au Estim Construction Company Limited (ECCL), na kwa maana hiyo wanajihakikishia umiliki wa milele wa hiyo prime property.
 
Kwa hakika hali ni mbaya sana kwa CCM, lakini itategemea na JK atavyo handle hoja za uchaguzi wa jumuiya za chama.Nianze na hili la wajumbe kuchaguliwa vipi...WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI HUPENDEKEZWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI(MWENYEKITI WA UVCCM-NCHIMBI) NA KUPELEKA MAJINA KWA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA KWA UTHIBITISHO KAMA ULE WA PM KWA BUNGE..kilichofanyika kwa Masillingui aliingizwa kwa hoja kuwa bodi ya wadhamini kwa kuwa inahusika na mali za jumuiya iwe na mwanasheria lakini akawa mwiba kwa mafisadi kaondolewa kinyemela ndo akawekwa fisadi mwenzao Karamagi...

-----WAGOMBEA WANAENDELEA KUFANYIWA USAILI DODOMA MPAKA SASA LAKINI TAARIFA ZILIZOPO MAFISADI WAMEJIPANGA NA KUAPA KUMFUTILIA MBALI NAPE...Mfano Nchimbi amekaririwa akisema Nape akipita katwe uume wake awe mwanamke....tuungane kuwatokomeza mafisadi....
 
WAGOMBEA WANAENDELEA KUFANYIWA USAILI DODOMA MPAKA SASA LAKINI TAARIFA ZILIZOPO MAFISADI WAMEJIPANGA NA KUAPA KUMFUTILIA MBALI NAPE...

Wakuu mjifunze maana ya neno siasa, unafikiri Nape ni mjinga kiasi anaweza kwenda public na serious accusations kama zile bila ya kuwa na kinga? Unajuaje kuwa hakutumwa na Muungwana? Hivi Muuungwana mnajua vizuri au manabahatisha?

Mimi habari serious nilizo nazo kutoka ndani ni kwamba Nape asingpita bila ya kuamusha hii kasheshe, maana ilikuwa akatwe jina ndio maana akapewa hii hoja, ili kumnusuru, Nchimbi sio rais wa Tanzania na hana hizo nguvu mnazompa kichwa nazo, angekuwa Lowassa asingetoka u-Waziri Mkuu, na Lowassa mwenyewe angekuwa na hizo nguvu za kumtoa Nape, angezitumia kwanza kujinusuru asitoke kwenye u-Waziri Mkuu.



Mfano Nchimbi amekaririwa akisema Nape akipita katwe uume wake awe mwanamke....tuungane kuwatokomeza mafisadi....

Mbona huo uume haukukatwa aliponyimwa ukatibu mkuu wa CCM, aliokuwa ameuallia macho kila siku? Uwaziri alioahidiwa mbona hajapewa mpaka leo na bado anao huo uuume? Unafikiri Nape ni Amina? Mshauri rafiki yako kuwa this time akicheza anaondoka yeye maji ya shingo hayo anayojaribu kuyaoga bila ya kuyajua!
 
Kwa hakika hali ni mbaya sana kwa CCM, lakini itategemea na JK atavyo handle hoja za uchaguzi wa jumuiya za chama.Nianze na hili la wajumbe kuchaguliwa vipi...WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI HUPENDEKEZWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI(MWENYEKITI WA UVCCM-NCHIMBI) NA KUPELEKA MAJINA KWA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA KWA UTHIBITISHO KAMA ULE WA PM KWA BUNGE..kilichofanyika kwa Masillingui aliingizwa kwa hoja kuwa bodi ya wadhamini kwa kuwa inahusika na mali za jumuiya iwe na mwanasheria lakini akawa mwiba kwa mafisadi kaondolewa kinyemela ndo akawekwa fisadi mwenzao Karamagi...

-----WAGOMBEA WANAENDELEA KUFANYIWA USAILI DODOMA MPAKA SASA LAKINI TAARIFA ZILIZOPO MAFISADI WAMEJIPANGA NA KUAPA KUMFUTILIA MBALI NAPE...Mfano Nchimbi amekaririwa akisema Nape akipita katwe uume wake awe mwanamke....tuungane kuwatokomeza mafisadi....

Haya uliyomkariri Nchimbi siyo maneno yake wala siyo kauli zake ata siku moja.Nchimbi hawezi kuongeamaneno ya uume ata mara moja...Hayo ni maneno ya wapambe wanaodanganya...Ata hivyo Nape kamwe hawezi kupita kta mchakato huo kwa kuwa mambo yanayoihusu kanuni hayawezi kupindwa ata siku moja....kama kupendwa alipendwa Reagan lakini muda ulipofika aliondoka na pia Nape hawezi kupindiwa katiba ya uvccm kwa ajili yake.

He must GOOOOOOOOO
 
Wewe kibaraka mwaminifu wa JMS,nani alikwambia Nchimbi alitaka kuwa Katibu Mkuu wa Chama?unajitungia tu habari mkishakaa na mama kilango jikoni.mama kilango tunajua kisaokolojia hayuko ok toka alipotendwa na wale majambazi morogoro....ni kawaida mwanamke akitendwa bila ridhaa yake huwa anaumizwa sana kisaikolojia na wengine huwa mpaka wanakufa.

Haya maneno ni too low kwangu, mkuu I am too big for this na yana maana moja tu nayo ni kwamba huna hoja,

Tabia yangu siku zote ni kusimamia ukweli bila kujali nani anahusika, na huwa siogopi mtu wala maneno ya chooni, majibu yako haya ni clear kuwa ujumbe umefika, saaafi sana, hayo matusi yako nafikiri sheria za JF ziko very clear,

Lakini pole sana ndugu yangu nilifkiri baada ya yaliyokukuta majuzi umejifunza kumbe bado tu! Mbona Nchimbi hakuja kukusaidia? Na huwa nina dharau sana na watu wanabadilika rangi wanapozidiwa hoja!
 
1.
Originally Posted by ACHEBE
Kwa hakika hali ni mbaya sana kwa CCM, lakini itategemea na JK atavyo handle hoja za uchaguzi wa jumuiya za chama.Nianze na hili la wajumbe kuchaguliwa vipi...WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI HUPENDEKEZWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI(MWENYEKITI WA UVCCM-NCHIMBI) NA KUPELEKA MAJINA KWA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA KWA UTHIBITISHO KAMA ULE WA PM KWA BUNGE..kilichofanyika kwa Masillingui aliingizwa kwa hoja kuwa bodi ya wadhamini kwa kuwa inahusika na mali za jumuiya iwe na mwanasheria lakini akawa mwiba kwa mafisadi kaondolewa kinyemela ndo akawekwa fisadi mwenzao Karamagi...
-----WAGOMBEA WANAENDELEA KUFANYIWA USAILI DODOMA MPAKA SASA LAKINI TAARIFA ZILIZOPO MAFISADI WAMEJIPANGA NA KUAPA KUMFUTILIA MBALI NAPE...Mfano Nchimbi amekaririwa akisema Nape akipita katwe uume wake awe mwanamke....tuungane kuwatokomeza mafisadi....

2.
Haya uliomkariri Nchimbi siyo maneno yake wala siyo kauli zake ata siku moja.Nchimbi hawezi kuongeamaneno ya uume ata mara moja...Hayo ni maneno ya wapambe wanaodanganya...Ata hivyo Nape kamwe hawezi kupita kta mchakato huo kwa kuwa mambo yanayoihusu kanuni hayawezi kupindwa ata siku moja....kama kupendwa alipendwa Reagan lakini muda ulipofika aliondoka na pia Nape hawezi kupindiwa katiba ya uvccm kwa ajili yake.He must GOOOOOOOOO

Inahuzunisha sana mtu mzima anpojifanya mtoto mdogo kwa sababu tu hakuna anayemuona nyuma ya Computer, this is childsh! No wonder!
 
beno malisa na ridhiwani ni marafiki wa karibu na walisoma darasa moja pale UDSM sheria ni vigumu kutenganisha hawa watu maana urafiki wao ulikuwa hata kabla ya haya mambo ya siasa.
 
Nape Nnauye atoswa kinyang'anyiro cha uongozi Vijana wa CCM

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi
Date::8/19/2008

SAFARI ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), Nape Nnauye kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa, imeishia njiani baada ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM kumpa alama E inayoonyesha kwamba hafai kugombea nafasi hiyo.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa, kikao cha Kamati ya Utekelezaji cha Agosti 16 na 17 mwaka huu mjini Dodoma kimemuengua Nnauye katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo na kupendekeza majina ya watu watano kuwania nafasi hiyo.

Majina yaliyopendekezwa ni Zainab Kawawa, Said Mtanda, Benno Malisa, Hussein Bashe na Suleiman Suleiman.

Kwa mujibu wa habari hizo, Nnauye amewekewa alama ya kutofaa kugombea nafasi hiyo kutokana na kigezo cha umri, ingawa kuliibuka mjadala mzito ndani ya kikao hicho kabla ya kufikia maamuzi hayo.

Mjadala uliibuka na kuwagawa wajumbe katika makundi mawili yanayopinga na kukubali uamuzi huo, lakini kundi lililopinga lilionekana kuwa dhaifu kutokana na idadi yao kuwa ndogo.

"Haikuwa rahisi kufikia maamuzi hayo, kwani kamati iligawanyika katika makundi ya wajumbe kutoka Zanzibar na wale wa Bara. Zanzibar waligoma, lakini walishindwa kutetea uamuzi wao kutokana na idadi yao kuwa ndogo na hoja zao kuonyesha kwamba zinataka kuvunja kanuni ambao walijiwekea," kilisema chanzo cha habari.

Awali, imedaiwa kuwa kabla ya kuanza kikao hicho, Mwenyekiti wake, Dk Emmanuel Nchimbi aliwatahadharisha wajumbe kuwa kikao kingekuja na maamuzi ya kihistoria ya ama wajumbe kuondoka wakiwa wameungana ama kugawanyika kama wangevunja kanuni na kujali zaidi watu.

Sababu zilizotolewa na upande uliounga mkono kuondolewa kwa Nape ni kutetea maamuzi ya vikao vyake vilivyopitisha kanuni ya kikomo cha umri katika uwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Nape aliliambia gazeti hili jana kuwa Kamati ya Utekelezaji ya UVCMM haina mamlaka kisheria kukata jina la mgombea na kufafanua kuwa mamlaka ya maamuzi hayo yako katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

"Vikao vya chini havina mamlaka kukata jina la mgombea, wanachofanya ni kujadili na kuweka alama na mimi waliniwekea alama mbaya ya E ikimaanisha kwamba sifai. Hata hivyo, kikao chenye mamlaka ya kukata jina na Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete," alisema.

Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM imefikia hatua hiyo baada ya kupitia vyeti halisi vya kuzaliwa vya wagombea hao na kubaini kuwa, Nape alizaliwa mwaka 1977.

Sambamba na kupitia vyeti hivyo, wagombea wote walihojiwa mmoja baada ya mwingine na kutakiwa kuwasilisha kadi ya uanachama na nyaraka zingine za kuthibitisha maelezo waliozaja kwenye fomu za maombi, ikiwa ni pamoja na vyeti halisi vya kuhitimu darasa la saba.

Kamati ya Utekelezaji ni kikao cha pili kujadili majina ya wagombea hao. Kikao cha kwanza ni Sekretarieti ya UVCCM iliyokaa jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Mtinga, ambako pia habari zinadai kuwa alipewa alama za chini.

Kwa mujibu wa kanuni za CCM katika uchaguzi huo, Kikao cha Kaamati ya Utekelezaji kitafuatiwa na Baraza Kuu la UVCCM kabla ya mkutano wa Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu wake Mkuu, Yusuf Makamba.

Vikao vingine katika mchakato huo ni Kamati ya Maadili ya CCM na Kamati Kuu (CC) ambavyo vitakaa Agosti 20 na 21 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Vikao hivyo vitapitia maamuzi ya vikao vilivyopita na kutoa ushauri wake kwa Halmashauri Kuu (NEC), itakayokaa Septemba 2 na 3 mwaka huu kuchambua na kutangaza majina ya wagombea walioteuliwa.

Zengwe la umri ni kanuni iliyoingizwa kwenye taratibu za Uchaguzi wa UVCCM mwaka 2003 wakati Mwenyekiti wa sasa, Dk Emmanuel Nchimbi anawania nafasi hiyo kwa mara ya pili, ikilenga kumuengua, lakini busara ya Kamati Kuu ya CCM iliiweka pembeni kwa muda.

Kulingana na kanuni hiyo umri wa mwisho wa kugombea ni miaka 30 ili kiongozi husika asizidi miaka 35 akiwa madarakani umri ambao ni wa mwisho wa uanachma wa UVCCM.

Zengwe la umri safari hii linalekea kuwalenga baadhi ya wagombea machachari katika Uchaguzi wa UVCCM, ambao ni pamoja na Nape Nnauye.

Habari za ukahakika zanasema kwamba, baada ya hoja ya umri wa miaka 30 kuahirishwa mwaka 2003, kabla ya kutumika ilipaswa kwanza kupata baraka za vikao vya UVCCM kuanzia kwenye sekretariati, Kamati ya Utekelezaji na mwishowe kwenye Baraza Kuu. Hatua hizi hazikufuatwa ila ni NEC iliagiza tu kuanza kutumika.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa UVCCM ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo, Francis Isaac, aliambia Mwananchi hivi karibuni kwamba, kanuni ya umri ilipitishwa na Kamati Kuu ya CCM miaka mitano ilyopita.

Isaac alisema kuwa, haikuweza kutumika katika Uchaguzi wa UVCCM uliopita kwa sababu wakati uamuzi unapitishwa wa kanuni hiyo tayari uchaguzi ngazi ya wilaya ulikwisha kufanyika na hivyo kuamuliwa ianze kutumika katika uchaguzi huu.

Isaac pia alisema kwamba mchakato wa kutungwa kwa kanuni hiyo ulifuata taratibu zote kuanzia kwenye sekretariati, Baraza Kuu, Kamati Kuu ya CCM, NEC na baadaye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika miaka mitano iliyopita.

Nape aliyezaliwa Novemba 26, 1977, aliwasha moto ndani ya chama hicho siku amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, baada ya kulipua bomu kwamba, mkataba wa kujenga jengo jipya la UVCCM umegubikwa na ufisadi.
 
Hata hivyo, Nape aliliambia gazeti hili jana kuwa Kamati ya Utekelezaji ya UVCMM haina mamlaka kisheria kukata jina la mgombea na kufafanua kuwa mamlaka ya maamuzi hayo yako katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

“Vikao vya chini havina mamlaka kukata jina la mgombea, wanachofanya ni kujadili na kuweka alama na mimi waliniwekea alama mbaya ya E ikimaanisha kwamba sifai. Hata hivyo, kikao chenye mamlaka ya kukata jina na Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete,” alisema.

Nilijua tu kichwa cha hii habari hkiko sawa maana hapo kuna mkono wa kiongozi flani kwenye hii habari, yaani hawa waliotuletea mtandao bado wanajaribu tena kutuletea magoi goi wenzao wengine tena badala ya kukaa pembeni na kukubali kuwa hawana uwezo wa kuongoza, kwa hiyo hata wa kutuchagulia viongozi!

Cha ajabu kuna mamluki wenzetu wanaowanuga mkono, kweli ni aibu kubwa sana!
 
Mkuu

Zengwe lilishaanza hilo. Chama chetu ndivyo kilivyo. Kama uchaguzi ulipita walifumba macho kwa nini sasa wamemtolea macho yeye?
 
Mkuu

Zengwe lilishaanza hilo. Chama chetu ndivyo kilivyo. Kama uchaguzi ulipita walifumba macho kwa nini sasa wamemtolea macho yeye?

Chama cha mafisadi hicho!! Ukionyesha kuuvalia njuga ufisadi wanaoufanya kupitia mgongo wa CCM basi lazima wafanye kila njia wakutose. Halafu wanajidai kushangaa wanapoitwa Chama Cha Mafisadi. Watu kama Nape hawatakiwi kabisa ndani ya CCM.
 
Nnauye alifanya kosa la kukemea ufisadi ndani ya CCM akiwa nje ya madaraka; alitakiwa aende "kimya" kama yule simba wa kwenye methali....
 
Kikwete akitaka kuandaa njia yake kwa namna moja ahakikishe Nape anpew uenyekiti wa UVCCM watu wanataka cheche! Cheche za Fikra mpya!
 
Back
Top Bottom