Sakata la moto Karume, busara ichukue mkondo wake

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Migogoro isiyo na tija katika jamii yeyote iliyo staraabika husababisha ghasia na machafuko yasiyo na tija kwa taifa.

Mwanafalsafa Chuck Palahniuk aliwahi kusema "There are only patterns, patterns on top of patterns, patterns that affect other patterns. Patterns hidden by patterns. Patterns within patterns.

If you watch close, history does nothing but repeat itself. What we call chaos is just patterns we haven't recognized. What we call random is just patterns we can't decipher. what we can't understand we call nonsense. What we can't read we call gibberish.
There is no free will. There are no variables.

Akiaminisha dunia kuwa kuna mifumo tu, mifumo juu ya mifumo, mifumo inayoathiri mifumo mingine. Sampuli zilizofichwa na mifumo. Sampuli ndani ya mifumo.

Ukitazama kwa makini, historia haifanyi chochote ila kujirudia yenyewe. Tunachoita fujo ni mifumo tu ambayo hatujaitambua. tunachokiita nasibu ni mifumo tu hatuwezi kuifafanua. tusichoweza kuelewa tunaita upuuzi. Kile ambacho hatuwezi kusoma tunaita gibberish.

Hakuna hiari.

Hakuna vigezo.

Sakata la MCHIKICHINI lisichukuliwe jepesi kwa kuwa tu mifumo ndani ya watengeneza mifumo hawaamini katika mifumo inayoathiri mifumo mingine.

Imekuwa desturi kila inapotokea sakata la kuhamisha machinga biashara zao huchomwa Moto,kwa maana ya soko wanalo tegemea kukuza ajira na uchumi wa mmoja mbali na Taifa kwa maana ya tozo mbalimbali kwa uwekezaji huo.

Hali imezua taharuki na kusababisha ghasia zinazo pelekea nguvu kubwa ya serikali kuzuia hasira za wahanga hao.

Haya yote Yana kwenda sanjari na kauli ya naibu waziri wa kazi maendeleo ya vijana na ajira kubeza juhudi za vijana kusaka ajira ilihali serikali anayo hudumu imeshindwa kulinda rasilimali za machinga hao.

Mabenki si rafiki wa maskini japokuwa mikopo yao ni fursa ya kukuza uchumi, lakini kufikia kukuza kupata mikopo hiyo katika kuinua vipato vyao hawakwenda benki wakiwa wamejifunika shuka,waliweka dhamana zao,lakini bila kufikiri hili kwa umakini mna Leta siasa kwenye maisha ya watu.

Chuck anatufundisha kuwa historia haifanyi chochote zaidi ya kutukumbusha yaliyopita. Machafuko makubwa duniani husababishwa na mifumo inayoharibu miundo mbinu ya utafutaji riziki. Yamefanyika Tunisia na matokeo yake ni anguko la serikali. Kufikia huko ni mchakato na mchakato huo mnautengeneza wenyewe serikali bila kuzingatia usalama wa raia na Mali zake.

Kejeli za viongozi wasio na vision kwa Taifa sambamba na matukio hayo yanaifanya jamii iliyo athirika kupoteza Imani na serikali yao, Rais simama toa neno machinga wa mchikichini wapate pumbazo la moyo.
 
Sina chuki na wamachinga japo kinachotokea ni matokeo ya matatizo yaliyo tengenezwa na wanasiasa.

kama bomu la kutegwa ardhini linavyo weza kuwa hatari kwa aliyelitega vivyo hivyo kwa wamachinga wanavyotumika na wanasiasa.

Kulikua na vilio vya wafanyakazi, wafanyabiashara na sekta binafsi kipindi cha nyuma wakati huo wamachinga walikua wakikenua meno na kuchekelea, hawakujua wala kufikiri kuwa ipo siku na wao wanaweza wakaonewa kama makundi mengine.

Ni wakati wa wote kuwa kitu kimoja sasa kukemea na kupinga ukandamizaji pia tujifunze mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
 
Exactly,kinacho fanyika ni kuwatumia kama ngazi ya kupandia,wakishafanikiwa malengo yao ngazi inaondolewa,can imagine what a gap will be there!! Ni suffering, kwa hiyo tusimame kuionya serikali kuwa jukumu la ustawi wa wananchi ndiyo msingi mkuu wa serikali
 
Back
Top Bottom