Sakata la Morrison: Yanga yaishtaki Simba TFF na kutaka haki itendeke

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,519
9,322
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umepeleka rasmi malalamiko Shirikisho la Soka nchini (TFF) dhidi ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam pia ikidai inamshawishi winga wake, Bernard Morrison, kujiunga na klabu hiyo kinyume cha sheria na ikitaka haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

“Mchezaji wetu ameeleza kila kitu, hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitayasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kuutolea maamuzi,” amesema Patrick na kuongeza kwamba tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Source:Yanga App.
 
Utopolo mnahangaika sana dah, Bernard ni mali yenu hadi milele ? Mkataba sio msaafu useme hauvunjwi

Amekuja kutafuta pesa bongo sio kupewa sifa na utopolo fc
 
Kwani huko utopoloni BM33 ashaingia kambini au bado yuko mafichoni kwenye ile hotel ya nyota 6
 
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umepeleka rasmi malalamiko Shirikisho la Soka nchini (TFF) dhidi ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam pia ikidai inamshawishi winga wake, Bernard Morrison, kujiunga na klabu hiyo kinyume cha sheria na ikitaka haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

“Mchezaji wetu ameeleza kila kitu, hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitayasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kuutolea maamuzi,” amesema Patrick na kuongeza kwamba tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Source:Yanga App.
Sijaona kama kuna umuhimu hapo, wanataka kumzibia riziki huyoo morrison hao utopolo fc....
 
Walipe madeni baada ya Zahera, Pondamali na Chirwa kujitokeza kudai pesa zao Hamisi Tambwe naye kajitokeza kudai pesa zake
 
Jamaa anawarusha roho tu ili wampandishie dau,hivi kwa bata wanayokula wachezaji wa Simba ,hela wanazolipwa jamaa asitamani kuingia yanga
Kwani huko utopoloni BM33 ashaingia kambini au bado yuko mafichoni kwenye ile hotel ya nyota 6
 
Pamoja fedha walizonazo Simba kama kweli , wanatakiwa kufuata taratibu za kusajili mchezaji kutoka Club nyingine bila kutumia ubabe. Kama wanamtaka Morrison, waende mlango wa mbele kwa uongozi wa Club ya Young Africans Sport Club wavunje Mkataba. Kama kweli Simba Sports Club wamefanya mazungumzo na Morrison nje ya utaratibu hilo ni kosa na hategemei Club inayendeshwa kwa uekedi kama Simba kufanya. Hivyo kama ni kweli Simba waombe msamaha. Sheria haibagui kwa tajiri au fukara.
 
Simba haindeshwi kiuweledi kama inavotajwa, wahuni tu.
 
Vilabu hivi kuitwa KULWA NA DOTTO basi majina hayo yamekuwa yakisadifu vitendo vyao .

Kulwa alitamka kutaka kumsajili CHAMA , daaaah wawakilishi wa Dotto povu la kiwango cha dry cleaner lilionekana kwa sifa na majigambo ya ueledi katika uendeshaji klabu yao.

Kulwa naye kakurupuka baada ya Dotto kuhisiwa kufanya mazungumzo kinyemela ya kutaka kumsajili kata ngebe wao MORRISSON, hawa wameonesha kutumia njia za kisheria na kiutawala zaidi ( HAWAHUKUMU)

Mashabiki sasa ndo povuuuuu, huku mtoa povuuuuuu mkuuu yupo kimyaaa kama hayupo.

Radio zetu zinazochagiza mapovu kama hazipo vile, wakati sasa walitakiwa wakati wanasubiri maamuzi ya kisheria toka TFF wao wangekuja na taarifa za kiuchunguzi lkn wamekalia mawazo yao na fikra zao zitoe majibu.
 
Mbumbumbu lile tukio la tarehe 8 march bado linawasubua sana
Morrison.jpg
 
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umepeleka rasmi malalamiko Shirikisho la Soka nchini (TFF) dhidi ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam pia ikidai inamshawishi winga wake, Bernard Morrison, kujiunga na klabu hiyo kinyume cha sheria na ikitaka haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

“Mchezaji wetu ameeleza kila kitu, hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitayasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kuutolea maamuzi,” amesema Patrick na kuongeza kwamba tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Source:Yanga App.
[/QUOTE

Paka haishi kwenye nyumba ya bachela.
 
Back
Top Bottom