Ushauri kwa Yanga: Kateni rufaa FIFA kupinga kona ya Simba kwenye mechi yao na Singida FC

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Kumekuwa na vijimaneno vingi juu ya Ushindi wa Simba dhidi ya Singida jana kwenye Uwanja wa Aman katika Mchezo wa Nusu fainali.

Malalamiko haya yamekuja baada ya Simba kupata Kona iliyozaa Goli. Wadau wakubwa wa malalamiko haya ni mashabiki wa Yanga wenye Hasira na Chuki baada ya Klabu yao kufungwa na APR na kutolewa.

Najiuliza, kama SIMBA wasingefunga lile goli kwa kupata ile kona wangeendelea kudai ile kona sio halali?

Yanga kubalini Matokeo kuwa mlitolewa na APR. Wao Singida FC wapo kimya kwani ukweli wa ile kona wanaujua kwa Mchezaji wao kuguswa na ile krosi iliyozaa kona.

Kwa kuwa Yanga hamjaridhika na Uamuzi wa Refa juu ya ile kona basi kateni rufaa FIFA kupinga kona iliyozaa goli.

Nichukue nafasi hii kuwatakia Ushindi mkubwa katika Mchezo wao wa Fainali.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
mashindano haya hayapo popote. ni kama chandimu 😂😂. mimi mapema sana ningeandika barua na jina la referee fifa. tff and zff ni kama vichaa.
 
Kumekuwa na Vijimaneno vingi juu ya Ushindi wa SIMBA vs SINGIDA jana kwenye Uwanja wa Aman ktk Mchezo wa Nusu fainal.Malalamiko haya yamekuja baada ya Simba kupata Kona iliyozaa GOLI.WADAU wakubwa wa Malalamiko haya ni MASHABIKI wa YANGA wenye Hasira na Chuki baada ya Klabu yao kufungwa na APR na kutolewa.Najiuliza Kama SIMBA wasingefunga lile GOLI kwa kupata ile KONA je Wangeendelea kudai ile KONA sio Halali?YANGA kubalini Matokeo kuwa mlitolewa na APR.Wao SINGIDA FC wapo kimya kwani ukweli wa ile kona wanaujua kwa Mchezaji wao kuguswa na ile KROSI iliyozaa Kona .Kwa kuwa YANGA hamjaridhika na Uamuzi wa Refa juu ya ile KONA basi KATENI RUFAA FIFA kupiga KONA iliyozaa GOLI.
Nichukue nafasi hii kuwatakia USHINDI MKUBWA SIMBA ktk Mchezo wao wa FAINAL

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Mambo yako hivi hadi sasa, mbivu na mbichi itakuja kujuikana mwisho wa msimu.
IMG_20240111_234100.jpg
 
Back
Top Bottom