Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Mhe Mnyika, Tundu Lissu, Mdee, Zitto na wengine mlio machachari; changamoto ndio hiyo hapo - mdau Ndugu SISI KWA SISI ndio hivo kakereka mwisho-wa-reli Kigoma.
Mkuu unaonekana hujui siasa,hujui kufanya analysis,kwa namna yoyote ile ni ngumu kuuliza swala la madaktari kwasasa kwasababu limekwisha tolewa ufafanuzi juzi na jana...na jana waziri Lukuvi amesema kuwa kauli ya serikali uwa haiwekwi kwenye ratiba kulingana na taratibu za Bunge..kwa hiyo wanasubiri Spika hawape nafasi watoe kauli yao.Sasa kwa upepo huu ni ngumu sana kuanza kuingiza hoja hii,unaweza ukaonekana ni mtu usiyejua utaratibu,haupo makini nk...kwa hiyo mie naunga mkono wabunge wa CDM kukaa kimya kwasasa mpaka watakapo pata kauli ya serikali inayotakiwa kutolewa.
Lowassa anatumiwa na CHADEMA
Acha kukata tamaa, rudi kazini kama umeishiwa.Tulisoma tamko la CHADEMA kuhusu kuwaunga Mkono madkatari nchini. wengi tuliamini Mnyika leo angalipanga timu yake kabambe kumbana waziri Mkuu kuhusu mgomo huu. kitendo cha Mnyika kutopanga timu yake bungeni na kumbana waziri mkuu ni wazi mnyika ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine wasiojali maslahi ya watanzania.
Leo madaktari wote waliamini Chadema na makamanda wengine watapata mdomo kupitia Mh Mnyika kama Mbunge na msemaji wa chadema hasa baada article nzuri aliotoa kupitia Vyombo vya habari.
Mnyika yupo bizz na Hoja ya Richmond ambayo anaamini haitaleta tija kwa wananchi. hii italeta tija zaidi na mbio za urais wa CCM na sio madokta na wagonjwa.
Kama Chadema ni wazuri wa kuandika, lkn kivitendo kwa madokta ni kiini macho
Acha kukata tamaa, rudi kazini kama umeishiwa.
Embu soma sheria na kanuni za bunge kwanza kabla yakutoa thread inayohusu bunge.
Mkulu Chadema swala la madaktari walikuwa wa kwanza kukutana na waandishi wa habari na kulitolea tamko. Suala la Richmond lina tija kumbuka Owner alikuwa analipwa 152,000,000/= kila siku hizo ela zingepatikana sidhani kama madaktari wangegoma kwa sababu chakuwapa kingekuwepo. Hivyo swala la Richmond lina tija, mbunge wangu Mnyika endelea na mapambano achana na vichaa wanaoingilia mtandao wetu wa JF. Peoples Power hakuna kulala mpaka kieleweke.
Ukatibu mwenez ulimfaa tindu lissu au lema as mnyika yupo too cold,yeye inamfaa kazi ya naibu katibu!
Kinachoonekana hapa ni kuchonganisha madaktari na CHADEMA.mnyika ndo waziri wako wa afya?
acha unafiki,leo lisu na lema wamekuwa wazuri?ka hadithi ka sungura
Madokta walitaka wasipatiwe msaada wa kisiasa. chadema imeheshimu uamuzi huo.