Sakata la mgomo wa madaktari : Mnyika jiuzulu upesi umetuaibisha na kutufedhesha

sisi kwa sisi

Senior Member
Feb 1, 2012
119
2
Tulisoma tamko la CHADEMA kuhusu kuwaunga Mkono madkatari nchini. wengi tuliamini Mnyika leo angalipanga timu yake kabambe kumbana waziri Mkuu kuhusu mgomo huu. kitendo cha Mnyika kutopanga timu yake bungeni na kumbana waziri mkuu ni wazi mnyika ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine wasiojali maslahi ya watanzania.

Leo madaktari wote waliamini Chadema na makamanda wengine watapata mdomo kupitia Mh Mnyika kama Mbunge na msemaji wa chadema hasa baada article nzuri aliotoa kupitia Vyombo vya habari.
Mnyika yupo bizz na Hoja ya Richmond ambayo anaamini haitaleta tija kwa wananchi. hii italeta tija zaidi na mbio za urais wa CCM na sio madokta na wagonjwa.

Kama Chadema ni wazuri wa kuandika, lkn kivitendo kwa madokta ni kiini macho
 
Mbona sijaelewa? Nilivyosoma heading nilidhani Mnyika kawasaliti ma dr wa tz kwa namna fulani bungeni.
Ghoosh!!
 
Mmetumwa nyie na magamba,nchi imewashindwa mnabaki eti watu baki wajiuzuru,mwambieni Vuvuzela lenu Nape na Pinda wajiuzuru mana wanatoa kaulu tofauti wakati wapo katika serikali moja na chama kimoja cha majambazi CCM! Au kamwambiye mama yako na baba yako wajiuzuru kukutambua wewe kama mtoto wao! Filauni mkubwa wewe.
 
Mkuu unaonekana hujui siasa,hujui kufanya analysis,kwa namna yoyote ile ni ngumu kuuliza swala la madaktari kwasasa kwasababu limekwisha tolewa ufafanuzi juzi na jana...na jana waziri Lukuvi amesema kuwa kauli ya serikali uwa haiwekwi kwenye ratiba kulingana na taratibu za Bunge..kwa hiyo wanasubiri Spika hawape nafasi watoe kauli yao.Sasa kwa upepo huu ni ngumu sana kuanza kuingiza hoja hii,unaweza ukaonekana ni mtu usiyejua utaratibu,haupo makini nk...kwa hiyo mie naunga mkono wabunge wa CDM kukaa kimya kwasasa mpaka watakapo pata kauli ya serikali inayotakiwa kutolewa.
 
mkuu unaonekana hujui siasa,hujui kufanya analysis,kwa namna yoyote ile ni ngumu kuuliza swala la madaktari kwasasa kwasababu limekwisha tolewa ufafanuzi juzi na jana...na jana waziri lukuvi amesema kuwa kauli ya serikali uwa haiwekwi kwenye ratiba kulingana na taratibu za bunge..kwa hiyo wanasubiri spika hawape nafasi watoe kauli yao.sasa kwa upepo huu ni ngumu sana kuanza kuingiza hoja hii,unaweza ukaonekana ni mtu usiyejua utaratibu,haupo makini nk...kwa hiyo mie naunga mkono wabunge wa cdm kukaa kimya kwasasa mpaka watakapo pata kauli ya serikali inayotakiwa kutolewa.

la arusha lilitolewa ufafanuzi na kila kiongozi. Lkn kwa kuwa linamanafuaa ya kisiasa uliona bungeni kila anaepata muda wa chadema humbana waziri mkuu
 
Tulisoma tamko la Chadema kuhusu kuwaunga Mkono madkatari nchini. wengi tuliamini Mnyika leo angalipanga timu yake kabambe kumbana waziri Mkuu kuhusu mgomo huu. kitendo cha Mnyika kutopanga timu yake bungeni na kumbana waziri mkuu ni wazi mnyika ni mawnasiasa kama wanasiasa wengine wasiojali maslahi ya watz.
Leo madaktari wote waliamini Chadema na makamanda wengine watapata mdomo kupitia Mh Mnyika kama Mbunge na msemaji wa chadema hasa baada article nzuri aliotoa kupitia Vyombo vya habari.
Mnyika yupo bizz na Hoja ya Richmond ambayo anaamini haitaleta tija kwa wananchi. hii italeta tija zaidi na mbio za urais wa CCM na sio madokta na wagonjwa.
Kama Chadema ni wazuri wa kuandika, lkn kivitendo kwa madokta ni kiini macho

Unaonyesha wazi kuwa haufahamu hata ABC za bunge, ni dhahiri kwa kuwa Serikali imesha toa ahadi ya kutoa taarifa bungeni juu ya mgomo huo swali lolote kuhusu suala hilo lisingekubaliwa na spika huko ndio kujua kanuni kaka.
 
Mkulu Chadema swala la madaktari walikuwa wa kwanza kukutana na waandishi wa habari na kulitolea tamko. Suala la Richmond lina tija kumbuka Owner alikuwa analipwa 152,000,000/= kila siku hizo ela zingepatikana sidhani kama madaktari wangegoma kwa sababu chakuwapa kingekuwepo. Hivyo swala la Richmond lina tija, mbunge wangu Mnyika endelea na mapambano achana na vichaa wanaoingilia mtandao wetu wa JF. Peoples Power hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Ndiyo shida ya kukandamiza kinywaji siku za katikati ya wiki, mtu unaamka kichwa kikiwa hakiko sawa harafu unakurupuka kuweka upupu hapa JF. Ulikandamiza kinywaji mpaka umepoteza kumbukumbu kuwa tamko la serikali juu ya mgomo wa madaktari lilishatolewa? Pole sana mzee!
 
John Mnyika na Nyambari Nyangwine wameliweka juu suala la madaktari dakika chache zilopita Bungeni: Kama kawaida naibu Spika ameyeyusha hoja kama hana ndugu wanaotibiwa nchini: IPO SIKU....
 
Wacheni kwanza taratibu za kibunge zifuatwe ikionekana hawatoi suluhisho la uhakika hapo ndo cdm watakapo ingilia kati.
 
Back
Top Bottom