Sakata la Mchanga wa Madini: Rais Magufuli ateua kamati ya Wataalam Kuchunguza Makontena ya Mchanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, leo March 29 2017 ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni;
⦁ Prof. Abdulrahman Hamis Mruma
⦁ Prof. Justianian Rwezaura Ikingula
⦁ Prof. Joseph Bushweshaiga
⦁ Dkt. Yusuf Ngenya
⦁ Dkt. Joseph Yoweza Philip
⦁ Dkt. Ambrose Itika
⦁ Mohamed Zengo Makongoro
⦁ Hery Issa Gombela
Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 31 Machi, 2017 saa 4:00 asubuhi.
 
Kiwango cha Madini kwny Mchanga kitathibitishwa Maabara kwa vipimo sio Wajumbe wa Kamati!

Tumsaidie Rais awe anatumia Mifumo rasmi kufanya kazi badala ya kichwa chake!

Sio kila Jambo ni kuteua tu, Wataalam wa Madini na Maabara wangetosha na kazi ya Kamati ingekuwa kupendekeza labda Mabadiliko ya Sheria na sera za Madini sio Kamati kuchunguza Kiwango cha Madini kwny Mchanga!

Waafrika tunastahiki kudharauliwa na wasio Waafrika
 
Wasomi watupu safi, Ila sijui kama kati yao kuna wanasheria mfano majaji Mara nyingi tunawaona kwenye tume, maana kuna suala la mkataba kuhusu upakiaji na usafirishaji, au wote ni wachenjuaji wa michanga tu.
 
a93665e16ca0fda53aeae0ad4bf1cea7.jpg
Safi Sana Mhe.Rais Wetu Kwa Hatua Hii Nzuri. Tunaomba Wataalam Hao Waitendee Haki Tanzania Kwa Kuhakikisha Usomi Wao Unalinda Rasilimali Zetu. Pia Tunaomba Tanzania Ijitoe kwenye mahakama za kimataifa za usuluhishaji wa migogoro ya kiuwekezaji kama walivyofanya BOLIVIA ili tuepukana na kushtakiwa hovyo na wazungu hao katika mahakama zao wenyewe na hatimaye kutudai Kulipa mamilioni ya dola endapo tunavunja mkataba (Wanasheria waliangalie hili na kufuata taratibu stahiki za kujitoa kwetu kwenye hizo MIGs na BITS - wakisoma hapa watanielewa).
 
Profesa Ntalikwa, katibu mkuu wa madini alitoa ushauri huu wa kuunda kamati ya kuchunguza mchanga. Kilichofuata ni kutumbuliwa on the same day. Sasa imekuwaje amekula Matapishi tena?. JPM Bwana. Mkurupukaji sana. I wonder his decions, ameshindwa kumtumbua Bashite, anatumbua watu wanaotoa right advices.

Ukitaka kupata details ya kilichotokea siku hio, soma link hii hapo chini. Utaona Profesa alitoa ushauri wa kuunda tume ya wataalam while mkurugenzi wa bandari alasema tofauti. Kilichofuatia ni Profesa kutumbuliwa.

Katibu Mkuu Madini abishana, atumbuliwa
Labda alitumbuliwa kwa issue nyingine lakini hiki kinachofanyika sasa kusema kweli ndicho alichokishauri Prof.Ntalikwa.
 
Malalamiko ktk maamuzi in lazima hivyo Chadema subilini bungeni huko ndiko nyumbani kwenu maana hats matawi mfano huku kawe yamefungwa na kuwa sehemu za ufundi radio au fundi wa nguo maana kodi zimeisha na wanachama wsmetokomea mbaka 2020
 
Rais kafanya kizuri sana lakini wote hao kuna sehemu watapigwa chenga kwenye zoezi lao kwani wengi wao hawajafanya kazi migodini.Mining is about practical not theory.Kuna sehemu inahitaji ujanja fulani wa kimigodi.Ngoja nikae kimya.
 
Back
Top Bottom