Sakata la Manji na Wanachama wa Yanga dhidi ya Madega- Picha halisi ya Watanzania

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wadau,

SIku ya mechi kati ya Brazil na Taifa Stars, Klabu ya Yanga ilikuwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama. Tarehe ya Mkutano huo iligongana na tarehe ya mechi kati ya Brazil na Taifa Stars; Mdhamini wa Yanga Yusuf Manji wa Quality Group of Companies katika hali ya kushangaza ambayo ilikuwa na hila ndani yake alitangaza ofa ya tiketi za bure kwa Wanachama wataohudhuria Mkutano huo. Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga; Madega agenda ya Mkutano huo ilikuwa moja- kupitisha mabadiliko ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya YAnga.

Kilichojiri ilikuwa ni kituko, badala ya kujadili agenda iliyopangwa Wanachama walishinikiza agenda yao ya kutaka Uchaguzi. Tarehe aliyoipanga Madega ilipingwa vikali na hatimaye Kamati ya Uchaguzi pamoja na wanachama waliofadhiliwa na Manji wakapanga tarehe yao ambayo kisheria haiwezekani. Baadaye tunajulishwa kuwa tarehe aliyopanga Madega kufanya Uchaguzi Julai 4 ilikuwa ni sahihi zaidi kwani Kamati ya Uchaguzi imelazimika kusogeza mbele zaidi ya tarehe aliyopendekeza MAdega kwani itabidi kwa tarehe mpya ya Kamati ya Uchaguzi, Madege atakuwa amepitisha muda wa kukaa madarakani!

Kinachooneka leo (baada ya Kamati kupendekeza tarehe mpya ya Uchaguzi) ni kuwa kulikwa na shinikizo la aina fulani kutoka kwa Mfadhili wao Manji kupitia kwa Wanachama walipewa tiketi za bure kuiona Mechi ya Brazil Vs Taifa Stars. Shinikizo hilo ni takrima ya Manji kwa wanachama! Hii ni kutokana na mahusianao dhaifu kati ya Madega na Manji kwani Manji amekuwa na nguvu kubwa Yanga dhidi ya Uongozi halali wa Madega.

Tunakumbuka mara baada ya Madega kuchaguliwa Uenyekiti, alisimama kidete kupinga nguvu kubwa ya Manji ya maamuzi kwenye Klabu ya Yanga dhidi ya Uongozi uliochaguliwa. Mtafaruku wao ulileta kituko kingine cha ajabu pale ambapo Wazee wa Yanga wakiongozwa na Mzee Mzimba kumpinga vikali Madega na kumtaka Madega ama akubali kuendelea kuwa chini ya Manji au ajivue Uongozi! Madega likubali shionikizo na kukubali kufanya kazi chini ya Manji! Baada ya muda, MAdega akaonekana kuepuka kuwa Chini ya Manji na kilichojiri ni Yanga kujikuta haina uwezo wa kulipa mishahara ya Wachezaji na Makocha. Kwa Yanga Manji anaonekana kuwa kila kitu- Kiongozi Mkuu na Mfadhili, jambo lolote asilotaka Manji, Uongozi ukifanya bila idhini yake Manji anafinya pesa-no salaries to the coach and players!

Mlolongo huo wa matukio ya Yanga kati ya Manji na Wanachama (waliokula takrima ya Manji) ni picha halisi ya Taifa letu; Watanzania duni wasio na maamuzi juu ya mustakabali wa nchi yao bali wenye pesa (Mafisadi?) wanaofadhili Chama Tawala CCM pamoja na kutuchagulia viongoziw wa kututawala badala ya Viongozi wa kutuongoza pamoja na Wafadhili (IMF, WB) na nchi wafadhili ambao kwa kuona udhaifu wa Viongozi wetu- wa kutukuwa na maamuzi yao binafsi ya Kizalendo bali ya Wenye mapesa, nao imebidi watumie njia hizo hizo za kulazimisha Watawala wetu kufanya yale ambayo wao (Wafadhili) wanayataka.

HITIMISHO
Wito wangu na maombi yangu kwenu Watanzania ni kufumbua macho na kuona hila za akina Manji. Tuache kudanganyika na hizo pesa zao ambazo si zao bali zetu wenyewe, ambazo tunaibiwa kupitia EPA 1 na EPA 2, ambazo tunaibiwa kupitia mikataba laghai kati ya Serikali na Wawekezaji-haina tofauti kati ya Mikataba ya Chifu Mangungo wa Msovelo na Karl Peters- tunaona Makampu ni yanapewa miasamaha ya kutolipa kodi kwa miaka kadhaa na inapoisha Makampuni huuzwa au kuzaliwa Makampuni mapya!

Juzi tumeona tena! Pamoja na Tume ya Bomani na Wananchi kupinga misamaha ya kodi kwa Makampuni ambayo yanapata faida kubwa sana kwa madini yetu bado Serikali imeamua kuwapa msamaha wa kodi ya Mafuta na bajeti imepita hivyohivyo!
 
Huyu Manji si alishatangaza kujivua udhamini wa Yanga, au? Na by the way, kampuni ya Yanga iko wapi? Mbona bado clabu ni tegemezi kwa mdosi mmoja?
 
Back
Top Bottom