Magori amlilia Imani Maugila Madega

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,018
Imani Maugila Madega, “mate” wangu Chuo Kikuu, wakati huo akisoma Sheria na Mimi Biashara lakini mapenzi ya mpira wa miguu hasa Simba na Yanga yakatuweka karibu.

Tulikuwa tunakacha vipindi tunaenda mpirani pamoja na yeye na Marehemu Gerase Lubega!! Ulikuwa ulevi wa mpira uliopindukia!! Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Mimi kufahamiana na Marehemu Imani Madega.

Wakati wa Uongozi wake kuna kundi kinzani lilijitokeza kutaka kumfukuzisha kwa kuitisha kikao Jangwani, lakini Marehemu Madega alizunguka anakojua mkutano ukafutwa na Polisi ikatanda. Kiongozi wa hilo kundi akaitwa Central na kumkuta Madega! Jaribio likazimwa na hatimae akamaliza muhula wale wa Uongozi Yanga. Alikuwa ni Mwamba na Mjanja wa kujua kupambania haki bila kuogopa.

Pia katika historia ya mpira Tanzania atakumbukwa kama Kiongozi wa kwanza katika Vilabu kuondoka madarakani na kuacha bakaa ya pesa! Wengi huacha madeni! Alama kubwa ya Uadilifu.

Baadae tulihudumu wote Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Sir Leaodgar Chilla Tenga! Wakati huo tukiunda utatu kati yake na Mimi na Alex Mgongolwa! Tulikuwa Washauri wakuu wa Sir Tenga. Kabla ya jambo lolote halijafika kwenye Kamati ya Utendaji ni mara nyingi alituita Sisi watatu kuomba ushauri.

Katika maisha yake alikuwa mtu wa kujichanganya na watu. Enzi hizo nyakati za jioni alikuwa mara nyingi alitembelea Brake Point Makumbusho kuja kujigamba na Yanga yake huku akipata supu yake ya samaki na juice fresh.

Katika moja ya majigambo yake ya kukumbukwa ambayo yalifanya Wanasimba waogope ni usajili wa Jimmy Mba toka Cameroon.

Alitamba jioni ile pale Brake Point huku akijinasibu juu ya Kifua kipana cha Jimmy Mbaa ambacho kilikuwa na uwezo wa kubeba Mabeki wawili kwa mpigo Nyoso na Yondani !! Lakini ukweli ulikuja kudhihiri kuwa Jimmy Mbaa hakuwa Mchezaji wa maana! Hizi ndiyo zilikuwa mbwembwe na burdani za Ndugu yetu Madega. Ndugu zake wa Brake Point (Wazee wa Ukuta) tutamkumbuka sana.

Pamoja na kupenda sana Yanga, lakini kwenye haki hakupepesa macho alisema wazi hiki ni sawa na hiki siyo sawa!!

Apumzike kwa amani Marehemu Imani Maugila Madega! Wanasoka tutamkumbuka sana.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Amen
 
Back
Top Bottom