Sakata la Mafao: Serikali kukutana na TUCTA

Sakata la Mafao: Serikali kukutana na TUCTA

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Siku tisa baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kuzungumzia malipo ya pensheni na kupinga kanuni mpya za kukokotoa malipo hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Jenista Mhagama amesema wako tayari kukutana na chombo hicho.

Tucta inadai mapendekezo yake kuhusu kanuni mpya za mafao hayakuzingatiwa na ilitaka mifuko yote ilipe kati ya asilimia 40 na 50 za mkupuo, tofauti na malipo ya asilimia 25% yaliyopo katika kanuni mpya

IMG_20181215_083134.jpg

Chanzo: MWANANCHI, Desemba 15, 2018
 
Chanzo : MWANANCHI, Desemba 15, 2018
Ester alipoibua suala hili wafia chama wa mtaa wa Lumumba walimuita mnafiki, malaya, amechuja nk. Hebu leo wajitokeze japo wamuombe radhi.
 
Nasema 25% ni nyingi, ziwe 5%, tuna miradi mingi sana tunafanya, tujifunze kuchangia maendelo ya nchi, hiyo asilimia 95% iende kwenye miradi ya umeme, reli nk

Watu wajifunze kujitegemea siyo kulia kulia hapa. Hutaki piga mbizi...
 
Rais wa TUCTA ni wa ccm, muswaada ni wa ccm, walioupigia kura ukapita ni wabunge wa ccm, aliye usign ni mwenyekiti wa ccm taifa. Sasa mleta mada ccm wanapokutana kujadili mambo ya chama unawaita serikali na TUCTA?! Hao dugu moja. Hiyo ni ajenda ya uchaguzi ukikaribia utamsikia rais eti anajidai hakuujua na atautengua kujidai anawatetea, uchaguzi ukiisha tu, mtakoma. Na kwakua hiyo itakuwa term ya mwisho, hahaha mtakulana.
 
Nasema 25% ni nyingi, ziwe 5%, tuna miradi mingi sana tunafanya, tujifunze kuchangia maendelo ya nchi, hiyo asilimia 95% iende kwenye miradi ya umeme, reli nk

Watu wajifunze kujitegemea siyo kulia kulia hapa. Hutaki piga mbizi...
[emoji56] [emoji56] [emoji56]
 
Hili jambo ni muhimu sana ni vyema busara ikatumika ili kuweza kulitatua......tusifanye mambo kwa mazoea na jazba......nyakati zimebadilika
 
Rais wa TUCTA ni wa ccm, muswaada ni wa ccm, walioupigia kura ukapita ni wabunge wa ccm, aliye usign ni mwenyekiti wa ccm taifa. Sasa mleta mada ccm wanapokutana kujadili mambo ya chama unawaira serikali na TUCTA?! Hao dugu moja. Hiyo ni ajenda ya uchaguzi ukikaribia utamsikia rais eti anajidai hakuujua na atautengua kujidai anawatetea, uchaguzi ukiisha tu, mtakoma. Na kwakua hiyo itakuwa term ya mwisho, hahaha mtakulana.
actually, 2019 hii nategemea wafanyakazi kilio chao kusikilizwa, wanaoweza hata kuongezewa mishahara n.k lkn ukipita uchaguzi atabatilisha......
 
actually, 2019 hii nategemea wafanyakazi kilio chao kusikilizwa, wanaoweza hata kuongezewa mishahara n.k lkn ukipita uchaguzi atabatilisha......
Hahaha baada ya uchaguzi watasaga meno, maana ndiyo term ya mwisho habembelezi mtu.
 
Siku tisa baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kuzungumzia malipo ya pensheni na kupinga kanuni mpya za kukokotoa malipo hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Jenista Mhagama amesema wako tayari kukutana na chombo hicho.

Tucta inadai mapendekezo yake kuhusu kanuni mpya za mafao hayakuzingatiwa na ilitaka mifuko yote ilipe kati ya asilimia 40 na 50 za mkupuo, tofauti na malipo ya asilimia 25% yaliyopo katika kanuni mpya

View attachment 968565

Chanzo: MWANANCHI, Desemba 15, 2018
Tukta nao hovyooo! Walitakiwa wapate maoni ya wenye fedha kabla ya kutoa tamko la kijinga.
Formula ni 75% mbele na 25% monthly.
 
Hiki kitu siyo rahisi kuzungumzika kama mnavyofikiria.Kwa sasa hazina ina wakati mgumu sana lazima hizo pesa ziwe zinafidia budget ili kuendesha nchi.
 
Huu ni ujuha wa hali juu mtu akatwe pesa yake na ikusanywe kwa zaidi ya miaka 30 leo anastaafu unampa 25% ya makusanyo na zingine umpe kidogo kidogo. Kwani kuna shida gani ukimpa 100% ili tusijuane tena?
 
Siku tisa baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kuzungumzia malipo ya pensheni na kupinga kanuni mpya za kukokotoa malipo hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Jenista Mhagama amesema wako tayari kukutana na chombo hicho.

Tucta inadai mapendekezo yake kuhusu kanuni mpya za mafao hayakuzingatiwa na ilitaka mifuko yote ilipe kati ya asilimia 40 na 50 za mkupuo, tofauti na malipo ya asilimia 25% yaliyopo katika kanuni mpya

View attachment 968565

Chanzo: MWANANCHI, Desemba 15, 2018
Vipo vigezo vingi katika mjadala huu! Suala la kwanza ambalo TUCTA wanatakiwa kuangalia ni uhalali wa Wanachama wa mifuko waliokuwepo kabla ya PSSSF kuingizwa kwenye hili saga la 25% wakati wao halikutakiwa kuwahusu hata kidogo!

Ikumbukwe kuwa, tayari Serikali ilishaleta kanuni hizi 2014 na ikawekwa vizuri na aliyekuwa Waziri mwenye dhamana Mama yetu Gaudensia Kabaka na ikawa kwamba watakaokutwa ndani wataendelea na 50% yao na wale watakaojiunga na PSPF na LAPF baada ya Julai 1, 2014 ndio watahusika na 25% pamoja na madudu mengine yaliyoambatana nayo!

Sasa lack of consistence ndani ya Serikali ndiko kunatufikisha huku! Wafanyakazi endeleeni kudai haki yenu hii kupitia TUCTA au vyama vyenu vya Wafanyakazi, hakina nafahamu wapo Viongozi wenye damu na nyama watawasikiliza na kuondoa hii nightmare!
 
Mnamlipa mstaafu 25%ya mafao yake wakati hata wakati wa utumishi wake hajawahi hata kukopeshwa fedha taslim kwa ajili ya kufanyia biashara ili kumkwamua kiuchumi sasa hakuna jinsi walipeni 100% Kwani hiyo ni haki yao ni jasho lao.
Ushauri wangu;
Huu mfuko wa hifadhi uweke utaratibu wa kutoa mikopo ya kifedha ya kufanyia biashara kwa wanachama wake itawawezesha kuwakwamua. Kiuchumi.

Umri wa kustaafu uwe hiari miaka 45 lazima miaka 55 hii itasaidi vijana wengi kupata ajira.
 
Back
Top Bottom