Sakata la Loliondo lamvuruga Kikwete

Sakata la Loliondo lamvuruga Kikwete

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
551
*Sakata la mgogoro unaorindima kwa sasa kuhusu unyang'anywaji wa Ardhi ya Loliondo kwa lengo la kumpa mwekezaji wa kiarabu umemvuruga sana Rais Kikwete na kusita kujitokeza hadharani kulitolea kauli.

*Hapo awali Kupitia kikao cha baraza la mawaziri iliamriwa kuwa WAKAZI WA LOLIONDO WANYANG'ANYWE ENEO HILO na kumtuma Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kagasheki kwenda kulisimamia kwa nguvu zote, lakini Kauli ya hivi karibuni iliyotolewa rasmi na CCM kupitia kwa Naibu katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba ambaye alitumwa na Secretariety ya CCM akiwa kama mjumbe mkuu wa kamati maalum aliyotumwa kwenda Loliondo kujaribu kutafuta suluhu kwa njia za Kisiasa ya kuwa 'WANANCHI WA LOLIONDO WANA HAKI NA ARDHI YAO NA WAZIRI KAGASHEKI ALIKOSEA KATIKA MAAMUZI YAKE YA KUTAKA KUWANYANG'ANYA ENEO HILO' imemchanganya zaidi rais Kikwete kwa kuwa yeye pia ni mwenyekiti wa CCM na hata mtu aliyewahi kutoa Kibali(Kimakosa?) cha kisheria cha umiliki wa Ardhi hiyo wa wakazi wa Loliondo alikuwa pia waziri wake!!

*Habari za ndani kabisa zinasema kuwa, Rais alikuwa tayari ameamua kumtuma Waziri mkuu Pinda kwenda Loliondo ama kupitia Bunge Kutoa Kauli juu Mgogoro wa Loliondo lakini dakika za mwisho mwisho Pinda alizuiwa(Alikataa?) kufanya jambo lolote maana ingechafua Upepo wote, badala yake Alitumwa Kagasheki aendelee kufa nalo huku Serikali ikipima upepo!!
 
Mwigulu Nchemba[/U] ambaye alitumwa na Secretariety ya CCM akiwa kama mjumbe mkuu wa kamati maalum aliyotumwa kwenda Loliondo kujaribu kutafuta suluhu kwa njia za Kisiasa ya kuwa 'WANANCHI WA LOLIONDO WANA HAKI NA ARDHI YAO NA WAZIRI KAGASHEKI ALIKOSEA KATIKA MAAMUZI YAKE YA KUTAKA KUWANYANG'ANYA ENEO HILO' imemchanganya zaidi rais Kikwete kwa kuwa yeye pia ni mwenyekiti wa CCM ...

Nchemba is out of his mind .. yaani anazuia utekelezaji wa ahadi walizotoa kwa mfadhili wao?
 
.... wameshakula fedha za waarabu kurudisha hawawezi na ardhi hawawezi kuchukua..... WAMASAI WAMEAPA WATAKUFA NA HAWAONDOKI NG'O.....
 
Nafikiri anasubiri mpaka mwisho wa mwezi alitolee ufafanuzi.

Usiwe na haraka, subiri hotuba ya mwisho wa mwezi.
 
Kauli ya Mwigulu ni changa la macho! Ilichokusudia serikali ndicho kitatekelezwa!
 
Ni lini mkulu aliwahi kutoa ufanunuzi kwa wakati kwa masuala mazito kama haya? Ccm ilimtuma mwigulu akafanye nini? Kauli ya mwigulu ndio maamuzi ya sekretarieti?
 
Tusubiri mwisho wa mwezi atalitolea ufafanuzi ila tutegemee ufafanuzi UNAOKANGANYA
 
Pesa ya mwarabu walishakula tangu enzi za kampeni na mikataba binafsi ya biashara yao ya mafuta, return mali ya umma kupitia ardhi ya Loliondo.

Kazi kweli, wana wa Loliondo komaeni mpaka kieleweke na hii itawafungua macho kwingine, kama Dodoma kwenye uranium na kwingineko.
 
"Huu ni upepo tu utapita". "Mpaka mwisho wa mwezi nitakuwa nimeshajua cha kuongea kwenye hotuba, sio lazima liwe hili.Hili atamalizana nalo Pinda kwenye maswali ya waziri mkuu".
 
Kwahiyo wewe unadhani rais ni mtu wakuongea kila siku?kama atahitajika ataliongelea kwa mda atakaotaka ,rais hawezi umizwa kichwa na kipande cha ardhi cha mita 4000 za mraba.
 
kwahiyo wewe unadhani rais ni mtu wakuongea kila siku?kama atahitajika ataliongelea kwa mda atakaotaka ,rais hawezi umizwa kichwa na kipande cha ardhi cha mita 4000 za mraba.

Kipande cha ardhi ni zaidi ya hiyo mita za mraba unazosema wewe.

Kitakachomfanya Raisi aingilie kati ni kushindwa kwa watendaji wake kutatua tatizo kwa kufuata haki, sheria na katiba ya nchi, na zaidi kuweka MASLAHI ya nchi na WANANCHI mbele.
 
kwahiyo wewe unadhani rais ni mtu wakuongea kila siku?kama atahitajika ataliongelea kwa mda atakaotaka ,rais hawezi umizwa kichwa na kipande cha ardhi cha mita 4000 za mraba.

Wakati anakula kiapo alisema hiki kipande si ardhi ya Tanzania? Vinginevyo akiri hadharani kuwa ameshindwa kulinda katiba ya nchi kama alivyoapa. Rais kumpuuza Mtanzania na kumthamini Mwarabu aliyewatumikisha babu zetu kama watumwa na kuwauza kama bidhaa, hii si bure.
 
Had it been ningekuwa advisor wa jk ningemshauri a resign...maana ka fail kila aspect ya uongozi wake
 
Back
Top Bottom