Sakata la Loliondo lamvuruga Kikwete

Sakata la Loliondo lamvuruga Kikwete

Ndugu yangu Tuko wewe unadhani Ile kauli ya Mwigulu Nchemba ni Kauli ya nani? na Kauli ya CCM ni ipi mpaka sasa?

*Jaribu kuunganisha haya ndio utajua kauli ya Mwigulu ndio kauli ya CCM:

1/Mwigulu Nchemba ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM(Mahali popote anakuwepo pasipo Katibu mkuu basi Atakuwa anakaimu nafasi ya katibu mkuu wa CCM ambaye ndiye mtendaji/mratibu mkuu wa CCM)

2/Mwigulu Nchemba alitumwa rasmi na Secretariety ya CCM kama mjumbe mkuu rasmi kwenda kutatua mgogoro wa Loliondo Kisiasa!!(Alienda kujadiliana, kushawishi au kuhitimisha kiini cha mgogoro ule kwa niaba ya CCM, kwa hivyo ni lazima alitakiwa kutoa kauli)

3/Kauli ile aliitoa kwenye mkutano rasmi wa Kichama mbele ya Wananchi(WanaCCM!!), watendaji wote muhimu wa CCM na Serikali.

4/Kabla na hata baada ya Kauli ya Mwigulu Nchemba kutoka hakuna kauli nyingine yoyote uliyowahi kutolewa na CCM taifa kuhusiana na mgogoro wa Loliondo.

5/Toka Secretariety mpya ya CCM kuundwa mwishoni mwa mwaka jana, walikuja na mtindo wa kuwaadabisha viongozi wa serikali hadharani ili kukinusuru Chama mbele ya wananchi(Kauli mbiu ya Chama kuidabisha serikali!!)

umedadafua viizuri sana. lakini sekretariat iliktana na kutoka na maamuzi pamoja na njia ya kukabili mgogoro huu ndio maana nchemba akatumwa. nchemba ni mropokaji na ana uwezo mdogo wa kujenga hoja na upatanishi hivyo kuna uwezekano ile kauli ilimtoka tu baada ya kuona mazingira yalivyo. sasa je, ndicho walichokubaliana ktk secretariet? au uwezo wa ushawishi ulifikia kikomo?
 
Last edited by a moderator:
Loliondo,Kigamboni,Gesi.......n.k kuongoza nchi sio mchezo....IKULU ni pahali patakatifu sio pa kukimbilia!
 
Ni kuzoea kuchezea maisha ya watu na kuthamini ubinafsi. Jambo jema wote hulifurahia
 
umedadafua viizuri sana. lakini sekretariat iliktana na kutoka na maamuzi pamoja na njia ya kukabili mgogoro huu ndio maana nchemba akatumwa. nchemba ni mropokaji na ana uwezo mdogo wa kujenga hoja na upatanishi hivyo kuna uwezekano ile kauli ilimtoka tu baada ya kuona mazingira yalivyo. sasa je, ndicho walichokubaliana ktk secretariet? au uwezo wa ushawishi ulifikia kikomo?
Mkuu nimekupata vema, lakini kuna mambo ya kufafanua.
*Secretarieti ya CCM ilipokaa haikutoa kauli ya Hitimisho bali ilitoa mpango/mwongozo wa Kichama katika kutatua tatizo hilo, Lakini Mwigulu Nchemba alitoa kauli ya Kutaka Kuhitimisha mgogoro huo.

*Kwa nafasi alikuwanayo Mwigulu Nchemba inampa mamlaka ya kukisemia Chama Kisera, Itikadi au Msimamo pasipo hata kikao cha chama kukaa. Hii inaitwa Delegation Of Power+/- Position Authority.

*Yote kwa yote, nani anayejua kama Secretariety ya CCM kama haikumtuma Mwigulu kusema vile?
Kama Mwigulu Hakutumwa na CCM kusema yale, kwanini basi mpaka sasa CCM haijatoa kauli yoyote kumkana?
 
*Sakata la mgogoro unaorindima kwa sasa kuhusu unyang'anywaji wa Ardhi ya Loliondo kwa lengo la kumpa mwekezaji wa kiarabu umemvuruga sana Rais Kikwete na kusita kujitokeza hadharani kulitolea kauli.

*Hapo awali Kupitia kikao cha baraza la mawaziri iliamriwa kuwa WAKAZI WA LOLIONDO WANYANG'ANYWE ENEO HILO na kumtuma Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kagasheki kwenda kulisimamia kwa nguvu zote, lakini Kauli ya hivi karibuni iliyotolewa rasmi na CCM kupitia kwa Naibu katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba ambaye alitumwa na Secretariety ya CCM akiwa kama mjumbe mkuu wa kamati maalum aliyotumwa kwenda Loliondo kujaribu kutafuta suluhu kwa njia za Kisiasa ya kuwa 'WANANCHI WA LOLIONDO WANA HAKI NA ARDHI YAO NA WAZIRI KAGASHEKI ALIKOSEA KATIKA MAAMUZI YAKE YA KUTAKA KUWANYANG'ANYA ENEO HILO' imemchanganya zaidi rais Kikwete kwa kuwa yeye pia ni mwenyekiti wa CCM na hata mtu aliyewahi kutoa Kibali(Kimakosa?) cha kisheria cha umiliki wa Ardhi hiyo wa wakazi wa Loliondo alikuwa pia waziri wake!!

*Habari za ndani kabisa zinasema kuwa, Rais alikuwa tayari ameamua kumtuma Waziri mkuu Pinda kwenda Loliondo ama kupitia Bunge Kutoa Kauli juu Mgogoro wa Loliondo lakini dakika za mwisho mwisho Pinda alizuiwa(Alikataa?) kufanya jambo lolote maana ingechafua Upepo wote, badala yake Alitumwa Kagasheki aendelee kufa nalo huku Serikali ikipima upepo!!
Hati za umiliki za wanakijiji Loliondo kisheria haziwezi kutambulika kama zilitolewa kwa makosa. Zilitolewa na maafisa waliokua katika nyadhifa zao kwa mujibu wa sheria.
Kwa maoni yangu, hata kama maafisa waliotoa hizo hati wangeadhibiwa na mahakama au mwajiri wao kwa kutoa hizo hati bado hati hizo zingekua halali.
Jambo la aibu na kusikitisha kwa serikali hii ya ccm ni kusema bila haya kwamba hati za umili kwa wanavijiji zilitolewa kwa makosa huku nia ikiwa kuwaongezea ardhi wageni wanaowanyanyasa raia. Hao waarabu ndio waliopewa ardhi ya wananchi wa Tanzania kwa makosa na muda wa kusahihisha kosa hilo sasa umewadia
 
Wabongo wanasumbulia na njaa na uongozi wa kilaghai, punguwani, Ardhi ya Loliondo imilikiwa kihalali na wananchi, nahisi Waziri Kagasheki ana usingizi au anaumwa malaria.
 
Mwigulu anatamka yake Kagasheki ana ya kwake Jk na yake.Badala ya kutatua mugogoro huu naona tunaelekea kupata dawa nyingine ya mseto kwa ajili ya kutibu malalia na si kutatua mgogoro wa ardhi.
 
Nyie wanaloliondo kwanini mnakubali kutumiwa na CHADEMA? Teh te te Ritz, Ze marcopolo, Lukosi, Sumu etc mko wapi?

Hapa huaoni. Ni seme tu wamejitaidi kuutetea ccm na serikali yao lakini ndo hivyo tena, inaitaji moyo.
 
Mkuu Elungata nani alikwambia mwarabu ''alikodi'' hiyo ardhi?

Katika uhalisia ni kwamba Mwarabu ''Alimilikishwa'' ardhi hiyo, ndio maana yuko huru nayo kwa kitu chochote anachokitaka kufanya juu ya ardhi hiyo.
Toka lini Uwindaji ukafanyika kwa ndege za kijeshi, Uchimbaji wa madini, ujenzi wa kiwanja cha ndege, ujenzi wa mikonga ya mitandao ya simu za mkononi nk.

Kama unabisha iambie serikali yako imtimue huyo mwarabu sasa, ili uone moto wake.

Ushabiki ni mbaya jamani. I believe we great thinker. Uwindaji kwa ndege za kijeshi kweli? Uchimbaji wa madini ujenzi wa kiwanja cha ndege? Do you know the difference between an airport and an airstrip? Loliondo game controlled area is indeed a hunting block just like any other hunting block in this country. Kwa hiyo na makampuni mengine yenye kufanya uwindaji wa kitalii wamemilikishwa ardhi pia au ni ortello tu?
 
Last edited by a moderator:
Haki huinua taifa lakini dhambi ni chukizo; rushwa hupofusha macho na upendeleo ni ubatili. Hakuna dawa kwa ccm kujiosha dawa ni moja tu kupisha wengine ili ijitathimini ikiwa pembeni
 
Hili swala la LOLIONDO ni Sanda ya Kufunikia Maiti CCM, ktk Mazishi ya 2015!!

Huyu MWIGULU MZINZI kazi anayo mwaka huu! Sijui atafanya nini maana Ngoma imenoga kwa sasa! KAGASHEKI amesema Swala la Loliondo ni la Kitaalamu na Kisheria na si la Kisiasa! Kama MWIGULU MZINZI ameropoka, hiyo ni kauli yake na sio ya Serikali!!

MWIGULU aelewe kwamba Pesa za Mwarabu wameshakula wao CCM, sasa wananchi wa Loliondo wanasema hawajui hilo na wapo tayari kwa lolote!

Ushauri kwa MWIGULU MZINZI, kwa kuwa Mambo yamekua Magumu basi kwa vile yeye ni Kiherehere sana na anajidai kwamba anakereketwa kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya CCM, kama tunavyomuona Bungeni, basi Ajipendekeze [Yeye Mwigulu] kwa Mwarabu na hata ikiwezekana ampe "SABURI" ili Noma iishe!

CCM HAIKUBALIKI SOTE TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA!!!
 
Ushabiki ni mbaya jamani. I believe we great thinker. Uwindaji kwa ndege za kijeshi kweli? Uchimbaji wa madini ujenzi wa kiwanja cha ndege? Do you know the difference between an airport and an airstrip? Loliondo game controlled area is indeed a hunting block just like any other hunting block in this country. Kwa hiyo na makampuni mengine yenye kufanya uwindaji wa kitalii wamemilikishwa ardhi pia au ni ortello tu?
Mahanjam,
Inaonekana wewe unajua zaidi katika saga hili. Tueleze basi kampuni zilizomilikishwa ardhi ya uwindaji wa kitalii mbali na Ortello
 
Jamani naomba mnikumbushe. Ni tukio gani kweli ambao jk amewahi kuingilia kati na kutoa tamko ama uamuzi rmgogoro wowote ile, uamzi ambao una ladha ya tamko la mkuu wa nchi?​
Haha haa...., Zanzibar ni nchi ndani ya ''Tanzania''
 
Ushabiki ni mbaya jamani. I believe we great thinker. Uwindaji kwa ndege za kijeshi kweli? Uchimbaji wa madini ujenzi wa kiwanja cha ndege? Do you know the difference between an airport and an airstrip? Loliondo game controlled area is indeed a hunting block just like any other hunting block in this country. Kwa hiyo na makampuni mengine yenye kufanya uwindaji wa kitalii wamemilikishwa ardhi pia au ni ortello tu?

Hivi ndugu yangu unajua unachokisema? Unajua mambo yanayofanyika pale? Kwa taarifa yako iila hawa jamaa wakitaka kuondosha mizigo yako lazima Kinana(mndiyo huyu huyu unayemjua wewe) aje uwanjani kurahisisha uondokaji, pale
 
*Sakata la mgogoro unaorindima kwa sasa kuhusu unyang'anywaji wa Ardhi ya Loliondo kwa lengo la kumpa mwekezaji wa kiarabu umemvuruga sana Rais Kikwete na kusita kujitokeza hadharani kulitolea kauli.

*Hapo awali Kupitia kikao cha baraza la mawaziri iliamriwa kuwa WAKAZI WA LOLIONDO WANYANG'ANYWE ENEO HILO na kumtuma Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kagasheki kwenda kulisimamia kwa nguvu zote, lakini Kauli ya hivi karibuni iliyotolewa rasmi na CCM kupitia kwa Naibu katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba ambaye alitumwa na Secretariety ya CCM akiwa kama mjumbe mkuu wa kamati maalum aliyotumwa kwenda Loliondo kujaribu kutafuta suluhu kwa njia za Kisiasa ya kuwa 'WANANCHI WA LOLIONDO WANA HAKI NA ARDHI YAO NA WAZIRI KAGASHEKI ALIKOSEA KATIKA MAAMUZI YAKE YA KUTAKA KUWANYANG'ANYA ENEO HILO' imemchanganya zaidi rais Kikwete kwa kuwa yeye pia ni mwenyekiti wa CCM na hata mtu aliyewahi kutoa Kibali(Kimakosa?) cha kisheria cha umiliki wa Ardhi hiyo wa wakazi wa Loliondo alikuwa pia waziri wake!!

*Habari za ndani kabisa zinasema kuwa, Rais alikuwa tayari ameamua kumtuma Waziri mkuu Pinda kwenda Loliondo ama kupitia Bunge Kutoa Kauli juu Mgogoro wa Loliondo lakini dakika za mwisho mwisho Pinda alizuiwa(Alikataa?) kufanya jambo lolote maana ingechafua Upepo wote, badala yake Alitumwa Kagasheki aendelee kufa nalo huku Serikali ikipima upepo!!

Wewe kama hujui hiyo corridor ya wanyama imeshagawanywa kwa vigogo na watoto wa......kwa hiyo ma legwanani wanatumika tu kuleta vurugu ili serikali isichukue au kuwapokonya uhondo huo wa mgao.
 
Kwahiyo wewe unadhani rais ni mtu wakuongea kila siku?kama atahitajika ataliongelea kwa mda atakaotaka ,rais hawezi umizwa kichwa na kipande cha ardhi cha mita 4000 za mraba.

Si ndio dharau zenu.........hata kura za walimu alisema kejeli kama hizi na siku ya siku akajichekesha akisema wamemnukuu vibaya.....mita 4000 waona ndogo kama hazimuumizi kichwa mbona vijakazi wake(Mwigulu,Kagasheki) wanahaha kwenda kuwatuliza Morani?
 
Back
Top Bottom