Shinto
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 1,781
- 98
Hivi ndugu mnaukumbuka ule mkasa uliotokea kenya kama miaka miwili iliyopita? Watu zaidi ya kumi walipata upofu wengi kufariki baada ya kunywa changa'a iliyoongezwa chemical.
Sasa jana nilikutana na eye witness aliyekuwepo kwenye hicho club ya pombe za kienyeji siku ya tukio.
Ilikuwa hivi: Watu waliendelea kuywanga chang'aa kama kawaida kuanzia mida ya saa 6 hivi mchana. Kila aliyekuwepo alisifia lile tungi la siku ile kuwa ni kiboko zaidi ya siku zote..
Ilipotimia mida ya saa tisa, ndipo kila aliyekuwa anakunywa aliaanza kuona nuru ya macho inafifia, lakini wakazani labda giza tu la mawingu linaingia..
Baada ya kama nusu saa hivi, upofu ulikuwa tayari umewapata , lakini wao waliona ni giza totoro tu..
mlevi mmoja alisikika akisema, ' jua limezimika jo', mwengine akatia, ' naona uskiu wa leo ni mkali washa taa' mwingine akatia ' acha tuendelee tu..'
Kumbe masikini upofu umeshawakamata, akili zao hazitambui!
Ulevi noma!