Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo

Muhongo ana tatizo la mahusiano....hana lugha ya kiungwana (civilian) wala siyo mtu wa majadiliano. Atapata shida kama ataamua kubaki ktk siasa. Kwa utendaji na taalum kama mhandisi nafikiri hakuna tatizo
 
kwa hiyo hii Gesi ikishafika Dar Viwanda vyote viko kwenye yadi moja tu??? Acha kutumika bwana!! Kwanza Watanzania wanataka Mkataba uwekwe wazi wa huu Mradi, pili uzalishaji waweza fanyika Mtwara na Dar kukawa na Center ya distribution. Mbona maji ya Ruvu kiwanda chake kiko pale Ruvu na yakifika Dar ndo yanasambazwa kwa matumizi.

Tatizo linajirudia, unasoma ili ubishe badala usome ili unielewe niliandika maandishi yooote haya. Ndugu yangu Chungurumbira, acha ushabiki wa kijinga. Kama maji kiwanda kiko Ruvu, je bomba linaloenda nyumbani kwako linatokea Ruvu moja kwa moja au kuna Bomba kubwa limekuja hadi mjini na distribution inaanzia hapo kuja kwako?

Shida yetu hatupendi kuambiwa ukweli. Yaani kujaribu tu kukueleza kuwa haya yoote unayodai tayari yako hivyo, wewe umeshawahi kusema NATUMIKA.

Usinichoshe, ashakhum si matusi, wewe ni MPUMBAVU. Hiyo kwenye red ndicho ambacho mimi nimetoka kusema. Nimekuita mpumbavu kwa kuwa mpumbavu ni mtu asiyependa kujifunza. Hebu soma kwanza nilichoandika halafu utakubaliana na mimi kuwa wewe ni wa hovyo kabisa.

Unatoa mifano ya RUVU kipumbavu kabisa. Kama maji yanachakatwa Ruvu, yanabebwa kwa bomba kubwa mpaka Ubungo, yanaingia kwenye tank, hapo yanatoka mambomba tena makubwa kwenda hili Kurasini, hili Mabibo, hili Keko na kadhalika, sasa hiyo inatofauti gani na nilichosema kuwa Gesi itachakatwa Mtwara, itasafirishwa hadi Dar, hapo itagawiwa kwa watumiaji, au wewe unabishana nini sasa?
 
Last edited by a moderator:
Huyu mtu vipi yaani kwa sasa Pinda anafanya nini Mtwara kama ananchi hawajui nyimbo wa mashairi wanayoimba
 
Wananchi wa mtwara wanataka vitendo, wameshachoka kupewa ahadi kedekede zisizotekelezeka.
Tangu kikwete aingie madarakani amewaahidi mambo mengi sana moijawapo ni ujenzi wa barabara lakini kwa muda wa miaka yake saba ameweza kujenga barabara yenye urefu wa kilometa 60 tu!!

Wananchi wa Lindi waliahidiwa kiwanda cha mbolea sasa ni miaka nenda rudi lakini hakuna dalili ya kiwanda hicho kujengwa. Kama hiyo haitoshi, ilani ya uchaguzi ya ccm 2010 ibara ya 63 kifungu h na k vinataja ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme mtwara (300MW) kwa gesi ya mtwara bay na Kinyerezi (240MW) kwa gesi ya songosongo. Sasa imekuwaje tena ccm na serikali yake wanahamisha magoli? au kwakuwa wamezoea kuhamisha na wananchi hukaa kimya? Mwaka jana mwishoni raisi kikwete alipokea ripoti ya wachina na siemens juu ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mtwara/Lindi hadi singida yenye urefu wa kilometa 1,100 je mradi huo umeshatekelezwa?

Kama hali yenyewe ndio hii, unadhani wananchi hawana haki ya kumdharau profesa Muhongo ambaye ameshindwa kabisa kujibainisha usomi wake na kuishia kuongea na kutoa mifano dhaifu ambayo huwezi kumtofautisha na lakairo ama profesa maji marefu walioishia darasa la pili!!??

Safari hii hata ccm ifanyeje wananchi wa mtwara hawatakubali kurudi nyuma. Serikali lazima ijenge mtambo wa kuzalisha umeme kwa gesi asilia mkoani mtwara na ndipo iuingize kwenye gridi ya taifa. No more no less!!

Kaka tafadhali weka kwanza kusudi la kunielewa, vinginevyo hata nikiongea mwaka mzima kama umedhamiria tu kubishana hakuna tunachoweza kuongea.

Kiwanda cha Mbolea kilichoahidiwa, malighafi ni ya kutengenezea mbolea ni mabaki ya uchafu unaotokana na shughuli ya gesi. Kama gesi haijachimbwa bado, kiwanda kitazalisha mbolea kutumia hewa? Hapa utaona kwamba, ni mpaka gesi izalishwe ndio mbolea itapatikana, AU?

Twende kwenye hili la umeme. Tata Mwita Maranya, naomba ujiulize mwenyewe, ikiwa wewe ndio kiongozi wa nchi hii, utafanya nini kwanza kati ya haya:
1. Kujenga mtambo wa umeme kwa ajili ya Dar es Salaam ambayo ina uhaba wa umeme na mahitaji ni makubwa, au kujenga mtambo Lindi na Mtwara ambapo hata uliopo hautumiki wote? (Hata hivi sasa, Mtwara kuna uzalishaji wa 11MW ambapo ni 5MW tu ndio zinatumika) sasa mnataka ufahari wa kwamba kuna zingine 306MW hazitumiki au ni nini?

2. Unaweza kuniambia Mtwara kama Mtwara inanufaika nini na ujenzi wa njia ya umeme unaoenda Singida ikizingatiwa hakuna mkoa unaolipwa fedha kwa kuwa mkoa huo kuna power station au power lines zimepita?
Mwita Maranya, gesi matumizi yake si umeme tu. Gesi lazima ifike Dar es Salaam liliko soko kubwa. Hebu jenga picha ni akili gani itakuwa imetumika, kuleta bomba Dar kwa ajili ya kusupply gesi viwandani, majumbani na kwenye magari, halafu wewe huyo huyo ujenge tena njia ya umeme toka Mtwara hadi Dar kuuingiza kwenye Grid ya Taifa!!!

Maneno yako ya kumalizia ya No more, no less hayaambatani na logistic reasoning ni ushabiki na si zaidi.

Tusipende kuwa washabiki ndugu zangu. Acha nikwambie kitu. Amin Dangote (yule Mnigeria tajiri mkubwa kuliko wote Africa) anaplan kujenga kiwanda cha Cement Mtwara. Mawazo ya kujenga kiwanda yanakuja kwa kuwa tu anajua atapata malighafi ya kutengenezea cement kutokana na machimbo na uchakataji wa gesi. Hapa utasikia wengine wanasema tumeahidiwa kiwanda mbona hakijengwi, jibu linakuja pale pale, cement atazalisha kwa mabaki ya gesi. Sasa nyie mnatakaje?
 
Last edited by a moderator:
Kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni....
Kweli kuna haja ya kuangalia kwa makini viongozi tunaowapa dhamana ya kutuongoza. Huyu Prof. sizani kama ana cha kujivunia katika kutumikia uma. Inaelekea yeye ndiye mshauri no. 1 wa Jk katika kumshauri ----- kuhuusu GAS na Madini.
 
Mi nauliza tu, huyu Waziri Profesa hana uhusiano wowote na yule wa kina Masanja wa Orijino Komedi maarufu kama "La' Profeseri"?! Nahisi kama jamaa huwa wanamgusa huyu! Mtu ni waziri wa nishati, wananchi wanamgogoro juu ya nishati, anaulizwa ye anasema hajui?? Kweli? Ningekuwa mwandishi ningemjibu kwa swali kuwa kama yeye waziri husika wa nishati hajui wanamtwara wanachohitaji, anataka tumuulize waziri wa mifugo?! Hovyo!
 
Duh! Huyu jamaa nilikuwa namtegemea sana, sitaki kuamini kuwa ni bubusa kiasi hiki! Prof Muhongo unatukatisha tamaa tuliokuamini. Yaani bora uwe unakaa kimya tu uwaachie wanasiasa manaibu wako wakina Simbachawene wawe wanatoa matamko.
 
Muhongo ana tatizo la mahusiano....hana lugha ya kiungwana (civilian) wala siyo mtu wa majadiliano. Atapata shida kama ataamua kubaki ktk siasa. Kwa utendaji na taalum kama mhandisi nafikiri hakuna tatizo

Nafikiri tatizo lake ni u-profesa wake. Unampa 'superiority complex' ambayo haipo. Anahisi yeye amebobea kuliko mtanzania yeyote katika gesi. After all yeye ni profesa wa 'geology'- elimu ya miamba si mhandisi wa kuchimba gesi au mchumi wa gesi. Si vyema kumjadili yeye kama mtu binafsi lakini anayotetea yanatia shaka ..
 
cement atazalisha kwa mabaki ya gesi. Sasa nyie mnatakaje[/COLOR]?

Sina sababu ya kujibu hayo mengine uliyoandika kwakuwa hakuna hata hoja ya kujadili zaidi ya kuwakilisha tabaka tawala na hujipi nafasi ya kutazama hoja ya wanamtwara bali unaimbishwa wimbo na watawala bila kujua nani kautunga na kwa madhumuni gani.

Kwa akili yako unataka niamini kwamba Tanga Cement (Tanga), Mbeya Cement (Mbeya), Twiga Cement (Dsm), Rhino Cement (Tanga na Mkuranga), Lake Cement (Dsm) na Dar es salaam (Cement) viwanda vyote hivyo vinafanya kazi kwakuwa huko viliko kwakuwa malighafi ambayo ni mabaki ya uchakataji wa gesi inapatikana kwa wingi? Ndugu shizukan ni aibu sana kuongelea vitu ambavyo hujui hata abc zake. Malighafi kubwa na ya msingi inayotakiwa kwa ajili ya kiwanda cha cement ni gypsum ambayo ndiyo sababu ya hivyo viwanda nilivyovitaja vimeendelea kuwepo kabla ya kuwepo kwa uvumbuzi na matumizi ya gesi asilia.

Siku nyingine usikurupuke kuandika vitu usivyovifahamu kwakuwa tu umetumwa kuitetea serikali yako. Haya ndiyo maswali ya msingi ambayo seri8kali ya ccm imeshindwa kuyajibu na kubaki kupiga propaganda za hovyo. Sasa kwakuwa wananchi wanauelewa wa kutosha wanawachora tu jinsi mnavyoweweseka. Wewe na profesa Muhongo wote ni manzi ga nyanja....
 
Duh, yaani ...eti wana mkakati wa kufanya bandari ya Mtwara iwe kubwaaaaaa!! yakufanya biashara ya gesi Africa mashariki ..sasa kama wanao huo mkakati bomba la kazi gani???? si wajenge bandari basi wazalishe gesi, yaani wanawafanya wenzao kama watoto wadogo vile...."nyamaza!, ukiendelea kulia sintakununulia gari" kumbe hakuna gari, kama lipo ni toy....

Ati wawekezaji watahamia Mombasa sijui Beira. oooh!!! kwa hiyo mmliki wa gesi ni mwekezaji ...lazima kumpigia magoti asiondoke ili walau tupate chapaa za bandari. Kama wa Mtwara ambao ni sehemu ya watanzania wanachomiliki ni korosho tu sasa useme gesi inamilikiwa na nani? !

Ati, wamepeleka viongozi nje kusoma hadi viongozi wa vijiji, ha! kumbe ulaji umeanza mapema eeh , hebu kwanza litajwe jina moja tu la kiongozi wa kijiji aliyepelekwa nje "kujifunza faida za gesi". gesi ya Mtwara inayopigiwa kelele imevumbuliwa juzi juzi tu sasa mmetumia muda gani kuhakikisha watu wa mtwara na watanzania kwa ujumla wameshirikishwa kwenye mradi? walau hata kusoma mikataba tu... kwenye ufisadi mbio mbio, kwa maswala ya taifa eti "mikakati" DANGANYA TOTO.

Professor, weka mikataba 26 ya gesi wazi tuisome, halafu ueleze kwa nini sera ya utafutaji/uvunaji wa gesi ndio inaundwa sasa hivi, wakati gesi ilianza kuvumbuliwa tokea mwaka 1974??

Bora angenyamaza tu kuliko kuongea aliyoongea....yaani katia petrol kwenye moto
 
Kaka tafadhali weka kwanza kusudi la kunielewa, vinginevyo hata nikiongea mwaka mzima kama umedhamiria tu kubishana hakuna tunachoweza kuongea.

Kiwanda cha Mbolea kilichoahidiwa, malighafi ni ya kutengenezea mbolea ni mabaki ya uchafu unaotokana na shughuli ya gesi. Kama gesi haijachimbwa bado, kiwanda kitazalisha mbolea kutumia hewa? Hapa utaona kwamba, ni mpaka gesi izalishwe ndio mbolea itapatikana, AU?

Twende kwenye hili la umeme. Tata Mwita Maranya, naomba ujiulize mwenyewe, ikiwa wewe ndio kiongozi wa nchi hii, utafanya nini kwanza kati ya haya:
1. Kujenga mtambo wa umeme kwa ajili ya Dar es Salaam ambayo ina uhaba wa umeme na mahitaji ni makubwa, au kujenga mtambo Lindi na Mtwara ambapo hata uliopo hautumiki wote? (Hata hivi sasa, Mtwara kuna uzalishaji wa 11MW ambapo ni 5MW tu ndio zinatumika) sasa mnataka ufahari wa kwamba kuna zingine 306MW hazitumiki au ni nini?

2. Unaweza kuniambia Mtwara kama Mtwara inanufaika nini na ujenzi wa njia ya umeme unaoenda Singida ikizingatiwa hakuna mkoa unaolipwa fedha kwa kuwa mkoa huo kuna power station au power lines zimepita?
Mwita Maranya, gesi matumizi yake si umeme tu. Gesi lazima ifike Dar es Salaam liliko soko kubwa. Hebu jenga picha ni akili gani itakuwa imetumika, kuleta bomba Dar kwa ajili ya kusupply gesi viwandani, majumbani na kwenye magari, halafu wewe huyo huyo ujenge tena njia ya umeme toka Mtwara hadi Dar kuuingiza kwenye Grid ya Taifa!!!

Maneno yako ya kumalizia ya No more, no less hayaambatani na logistic reasoning ni ushabiki na si zaidi.

Tusipende kuwa washabiki ndugu zangu. Acha nikwambie kitu. Amin Dangote (yule Mnigeria tajiri mkubwa kuliko wote Africa) anaplan kujenga kiwanda cha Cement Mtwara. Mawazo ya kujenga kiwanda yanakuja kwa kuwa tu anajua atapata malighafi ya kutengenezea cement kutokana na machimbo na uchakataji wa gesi. Hapa utasikia wengine wanasema tumeahidiwa kiwanda mbona hakijengwi, jibu linakuja pale pale, cement atazalisha kwa mabaki ya gesi. Sasa nyie mnatakaje?

Labda ungesoma kwanza nyaraka za wana Mtwara kuhusu hili suala, hawajasema gesi isiondoke, wanataka waone matunda yake kwanza hapo walipo, kwa sababu wameachwa nyuma kwa miaka mingi, na hata sasa ambapo mlangoni kwao kuna opportunity ya kufaidika walau kidogo wanapitwa tu kama vile hawapo...

wamegundua kwamba "plans za mnaijeria tajiri, mikakati ya libandari likubwaaaa, na mipango kabambe" ni danganya toto, vinginevyo ingetekelezwa kabla au hata sambamba na ujenzi wa bomba la gesi. wanataka viwanda vijengwe, bandari ijengwe, barabara zijengwe etc ili nao waweze kupata ajira waweze kumudu kusomesha watoto wao kwenye shule za kawaida na sio unyagoni, na waweze kumudu hata huo umeme waliopunguziwa bei ambao sasa hivi hawana ubavu wa kuugusa kwa sababu ya umaskini.
 
Sina sababu ya kujibu hayo mengine uliyoandika kwakuwa hakuna hata hoja ya kujadili zaidi ya kuwakilisha tabaka tawala na hujipi nafasi ya kutazama hoja ya wanamtwara bali unaimbishwa wimbo na watawala bila kujua nani kautunga na kwa madhumuni gani.

Kwa akili yako unataka niamini kwamba Tanga Cement (Tanga), Mbeya Cement (Mbeya), Twiga Cement (Dsm), Rhino Cement (Tanga na Mkuranga), Lake Cement (Dsm) na Dar es salaam (Cement) viwanda vyote hivyo vinafanya kazi kwakuwa huko viliko kwakuwa malighafi ambayo ni mabaki ya uchakataji wa gesi inapatikana kwa wingi? Ndugu shizukan ni aibu sana kuongelea vitu ambavyo hujui hata abc zake. Malighafi kubwa na ya msingi inayotakiwa kwa ajili ya kiwanda cha cement ni gypsum ambayo ndiyo sababu ya hivyo viwanda nilivyovitaja vimeendelea kuwepo kabla ya kuwepo kwa uvumbuzi na matumizi ya gesi asilia.

Siku nyingine usikurupuke kuandika vitu usivyovifahamu kwakuwa tu umetumwa kuitetea serikali yako. Haya ndiyo maswali ya msingi ambayo seri8kali ya ccm imeshindwa kuyajibu na kubaki kupiga propaganda za hovyo. Sasa kwakuwa wananchi wanauelewa wa kutosha wanawachora tu jinsi mnavyoweweseka. Wewe na profesa Muhongo wote ni manzi ga nyanja....
Mwita Maranya, yoote niliyoyaweka hapo hukuyaona bali uliona kipande hiki tu cha kukupatia ushindi wa UBISHI. Sikumaanisha kuwa ni gesi ndio hugeuzwa kuwa cement, mimi si mtaalamu wa cement na wala sijatumwa na mtu kama unavyosema lkn sipendi unafiki kama uliotumia kuruka mada zoote na kuja hapa na kipengele kimoja tu ili uendeleze ubishi.

Cement hutengenezwa kwa miamba. Lakini hii miamba huchomwa. Namna za kuchoma (kiln) hutofautiana kuzingatia na upatikanaji wa malighafi za kuchomea. Kuna wanaotumia petroleum coke, coal, na natural gas extracts. Sasa kama hii ndio imegeuka mada kwa manufaa ya ubishi, itabidi twende darasani. Gypsum haichukuliwi na kupakiwa kwenye viroba kuuzwa mitaani.

Viwanda vya cement vina matumizi makubwa ya fuel, lkn upatikanaji wa hizi extracts unarahisisha uzalishaji kwa kiwango kikubwa. Kwa hiyo sioni point hapa, kwani hata niliposema mbolea itazalishwa mbona hukusema mbolea hupatikana kwa kinyesi cha wanyama, si ni kwa vile unajua kuna namna mbali mbali za mbolea na upatikanaji wake.

Acha kurukaruka, jibu hoja zangu za msingi
 
Last edited by a moderator:
Labda ungesoma kwanza nyaraka za wana Mtwara kuhusu hili suala, hawajasema gesi isiondoke, wanataka waone matunda yake kwanza hapo walipo, kwa sababu wameachwa nyuma kwa miaka mingi, na hata sasa ambapo mlangoni kwao kuna opportunity ya kufaidika walau kidogo wanapitwa tu kama vile hawapo...

wamegundua kwamba "plans za mnaijeria tajiri, mikakati ya libandari likubwaaaa, na mipango kabambe" ni danganya toto, vinginevyo ingetekelezwa kabla au hata sambamba na ujenzi wa bomba la gesi. wanataka viwanda vijengwe, bandari ijengwe, barabara zijengwe etc ili nao waweze kupata ajira waweze kumudu kusomesha watoto wao kwenye shule za kawaida na sio unyagoni, na waweze kumudu hata huo umeme waliopunguziwa bei ambao sasa hivi hawana ubavu wa kuugusa kwa sababu ya umaskini.

Waone matunda ya gesi ikiwa ardhini?
 
Kaka tafadhali weka kwanza kusudi la kunielewa, vinginevyo hata nikiongea mwaka mzima kama umedhamiria tu kubishana hakuna tunachoweza kuongea.

Kiwanda cha Mbolea kilichoahidiwa, malighafi ni ya kutengenezea mbolea ni mabaki ya uchafu unaotokana na shughuli ya gesi. Kama gesi haijachimbwa bado, kiwanda kitazalisha mbolea kutumia hewa? Hapa utaona kwamba, ni mpaka gesi izalishwe ndio mbolea itapatikana, AU?

Twende kwenye hili la umeme. Tata Mwita Maranya, naomba ujiulize mwenyewe, ikiwa wewe ndio kiongozi wa nchi hii, utafanya nini kwanza kati ya haya:
1. Kujenga mtambo wa umeme kwa ajili ya Dar es Salaam ambayo ina uhaba wa umeme na mahitaji ni makubwa, au kujenga mtambo Lindi na Mtwara ambapo hata uliopo hautumiki wote? (Hata hivi sasa, Mtwara kuna uzalishaji wa 11MW ambapo ni 5MW tu ndio zinatumika) sasa mnataka ufahari wa kwamba kuna zingine 306MW hazitumiki au ni nini?

2. Unaweza kuniambia Mtwara kama Mtwara inanufaika nini na ujenzi wa njia ya umeme unaoenda Singida ikizingatiwa hakuna mkoa unaolipwa fedha kwa kuwa mkoa huo kuna power station au power lines zimepita?
Mwita Maranya, gesi matumizi yake si umeme tu. Gesi lazima ifike Dar es Salaam liliko soko kubwa. Hebu jenga picha ni akili gani itakuwa imetumika, kuleta bomba Dar kwa ajili ya kusupply gesi viwandani, majumbani na kwenye magari, halafu wewe huyo huyo ujenge tena njia ya umeme toka Mtwara hadi Dar kuuingiza kwenye Grid ya Taifa!!!

Maneno yako ya kumalizia ya No more, no less hayaambatani na logistic reasoning ni ushabiki na si zaidi.

Tusipende kuwa washabiki ndugu zangu. Acha nikwambie kitu. Amin Dangote (yule Mnigeria tajiri mkubwa kuliko wote Africa) anaplan kujenga kiwanda cha Cement Mtwara. Mawazo ya kujenga kiwanda yanakuja kwa kuwa tu anajua atapata malighafi ya kutengenezea cement kutokana na machimbo na uchakataji wa gesi. Hapa utasikia wengine wanasema tumeahidiwa kiwanda mbona hakijengwi, jibu linakuja pale pale, cement atazalisha kwa mabaki ya gesi. Sasa nyie mnatakaje?

Mkuu shizukan mimi naomba nikuulize maswali madogo yafuatayo, tumeletewa hadi press release ya IKULU, na pia Mwita ame-quote manifesto ya CCM inayoonyesha kwamba serikali ilikuwa na mpango ya kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa 360MW Mtwara. Je unataka kutuambia huo Mpango wa serikali ulikuwa ni HADAA TU ya serikali kwa WanaMtwara? Maana unasema Mtwara sasa hivi kuna mtambo wa kuzalisha 11MW na matumizi ya Mtwara ni 5MW tu.

Pili Serikali inasema ina mpango wa kujenga viwanda vya cement na mbolea Mtwara. Je hizo 11MW ambazo ndiyo zinazalishwa sasa hivi Mtwara zitatosha kuendesha hivyo viwanda vinavyotarajiwa kujengwa Mtwara?.

POINT TO NOTE: WanaMtawara hawakatai gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam, bali wanataka waelezwe ni kwa vipi watafaidika na rasilimali ya gesi iliyovumbuliwa Mtwara. Huu ni upotoshaji ambao serikali inaufanya mara kwa mara. Naomba usome tamko la Shura ya maimum wa Mtwara.
 
Siamini kama huyu ndiye yule Waziri aliyesema "mgao wa umeme ukitokea tena atajiuzulu" au na hapa hakujua alichokuwa anamaanisha?
 
Ndio taabu ya hawa Maprofesa kuingia kwenye siasa za chama kama CCM mwisho lazima ushikiwe akili na akina Nape!!!!
 
WanaMtwara waliahidiwa wakati wa kampeni za urais kuwa mitambo ya kufulia umeme wa gesi ingejengwa huko kwao; sasa kitu gani kimetokea hapo katikati mpaka ahadi hiyo kubadilika na badala yake WACHINA kupewa tenda kubwa ya kujenga mabomba ya gesi kutoka Mtwara na kuipeleka Dar es Salaam? Je inawezekana kuwa mradi huu wa mabomba ya gesi ulibuniwa kama njia ya kulipa fadhila kwa serikali ya China? Kama hivyo ndivyo hiyo fadhila inalipwa na hawa waongoza nchi kwa lipi ambalo serikali ya China imewatendea? Tafakali.
 
Prof wa madini atajulia wapi ishu za PR!huko ni kukurupuka,he is making things to become worse!hana wasaidizi wake wa kumshauri cha kuongea?better arudi akafundishe tu!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tusipende kuwa Wakomunisti wa maneno wakuu, alichosema Waziri ni sahihi. Nchi hii haina utaratibu wa ukanda au majindo, kwa hiyo kauli ya Waziri ni kuwakumbusha wakaazi wa Mtwara kuwa, kuna tofauti ya Korosho uliyolima na Gesi ambayo ni MALI YA ASILI.

Kuwa darasa la 7 haimaanishi kuwa huna akili, tazama wewe na madarasa yako umeshindwa kuelewa suala dogo sana. Waziri hafananishi usafirishaji, Waziri anahoji 'Korosho za Mtwara zinaenda sokoni, gesi ya Mtwara itashindwaje kwenda sokoni?' Shida ni kwamba unajaribu kutumia hisia kuelewa.

Haya anayoyasema Waziri Muhongo hata Zitto Kabwe aliyasema BBC (simaanishi hizo mnazoziita kejeli) kwamba kuna viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Halmashauri na Wabunge wa mikoa ya Kusini walipelekwa nje kujifunza mambo kadhaa juu ya gesi. Kama nia ni kuweka maazimio wazi kwa Wanamtwara, mbunge wa Mtwara mjini ambaye nasikia naye ni kinara wa maandamano, anataka kuieleza nini Tanzania juu ya ushiriki wake katika ziara na vikao hivyo?

Hata wewe nimekuwa na wasiwasi na uelewa wako, kama hujui tofauti ya korosho na gesi, pamba na dhahabu, mahindi/maharage na tanzanite!
 
Back
Top Bottom