Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo

Sjaiona tofauti bado kati ya huyu profesa na yule wa tanzania ni muungano wa visiwa vya pemba na zimbabwe aka hamimu
 
Mwandishi: Upi ni wito wako kuhusiana na vurugu, migororo?

Waziri: Kwanza naomba kuwaambia wananchi wa Mtwara, kuwa wasicheze ngoma wasiyoijua. Wasiimbe nyimbo wasizozijua wala hawajui wanaotunga tenzi za nyimbo hizo.

Labda serikali ndiyo imeanza kuimba nyimbo zisizoeleweka na wana Mtwara, labda haikuwajua wana mtwara na haikuwa tayari kuwasikiliza ili kuwajua...
 
Mimi kwa maoni yangu nafikiri suala la gesi mtwara linaendeshwa kisiasa sana. Ungeniuliza mimi ningekuambia suala la msingi ni jinsi gani mapato ya gesi yatawasaidia wana mtwara na wananchi wa Tanzania kwa ujumla. Issue sio wapi inazalishwa na wapi inapelekwa tunataka mapato ya gesi tu sio usafirishaji. Tatizo la Tz tunaanza mambo then sera baadae. Tungetakiwa tuwe na sera kwanza inayobainisha mgawanyo wa mapato ya gesi na rasilimali nyingine kama madini na mafuta. Tukiwa na sera imara na tukazitekeleza inavyotakiwa hutasikia mtu kusema sijui gesi izalishiwe Mtwara au isafirishwe mpaka Dar. We need equitable distribution of resources not transportation issue. We need to address the core problem with usage of natural resources in Tanzania. Had we formulated a balanced and equitable policy we could not have experienced North Mara or Kahama problems. Lets think aloud and come with solutions.
 
Ndio maana mvutano hauishi, kumbe waziri haelewi wanamtwara shida yao nini, inavyoonekana na wanamtwara hawamwalewi waziri, kazi ipo.
Hivi vikao vya posho tangu lini vikapeleka feedbacks kwa wananchi, wananchi hakuna wanalolijua sio tu kuhusu gesi hata hivyo vikao kama vilifanyika.
waziri hizi ndio kejeli wasizozitaka wana mtwara, Muhongo ni kati ya mawaziri niliyokuwa nikifikiri wana uwezo wa kufikiri kumbe naye bure tu, ulitaka walime korosho na wazile huko huko mtwara. Waziri hawana korosho tu, wana gesi pia, kaeni chini muwasikilize acheni kuwakejeli.

Nadhani Kejeli na Matusi yao tumeyachoka, na Kama alivyosema wao wana Polisi na JWT basi waje na waanze kazi ya kutuua ili pasiwe na wankuhoji juu ya udhalimu wao, Nadhani sasa wanatakiwa kujua Nguvu ya umma ni kubwa kiasi gani kwa sasa maana uelewa wa haki zao umekuwa mkubwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, Vurugu na Mikasa ya Masasi iwe Fundisho kwao maana mji mdogo kama masasi uliweza kufunga kituo cha polis na kusimamisha shughuli zote za Serikali kwa siku mbili na hadi sasa mambo hayajatulia maana hata wakianza sasa Mahakama zetu za Analojia sijui wataanzia wapi Nyaraka zote zimechomwa. SISIEMU tafakarini kasha chukueni hatua muafaka za kutatua matatizo ya wananchi na sio kutumia mabavu.
 
Back
Top Bottom