Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jan 28, 2013.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2013
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, amesema anawaeleza Watanzania kuwa, uchumi wa Dunia wa sasa ni wa ushindaji, hivyo "sisi" Watanzania tumetaka tuifanye Bandari ya Mtwara kituo kikuu cha utafiti na uendeshaji wa shughuli zote za gesi. Kwa hivyo, wawekezaji waliotaka kuwekeza wakiondoka, bandari ya Mtwara kutokana na sababu zozote za kushindwa utulivu wa kufanya kazi zao, watahamishia shughuli zao bandari za Beira au Mombasa.

  Mwandishi: Tatizo la wakazi wa Mtwara ni lipi?

  Waziri: Mimi sielewi, inabidi wao waulizwe. Watu wa Mtwara kitu walicho nacho haki ni Korosho... Hizo korosho ni mali zao kabisa, mbona hizo korosho zinasafirishwa? Watanzania tuwaulize kwa nini korosho zao zinasafirishwa kutoka Mtwara.

  Mwandishi: Huoni vyema nyie Serikali mkakaa na wananchi kutoa elimu kuhusiana na suala la gesi?

  Waziri: Serikali na TPDC tumefanya vikao vingi sana na viongozi wa Mtwara na Lindi... wakiwemo Wabunge wao hadi wale wa Halmashauri wamepelekwa nje ya nchi kujifunza umuhimu unaotokana na hiyo gesi asilia.

  Isitoshe, wananchi wa Lindi na Mtwara wamepunguziwa bei ya umeme... Je, wanavyounganishiwa huo umeme kwa bei nafuu kuliko wananchi wengine, hawajiulizi? Pili, vijana wao tumewachukua wanakwenda kusoma VETA...

  Mwandishi: Upi ni wito wako kuhusiana na vurugu, migororo?

  Waziri: Kwanza naomba kuwaambia wananchi wa Mtwara, kuwa wasicheze ngoma wasiyoijua. Wasiimbe nyimbo wasizozijua wala hawajui wanaotunga tenzi za nyimbo hizo.

  Pili, Watanzania wote kwa miaka mingi tumepata matatizo ya umeme, suluhisho la umeme linapatikana sasa.

  Shukrani za dhati ziende kwa wavuti.com kwa kuyaweka hayo mahojiano kwenye maandishi. Unaweza kumskiliza Mh. Muhongo mwenywe hapa: audio:-Kauli ya Waziri wa Nishati na Madini & Taarifa za habari Januari 27, 2013 - wavuti.com
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,310
  Likes Received: 13,657
  Trophy Points: 280
  Mkuu EMT, hili la Muhongo, naomba ni reserve comments to avoid conflict of interest, mimi kupitia PPR ni mdau wa TPDC na Wizara kwenye publicity, saa hizi tunajiandaa mkutano wa Gesi na Mafuta, tarehe 4 Feb. Mgeni rasmi ni JK.
  Ila ... yaani, wee acha tuu!
  P.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2013
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ndio maana mvutano hauishi, kumbe waziri haelewi wanamtwara shida yao nini, inavyoonekana na wanamtwara hawamwalewi waziri, kazi ipo.
  Hivi vikao vya posho tangu lini vikapeleka feedbacks kwa wananchi, wananchi hakuna wanalolijua sio tu kuhusu gesi hata hivyo vikao kama vilifanyika.
  waziri hizi ndio kejeli wasizozitaka wana mtwara, Muhongo ni kati ya mawaziri niliyokuwa nikifikiri wana uwezo wa kufikiri kumbe naye bure tu, ulitaka walime korosho na wazile huko huko mtwara. Waziri hawana korosho tu, wana gesi pia, kaeni chini muwasikilize acheni kuwakejeli.
   
 4. A

  AbasMzeEgyptian JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2013
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80


  Lakini AL HABIB PASCO wewe si unatumia nick name au ?
   
 5. A

  AbasMzeEgyptian JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2013
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
 6. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #6
  Jan 28, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hii ndo Tanzania, kauli ya profesa haina tofauti na kauli itakayotolewa na mtu wa darasa la saba! Ni jambo la ajabu sana kuona Waziri mzima, tena Profesa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu, anafananisha usafirishaji wa Korosho na usafirishaji wa gesi. Waziri Muhongo anataka kutuambia kuwa usafirishaji wa hiyo gesi uko sawa na namna korosho inavyosafirishwa kutoka Mtwara? Ama kweli dunia ina mambo! Yangu macho, ngoja tuone wanapotupeleka!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  goodness gracious....... Huyu jamaa anaweza kusema haya kweli??

  Imbechili
   
 8. m

  mahoza JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2013
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,236
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  mkuu Abas hapa tunachosubiri ni mkuu Pasco atuelimishe hatuhitaji nick name wala nini.mkuu Pasvo tunasubiri utupe taarifa zaidi maana huyo muhongo( a. k.a) muongo haelewi anachozungumza. kila la heri.
   
 9. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2013
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Ashakuwa Mateka wa mafisadi
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2013
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,914
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kwa miaka nane mfululizo nchi kama haina Rais!!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 28, 2013
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,160
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Na sisi wengine hatuelewi kwanini bado wako madarakani...
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  We may never find out why....
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  kama hajui sasa si akae kimya??

  anavyobwabwaja ndio anazidi kuharibu
   
 14. K

  Kalitike Member

  #14
  Jan 28, 2013
  Joined: Jan 3, 2013
  Messages: 90
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jk akiwaanamuachiachia huyu waziri aongeeongee ataharibu kabisa, yaani nje ya hayo ma jeolojia yake huwezi amini kama jamaa ni profesa inaonekana haelewi isues kabisa.
   
 15. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2013
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri nae haelewi teh teh teh! Wonders shall never end.
   
 16. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2013
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Maccm yamezoea ubabae na propaganda hata kwenye issue nyeti kwa kujiaminisha kuwa watz wote tu mazombi kama pasco, ritz, chama na Rejao!
   
 17. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2013
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 823
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hizi ndizo kauli ambazo hazitakiwi kabisa katika kutatua mgogoro hata wa ndoa tu. Ni dhahiri kwa kauli kama hii huwezi hata kidogo kupata muafaka. Ni kwa nini viongozi wetu wanjisahau sana? hivi ni lazima useme hayo, hakuna maneno ya kitaalam na weledi ya kuelezea watu wakaelewa ni lazima utumie vitisho? viongozi wetu naona bado wanaishi katika enzi nyingine kabisa. Mbona wanasafiri kila siku hawajifunzi kwa wenzao?
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 64,189
  Likes Received: 62,324
  Trophy Points: 280
  Hana tofauti na Mulugo. Anaongea kwa kiwango kinachokatisha tamaa kabisa hana hata uwezo wa kupanga hoja na huyu ndiye tuliyeambiwa kwamba ni kichwa. Anaendelea kutoa kauli zilizojaa vitisho. Serikali bandia, Rais bandia na mawaziri bandia.
   
 19. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2013
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  walijenga nyumba za mabati ila bado za ghorofa saba!
   
 20. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2013
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  ogopa profesa aliyezaliwia nyumba ya nyasi! ndio maana kauli zao zimekaa kinyasinyasi tuu!
   
Loading...