Sakata la DP World ni kipimo cha uzalendo. Tunawafuatilia viongozi wetu kwa ukaribu sana

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,896
3,206
Kama mzalendo katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliruhusu nizaliwe, naona kabisa kwamba hili suala la mkataba kati ya Serikali yetu na DP World ya Dubai, itakuwa kipimo cha uzalendo ambao tunapaswa kutumia katika kuwapima.

Tuko tunafuatilia kwa ukaribu sana maoni yenu.

Hata wale ambao mmeamua kuwa kimya au kutokuwa na upande, tunawa-zoom tu..

Kwanza kama kiongozi, sifa ya kwanza kabisa unapaswa kuwa jasiri ambaye uko tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya wale unaowaongoza. Ndo maana ukisoma vitabu vitakatifu ikiwemo Biblia, viongozi (Wafalme) ndo walikuwa wanakuwa msitari wa mbele kuongoza mashambulizi. Na viongozi wengi walikuwa wanapatikana kutokana na uhodari wao vitani. Sisi bahati mbaya sana tunaongozwa na viongozi waoga!!

Nimalizie kwa kusema kwamba, hili sakata la DP World, kama viongozi wetu hamtoliangalia kwa umakini na kufanya marekebisho pale yanapohitajika, basi mjue kwa hakika kwamba siku zenu zinahesabika na muda utasema.

Asalaam Aleykum.
 
Back
Top Bottom