Mi naona Pengo alifanya hivyo kupunguza hasira wakristu dhidi ya waislamu. Ikumbukwe baada ya lile tukio humu jamvini na mitaani, watu washajenga chuki na waislamu kitendo ambacho kingehatarisha amani. Mi binafsi na'pongeza kwa kuona mbali.
Sijui kwanini wakiristo hawa wa chini wasifate mawazo ya pengo kiukweli anaona mbali baadhi ya wakati
sio ponda kwasababu alikuwa jela akawa anaagiza wafuasi wake kufanya huo ugaidi
Tatizo lenu wengi hamtafakari matamko haya yanayotolewa kwa dhati. Mnachukua literally tu. Kardinali alichosema kilikuwa kinalenga kuonyesha kuwa wakristu na waislamu Tanzania hawana uadui. Waliofanya tenfo hili ni lazima wana nia ingine zaidi ya kuchonganisha uislamu na ukristu Tanzania. Alisisitiza taarifa sahihi matokeo ya uchunguzi, hii ni kutaka watu wasiendelee kuaminishwa kuwa kuna ugomvi wa kidini Tanzania.Bunge kwa upande wake wanaona dhairi kuna mmomonyoko wa mahusiano yanayosababishwa na kikundi cha watu kuuchochea ukristu na uislamu. Wanalenga Serkali kuchukua hatua stahili ikiwemo kutunga sheria. Kwa upande mwingine Bunge linailaumu serkali kwa kuzembea.Jana katika kujadiri azimio la bunge katika kulaani na kupinga kitendo cha kigaidi kilichofanywa na watu wasio julikana katika kanisa katoliki huko Arusha, wabunge wote bila kujari itikadi za vyama vyao wala imani zao za kidini walionyesha kuamini kuwa tukio hilo linatokana na imani za kidini kulaani na kuonya juu ya mtafaruku unaoendelea kujitokeza kati ya wakristu na waislam.Hii ni tofauti kabisa na tamko la kardinali Pengo ambaye kwa intelijensia yake ametamka kuwa shambulizi hilo alihusiani na na maswala ya kiimani.Lakini mimi naomba kujua, hivi msimamo wa bunge na tamko la Pengo haviingilii uchunguzi wa polisi?Hii ni kutokana na kwamba bunge lishajiaminisha na kuamisha watanzania walio wengi kwamba shamulizi hilo linatokana na mpasuko wa kidini unaolikumba taifa letu na huku Pengo kajenga imani na kuaminisha wengine kwamba shambulizi hilo halina mahusiano yoyote na maswala ya kiimani.Wakuu mie naona pande zote mbili yaani Pengo na bunge wamewahi mno kutoa kauli zao kwani polisi inaweza kuja na matokeo ya uchunguzi yakiwa kinyume kabisa na imani ya matamko yao, je watakubali?
Pengo ametumika kupoza upepo.
mbona baada ya tukio la Arusha matamko makali ya kukemea udini yanafuata.
kwa nini
Kuna haja ya kuwa na minimum qualification bungeni
Haya mambo ya maswali magumu kujibiwa na majibu mepesi inataka kuwa tabia zoelefu
kama polisi wanajua kazi yao barabara wanatakiwa wamkamate Pengo kama shahidi namba moja
Pengo ni mzoefu wa taratibu za undeshaji Serikali, na pia nadhani ana saikolojia. Hata mimi siamini kama tukio la ARusha ni kidini, na kama litakuwa la kidini litakuwa kosa kubwa sana kuwahi kutokea Tanzania kwa vile ni wazi kwamba "mbaya" wa waislam si wakristo, ni serikali yenyewe kupitia Bakwata, so hawawezi kushambulia watu walio kwenye ibada ilihali humo ndani yake kuna watoto, wanwake ambao uwezo wao wa kukimbia hatari ni mdogo. Siamni kama kuna muislam atakayekuwa na imani hiyo iwapo ni timilifu wa akili. Pengo yuko sahihi, lets wait!
Kongosho, tatizo tulilonalo hapa TZ kwa sasa ni kuwa siasa imeingilia kila kitu. Hakuna kitu cha maana kinachofanyika zaidi ya watu kuongea na kisha kuishia hewani.
Nikuulize swali la kipuuzi, ni tume ngapi zimeundwa kuchunguza mambo mbali mbali na zipi zimetoa matokeo yaliyofanyiwa kazi? Mangapi yanajadiliwa bungeni na ni mangapi yanatekelezwa? Juzi juzi tu jengo lilianguka na kutafuna makumi ya watu hupo kariakoo. Niambie ni hatua gani thabiti zimechukuliwa kufuatilia, kuchunguza na kuyabomoa majengo yenye sifa duni (chini ya kiwango)? Ni siasa, siasa siasa kwenye kila kitu!!!
Hao waloharibu vyanzo vya maji wako wapi? walioiba wanyama wamechukuliwa hatua gani? Wala rushwa? Richmond? Ile ishu ya jairo? nk nk. Ni siasa siasa siasa!!!