Sakata la Anerlisa na Ben Pol: Anerlisa atishia kumburuza Ben Pol Mahakamani, Ben Pol aomba kukutana na Familia

Gan star

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
380
980
Mwanadada na mfanya biashara Anerlisa , ametishia kumchukulia hatua za kisheria aliyekuwa mume wake, Ben Pol kutokana na madai kuwa amekuwa akimchafua kwenye mitandao ya kijamii. Anerlisa amepanga kumfikisha mahakamani mwimbaji huyo iwapo ataendelea kumtaja au kumhusisha kwenye mazungumzo yake au kwenye mitandao. Pia amemtaka amuombe radhi kwa kumchafua na kumpa siku 14 za za kutekeleza hilo. Taarifa hizo zimekuja baada ya kuvuja kwa barua ya mwanasheria iliyoandikwa kwa niaba ya Arnelisa kwenda kwa Ben Pol ambae hivi karibuni alifungua jalada mahakamani hapa nchini akiomba mahakama kuidhinisha kuachana kwao.

simulizinasauti_1619778115730903.jpg


simulizinasauti_1619778115730204.jpg


Kwa upande mwingine Ben Pol ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea duku duku lake kutokana na sakata Hilo...

Anaandika Ben Pol

TAARIFA,SHAURI LA TALAKA.
Ben Pol angependa kuthibitisha uwepo wa shauri la talaka dhidi ya mke wake linaloendelea katika Mahakama ya mwanzo hapa Dar es salaam. Mahakama bado HAIJATOA talaka/ maamuzi yoyote mpaka pale litakaposikilizwa na kukamilishwa. Masuala haya ni ya BINAFSI sana na kwa kuwa shauri linaendelea Mahakamani Ben Pol asingependa lizungumzwe zaidi kwa heshima ya pande zote na kwa kuheshimu kazi ya Mahakama. Pia anaomba nafasi na faragha kwake na kwa familia katika kipindi hiki kigumu. Anawashukuru wote kwa uelewa na pia kwa familia, marafiki na mashabiki wote kwa support mnayoendelea kuionesha. Uongozi wa Ben Pol.

KIMOMBO
By date: 29 April 2021 Headline: Ben Pol's divorce proceedings are ongoing. At this time, Ben Pol would like to confirm that his divorce proceedings are in progress at the primary court but have not yet been finalised. These proceedings are a very private matter and he will not discuss any details out of respect for all parties involved. He kindly asks that space and privacy be given to him and his family during these challenging times. He appreciate everyone's understanding and takes this opportunity to thank his family, his friends and his fans for their ongoing support. Ben Pol’s management

Soma pia

1. Ben Pol aomba Talaka Mahakamani dhidi ya Mke wake Anerlisa

2. Hatimaye Anerlisa asaini Hati ya Talaka iliyowasilishwa na Ben Pol Mahakamani
 
Wabongo bana kwa kidomo domo hatufai sasa Ben keshaomba talaka kakubaliwa si yaishe,hapo ndo kwanza alikua na mpango wa media tour kuongelea hio talaka,bora mkenya kamuwahi
 
Kwa hii kibri inaonekana binti ndie amempiga chini jamaa yetu.

Sio mbaya lakini.

Diamondi ndio anawaweza wanawake, yeye anawatwisha mimba tu anawaacha.

Mwanamke ukimtwanga mimba hata mkiachana bado lazima atakua na heshima na wewe maana ile heshima ya kumzalisha hua haiishi hadi mnakufa.

Sasa Ben pol atakua na kielelezo gani kua alikua anamtafuna yule mtoto?
 
Part 1 ya waraka wa wanasheria wa Anerlisa inasema "until you recently got divorced." Kwani talaka imeshakua finalized? Kwanini wao wanasema hivyo au kukosa umakini?
 
When love goes wrong nothing goes right. Coffee and love taste best when hot, vimeshapoa sasa tumeanza kuona mapicha picha.
 
Back
Top Bottom