Hatimaye Anerlisa asaini Hati ya Talaka iliyowasilishwa na Ben Pol Mahakamani

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,479
34,751
Hatimaye mwanadada mrembo na mfanya biashara maarufu tokea pande za +254 amefunguka na kudai ameshasaini kila kitu kilichomtaka yeye kufanya hvyo , na Kwa sasa anachoangalia yeye ni biashara zake na sio kitu kingine......

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi mei mwaka 2020 kwenye kanisa la St Gaspar jijini Dar es salaam na mapema mwez huu Ben Pol aliwasilisha Hati ya kuomba Talaka toka Kwa mke wake huyo katika mahakama moja jijini Dar es salaam ( jina kapuni)....


Hvi majuzi kamera za mapaparazi zilimnasa mrembo Anerlisa akiwa kwenye viunga vya jiji la Dar es salaam na bila Shaka alitua kukamilisha swala Hilo ...

IMG_20210428_182259.jpg


Katika hatua nyingine , kuna tetesi na nyepesi nyepesi zinazodai kuwa Ben Pol amemtuhumu nyota wa bongo fleva na Mla bata maarufu mjin Omy dimpoz , almaarufu kwa jina la Omy Kwa Poz kuwa anatoka na Mke wake huyo, na huenda ni moja ya sababu ya Ben Pol kuamua kujikata, huku akionesha kumponda Omy dimpoz ya kwamba hana kizazi.

IMG_20210428_190742.jpg
 
Back
Top Bottom