Sakata la Adamu Mchomvu na Mbasha

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,429
2,000
SAKATA LA MITAMA YA ADAMU DHIDI YA MBASHA

Na, Robert Heriel

Tamasha la CCM lilikuwa la kuvutia sana, lilichangamsha washabiki wa sanaa waliohudhuria katika uwanja wa Uhuru na wale tuliokuwa tunafuatilia live kwenye onlineTv, na wengine waliokuwa wakifuatilia kwenye Channel Luningani.

Kama sikuwapongeza waandaji wa Tamasha hilo, na CCM basi nichukue nafasi hii kuwapongeza. Watu walifurahi, waliopata hela walipata, basi mambo yalienda sawa.

Lakini Dosari ilijitokeza pale ambapo Adamu Mchomvu alipombunda mtama Mbasha. Dooh! Ilikuwa ni aibu sana. Binafsi sikutegemea kama jambo lile lingefanyika.

Wapo waliomsifia Adamu Mchomvu na Kumponda Mbasha, lakini pia wapo walikuwa upande wa Mbasha wakimponda Adamu mchomvu. Basi kila mtu na mtazamo wake na ufikiriaji wake.

Mimi nitakuwa upande wa Mbasha, Kwa nini?

Mbasha na Adamu wote ni vijana wanaokaribia utu uzima.

Vijana sisi tunalugha zetu, tuna misemo yetu, tuna matani yetu, tuna namna tunavyoishi ili kusukuma maisha yaende.

Sikuona kosa la Mbasha kumuita Adamu ni "bange'' Tena hata mimi Taikon mtu akiniita Bange sioni shida ikiwa anachokisema sio kweli na hakina Madhara.


Neno "BANGE'' maana yake ya msingi ni mmea ambao majani yake hutumika kutengenezea madawa ya kulevya yaitwayo bange. Hiyo ndio maana ya msingi ya neno hilo.

Lakini kuna maana za ziada, kwa sisi wana lugha tunajua maneno huweza kuwa na maana zaidi ya moja mbali na maana ya msingi.

Kwa mfano Neno "Simba'' maana yake ya msingi ni mnyama jamii ya paka alaye nyama aishiye mwituni. Lakini Simba huweza kutumika kama mtu mtawala, mwenye nguvu, mfalme. Hata Yesu alijiita Simba wa Yuda bila shaka akirejelea Maana ya '' mfalme wa Yuda''

Mfano wa Pili ni "Jiwe'' ambalo maana ya msingi ni madini aina ya chuma yapatikanayo ardhini. Lakini maana ya ziada ni kuwa kitu kigumu, kitu kisicho yumbishwa wala kutetereshwa, kitu ambacho ni mhimili. Wapo watu wengi waliojiita Jiwe, Hata Yesu alijiita Jiwe Kuu la pembeni, pia kama sijakosea Mhe. Rais naye aliwahi kujiita Jiwe, akirejelea maana hizo nilizozitoa na nyinginezo ambazo sijazitoa.

Kila mfano una upande hasi na upande chanya. Hivyo inategemea na akili ya mtu atakavyotafsiri

Mifano ipo Mingi, mtu kuitwa jina fulani inategemea na matendo yako au unavyoonekana. Inaweza kuwa ni utani au kweli.

Kwa mazingira ya Adamu na Mbasha ni wazi kuwa yalikuwa mazingira ya furaha, burudani, mazingira ya utani, basi tuu watu wafurahi. Mbasha alimtania Adamu, kwa misingi ya matani lakini nafikiri kwa kadiri anavyomfahamu.

Kutumia neno Bange kwa muktadha wa siku ile, usingeleta athari yoyote kwa Adamu. Ilikuwa ishu ndogo mno. Kwani kila mmoja angejua ni masihara tuu.

Mtu akikuambia kichwa chako ni bange, au wewe nawe ni bange, atakuwa na maana zifuatazo; Mosi, wewe ni waruwaru, wewe umechangamka sana, mtu ambaye hujatulia, mtu mchapakazi, mtu jasiri asiye na aibu, mtu mwenye maamuzi pasipo kushirikisha akili yake n.k

Sasa inategemea umechukua maana ipi.

Mimi ningeweza kusema kuwa Mbasha alimtania Adamu akimaanisha, Adamu ni mtu aliyechangamka sana, na mtu mchapakazi.

Nipo upande wa Mbasha kwa sababu, Mbasha hakuwa na dhamira mbaya, na hii tunaiona hata baada ya kupigwa mitama alijikausha tuu, kama Mbasha angekuwa amedhamiria toka moyoni basi ule ungekuwa ugomvi mkubwa.

Adamu kakosea kwa sababu hakupaswa achukue maamuzi ya namna ile. Yale ni maamuzi makubwa sana. Kumpiga mtu hadharani kisa utani tuu ni jambo ambalo sio la kiungwana.

Adamu sio kwamba hajui maneno ya mtaani, maneno ya vijana, anajua lakini Alikosa utulivu na hakuipa akili yake nafasi ifanye kazi, aliruhusu mihemko.

Mbasha huenda alikosea lakini kiukweli hakukosea pakubwa kama watu wanavyotaka kuaminisha Umma.

Adamu ndiye kajiaibisha kwa kudhihirsha maneno hasi ya neno bange,Alichoonyesha ndio bange yenyewe, yaani upande hasi wa Bange.

Adamu kadhihirishia Wote waliopata kuangalia tukio lile kuwa yeye hana subira, hana hekima, hajui namna ya kutatua migogoro, anapenda kukuza mambo, hawezi kutawala hasira yake, wachache ndio watamsifu lakini wengi hasa wenye akili na wenye nafasi nzuri kimaisha watamuona kama mtu asiye mstaarabu.

Kama Adamu alitaka kulimaliza palepale asingepaswa kumpiga, angemuambia Mbasha aombe radhi palepale na akanushe maneno yake, au Mbasha ampe maana ya kile alichokuwa amemuambia. Lakini kumpiga haikuwa suluhu zaidi ya kuonyesha Bange zenyewe kwa upande hasi.

Mwisho niseme, Pongezi kwa Msemaji Mkuu wa Serikali Mkuu wa serikali kwa kuwapatanisha vijana hao. Ni jambo nzuri sana. Lakini nitoe wito kwa Watanzania kuwa, tuangalie namna tunavyotoa maamuzi yetu pale tunapokuwa na hasira. Lakini pia kwa wale wapenda utani, tuangalie watu wa kutania kwa maana wengine hawajui hata maana ya utani.

Robert Heriel
Taikon waFasihi
0693322300
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
4,628
2,000
Msemeji mkuu wa serikali amekwishalimaliza japo Mbasha ni wazi hakuridhika lakini the case is closed, anayebisha aka appeal.
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,501
2,000
Mbaya zaidi haikuishia pale stagini tu adam still alimfata mbasha backstage akataka kumpiga watu wakaingilia kati wakamshika adam wakamvuta pembeni
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,429
2,000
mbaya zaidi haikuishia pale stagini tu adam still alimfata mbasha backstage akataka kumpiga watu wakaingilia kati wakamshika adam wakamvuta pembeni


Adamu hakuwa na sababu ya kufanya hayo yote, ukimuuliza hata sasa hivi alifanya yale kwa faida ipi mwenyewe hatajua ajibu nini.

Alikuwa chini ya mihemuko ya kijinga tuu
 

Elevat Kapela

JF-Expert Member
Dec 9, 2017
519
1,000
Ni rahisi sana kuwa na hekima na busara kama tukio limetokea kwa mwenzio!

Wewe mwenyewe umesema bange maana yake yaweza kuwa waruwaru. Je unadhani kuitwa waruwaru ni jambo la kheri.

Halafu Adam Mchomvu ame- make headlines za mitandao ya kijamii hadi kijijini kwetu Ipondamafulela wanamjadili kuliko kusudio la hilo tamasha!

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
3,522
2,000
Walikuwa wanajaribu kutengeneza Kiki lkn naona imegoma Lissu yupo mby sasa anachanja mbuga
 

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,529
2,000
Mfano uwe chongo mtu akuite hadharani kwamba wewe chongo utafurahi kweli? Vivyo hivyo uwe mvuta bangi mtu akuite mbele ya halaiki ya watu kwamba wewe bangi (bange) hautafurahi. Lazima utahamaki sana hali ambayo ni tofauti kama siyo mvutaji.
 

EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
4,882
2,000
Mbasha ni nabii alitabiri mchomvu ni bange na kweli tukaziona bange live jukwaani
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,429
2,000
Mfano uwe chongo mtu akuite hadharani kwamba wewe chongo utafurahi kweli? Vivyo hivyo uwe mvuta bangi mtu akuite mbele ya alaiki ya watu kwamba wewe bangi (bange) hautafurahi. Lazima utahamaki sana hali ambayo ni tofauti kama siyo mvutaji.
:D :D :D :D :D :D

Ndio maana nikasema Adamu amekosea maana kwa kumpiga mitama mwenzake ndio kunadhihirisha yeye ni Bange kweli kuliko angekaa kimya.

Sasa vile alivyofanya ndio kaharibu zaidi maana ametoa ushahidi ya shutuma alizopewa:D:D:D:D
 

orturoo

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
1,630
2,000
Mods izi nyuzi za Adam na mbasha zitawajazia server zifuteni, wameshajidhalilisha inatosha
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,771
2,000
Ndio kina nani hao Adam Mchomvu na huyo Mbasha naona storiii ndefuu utadhani wote tunaishi huko dar.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom